Usikubali kufia hapo

Eliah Geofrey Kamwela

Senior Member
Joined
Dec 30, 2018
Posts
185
Reaction score
511
USIKUBALI KUFIA HAPO!!!
Kwamba upo unasoma Ujumbe huu sasa ni ushahidi kuwa bado upo hai, na kama bado upo hai , basi u miongoni mwa wenye Bahati sana , kwa kuwa uhai una thamani kuliko chochote!!
Chukua kioo, halafu angalia unacho ona ndani yake! Huyo mtu unaye mwona, Mungu amewekeza vikubwa mno ndani yake. Anaweza kuwa hajui au hahisi hivyo kwa kuwa anayo pitia ni magumu kiafya, Kiuchumi, katika ndoa na familia nk. Lakini, hata kama dhahabu haijijui kama ni dhahabu, hii haiondoi ukweli kuwa hiyo ni dhahabu, ingawa isipo jitambua itaishia kuchezwa bao!

Usifie hapo ndugu! Yale ambayo Mungu ameweka moyoni mwako kuyafanya ni halisi, hakikisha yanatokea! Kuna ugumu hutokea unao shawishi watu wafanye mambo marahisi na waache Yale sahihi walio paswa kuyafanya!!
Tafadhali usiwe mmoja wao.
Inuka,
Jikung'ute ,
Songa mbele, ushindi ulipo .
Mungu akubariki.
#Divine_Solutions_Carrier
 
Sawa mkuu asante kwa nasaha nzuri,japo katika utafiti wangu usio lasimi nimegundua kuwa wanaotoa ushauri mubashara kama huu,mala nyingi wao si watekelezaji wa wanachokishauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…