USIKU WANGU HUU! (shairi)

Swahilian

JF-Expert Member
Apr 28, 2009
591
66
Usiku wangu umefika' natamani pale n'geshika'
Usiku wangu huu aah! nsingetaabika'
Moyo wangu huu! usingehuzunika'
Ningefika wakati huu aah! nsingechoka'

Ndoto yangu hii! lazima ingetimilika'
Lakini mmh! hakika nataabika'
Pangu pakavu pa mwenzangu patiririka'
Wale wanapeana huku wanacheka'

Kesho hivyo hivyo hadi kumwagika'
Usiku wangu huu! sijui nami ntaota na kuokoka'
Labda weye mwenzangu usiku wako ni sawa na huu!
Au weye ndo kuukuu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom