Usikate tamaa wakati unatafuta

Usikate tamaa wakati unatafuta

ikersmn

Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
18
Reaction score
16
Maishani ni jambo jepesi sana kukata tamaa tena endapo umeshajaribu jambo fulani mara nyingi na likaleta matokeo hasi. Mara nyingi tunakumbwa na hisia za kuliacha jambo hilo bila kutafuta mbadala au njia ya kusahihisha makwazo yanayotuzuia kufikia malengo yetu. Hapa nazungumzia vitu tunavyovifanya na vyenye tija kwenye maisha yetu mfano biashara, kazi, ideas mbalimbali zenye manufaa ya baadae, kutafuta kazi etc etc

Mfano halisi kwa sasa vijana wengi tumekua tukikata tamaa katika kazi zetu au bishara tunazoanzisha kwa sababu mbalimbali lakini sababu nyingi zimevaa sura ya kukata tamaa inayozaa malalamiko na sababu zisizo za msingi zinazotufanya kuacha shughuli hizi na kurudi nyuma bila kujali ni hatua gani umefikia, ni jambo gani lingeweza kufanyika kunusuru biashara yako au kazi yako.

Maswali ya muhimu ya kujiuliza kabla hujakata tamaa au kuacha kabisa kulifanya jambo fulani (kama vile kazi yako, biashara yako, kutafuta kazi, kuanzisha biashara au kuendeleza wazo zuri lenye tija):-
- Je, unajua jambo hilo linafanyikaje, je unatumia njia sahihi (jifunze, tumia njia sahihi na ongeza ujuzi)
- Je, kuna faida au hasara kwenye kuacha jambo hilo (kama kuna faida endelea kupambana)
- Je, jambo uliloliacha bado unaliwaza kichwani (kama ndio komaa na jambo lako; "Mt 6:21 For where your treasure is, there your heart will be also")
- Je usipolifanya jambo hilo kuna mbadala wake (kama hakuna komaa)
- Je, umekumbana na vikwazo usivyoweza kuvitatua (shirikisha watu, tafuta msaada kwa waliowahi kufanya jambo hilo au linaloendana, usifiche matatizo au kuyakimbia tafuta suluhisho)
- Je, kunawaliowahi kufanikiwa katika jambo hilo (kama ndio, tumia njia waliyotumia wenzio au boresha panapostahili, kama wameweza wengine na wewe pia unaweza tegeneza njia yako)

Kama ushauri wa jumla kwa wapambanaji wenzangu, tuzingatie pia yafuatayo kabla hujafikiria kukata tamaa katika jambo lolote unalolifanya, na kweli utaona mwana na utafanikiwa:-
- Tumia muda mwingi kujifunza juu ya jambo unalotaka kulifanya (kuna msemo mmoja wa ughaibuni unasema "repetitio est mater studiorum" maana yake repetition is the mother of study)
- Kama ni muumini wa dini yoyote fanya sana ibada utafanikiwa
- Tambua mshindani wako ni nani na uwe bora zaidi
- Tambua uwezo wako na ufanye kazi ukizidi kujifunza usichokifahamu, usichoke kijifunza
- Watumie sana watu na usijifunge; watu ni rasilimali muhimu sana kuliko kitu chochote
- Ni wakati mzuri wa kuwa na mpango 'plan' na kuchukua hatua na kuweka mikakati ili uweze kufanikiwa
- Tumia sana vizuri rasilimali ulizo nazo .. fedha, muda ..... usipoteze muda wako au fedha kwa mambo yasiyo ya msingi etc

Kama una la ziada tiririka na uzi.. Nawatakia mapambano mema vijana.. TUSIKATE TAMAA
 
Soma au sikiliza
Msanii: Maino ft T-pain
Nyimbo: All the above
Mwaka: 2009

Usikate tamaa.
 
Nadhani watu hawakati tamaa bali hukatishwa tamaa, unapasuka kichwa kupata mtaji, unaanzisha kijimradi ambacho lazima uwe na vibarua, bahati mbaya hawazingitii matwaka yako... Loss juu ya loss... Unaamua kufunga mradi.

Unapiga kazi miaka nendarudi, hakuna nyongeza ya mshahara, gharama za maisha na madeni vinakupasua kichwa... Unawaza mara mbilimbili, unaquit for better opportunities.

Unampenda mwenza wako na kuwajibika ipaswavyo kiasi cha kuacha kunywa soda njiani ili pesa ikafanye jambo la pamoja nyumbani, kumbe mwezio ni careless full michepuko... Unambwaga

Anyway, kukata tamaa ni dhambi. Ukiwa mwepesi wa kukatishwa tamaa ni rahisi kujitoa uhai...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom