ng'ombo
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 418
- 619
Binti mmoja alikuwa akiendesha gari akiwa na baba yake. Wakiwa njiani ghafla mvua kubwa ikaanza kunyesha na kuleta tufani, yule binti akamuuliza baba yake, "Nifanyeje?"
Baba yake akamwambia "endelea kuendesha"..
Magari yakaanza kusimama na kuegesha pembeni kwa kuhofia tufani ambayo ilikuwa kubwa mno.
"Nifanyeje?."
Binti akamuuliza baba yake?
"Endelea kuendesha," baba yake akajibu.
Mbele yake tena akaona malori makubwa kabisa yakiegesha pembeni.
Akamwambia baba yake, "Inabidi nisimame, angalia hata magari makubwa yanaegesha pembeni na sioni vizuri mbele. Hali ni mbaya sana!"
Baba yake akamwambia, "Usikate tamaa, wewe endelea kuendesha!"
Tufani sasa ilizidi, lakini yule binti hakusimama na mara akaanza kuona japo kwa shida kidogo mbele yake. Baada ya umbali mrefu akajikuta yuko kwenye ardhi kavu ambako hakukuwa na mvua, na jua lilikuwa linaangaza.
Baba yake akamwambia, "Sasa unaweza kusimama na toka nje."
Binti akauliza "Kwanini sasa?"
Baba yake akamwambia "Ukitoka nje, tazama nyuma ili kuangalia watu waliokata tamaa na bado wako katikati ya tufani, kwa sababu hukukata tamaa tufani yako imekwisha sasa."
Huu ni ushuhuda wa kila mmoja wetu ambaye anapitia kwenye "tufani na dhoruba nyungi za dunia."
Siyo kwa sababu kila mmoja, pamoja na wenye nguvu, wanakata tamaa haimaanishi hata wewe pia ukate tamaa. Kama utaendelea kupambana na kusonga mbele dhoruba yako itakwisha na jua litakuangazia nuru yake usoni kwako tena.
Habari hii imenigusa na niaamini hata wewe imekugusa!
Mweleze mtu yeyote anayepitia kwenye magumu.
Mwambie: "Asikate tamaa, maana MUNGU hatakata tamaa katika kukutetea. Yeye hashindwi, hasinzii wala halali mpaka utakapopata haki yako. Inaweza kuwa unatafuta kazi mpaka sasa haujapata, umri unaenda ujaoa au ujaolewa, umejaribu kila aina ya biashara hakuna mafanikio, matatizo ya kifamilia n.k.
Sikiliza Sauti ya Mungu nasi tutayavuka majaribu ata kama ni magumu kiasi gani.