Usikate Tamaa kuna Mtu anakutegemea

Amen Kaka, naona wakati ule uzi kule unatiririka kuna wenzetu wamekata tamaa, tusimuache mtu nyuma! Leo nimepiga za Makete, Ukungu mtupu
Haha nzuri hiyo, Nyuzi kama hizi ni muhimu sanaa hasa kwa jamii zetu ambazo changamoto za kimaisha zinatukabili kila kukicha, kuna muda unaweza ukatamani kurudi nyuma, lakini kupitia nyuzi kama hizi kiukweli wengi wanaweza kuregain ile energy na spirit ya kupambana.
 
Amen, MUNGU atupe uzima tuweze kuandaa hata ka tour kamoja tu kakumaliza mawazo kidogo, wenzetu wanakua na RETREAT nadhani majority tunahitaji Retreat, ngoja kesho nitaanzisha mada hio
 
Mkuu umetembea mulemule kwenye hisia zangu hasa ukifikiria kwa sasa kazi sina,mpenz wangu kanisaliti yaani kiufupi full stress ila naamini yote yatapita japo nikipindi kigumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app

Mpwa wala usijali, Mabaharia tupo pamoja nawe, MUNGU anakuona, yeye ndio dhaifu ulimwamini akavunja trust, yeye ndio atakua haunted daima, na natabiri leo hii kuwa ATAKUJA KURUDI KWAKO KWA MACHOZI

 
Mkuu elli asante kwa uzi mzuri,kuna wakati waweza jiuliza nimekosea wapi!!maana kuomba Mungu unaomba sana lakin mambo hayaendi.Hamna kipindi kibaya kama kudharauliwa na kukimbiwa na watu wako wa karibu.
 
Mkuu elli asante kwa uzi mzuri,kuna wakati waweza jiuliza nimekosea wapi!!maana kuomba Mungu unaomba sana lakin mambo hayaendi.Hamna kipindi kibaya kama kudharauliwa na kukimbiwa na watu wako wa karibu.
Ngoja nikwambie kitu, Mkulima mmoja alikua na Punda wake, yule Punda alishamzalishia yule Mkulima kwa kipindi kitrefu sana hadi kuzeeka, kwa bahati mbaya wakati wanarejea nyumbani kutoka shamba mchana wa jua kali, walipokaribia jirani na nyumbani kutokana na uchovu pengine, Punda aliteleza akadumbukia kwenye kisima mabcho kilikua haikutumiki tena.
Mkulima kaanza kuwaza kuwa gharama za kumtoa mle kisimani zingekua kubwa ukilinganisha na ukweli kuwa Punda alikua ameshazeeka na hivyo thamani yake ilikua ndogo mbele ya macho ya mkulima, Majirani pia walikuja wakaanza kumshauri kuwa ni heri wamzike tu mle mle kisimani akiwa hai maana hata kisima chenyewe hakitumiki tena.

Punda kusikia vile aliumia sana, sio kwamba aliumia kwasababu ya kile kilichikua kinakwenda kutokea bali alihisi uchungu mkubwa wa kuwa REJECTED, DENIED na Rafiki ambaye waliishi muda mrefu kama ndugu. Akatafakari sana huku akiiona mauti hii hapa, PUNDA hakukata tamaa, alijiongeza, wakaanza kurusha mawe kisimani kwakidhani ndio wanamzika Punda, Punda akayatumia mawe yale kukanyaga na kupanda juu, kila jiwe, uchafu, takatata, udongo uliporushwa shimoni alipata maumvivu kidogo lakini ajitikisa akapanda juu tena, mwishoni akajikuta yuko juu akatoka akiwa mzima.

I challenge you today, usiumie kwa ajili ya maneno, rejection na mengine, tumia hizo kama njhia za kukufanya ufukirie zaidi, wewe sio punda ila unja akili zaidi ya Punda, maneno yao, kejeli, dharau na mengine kama hayo, kayafanye yawe chachu na msingi wa kukusimamisha kwenye lengo lako.
shida yako ndio kisima chako, suikubali ubakie kisimani, tafakari, tulia, Muombe MUNGU utashinda, kiri kwamba wewe ni mshindi.

 

Ujumbe mzuri sana
 
Hayo maneno ya usikate tamaa kunamtu anakutegemea kila siku huwa yanaishi kichwani mwangu kuna mtu aliniambia kuwa nikifanikiwa mm kuna watu pia wamefanikiwa bila mm kufanikiwa basi nawao hawata fanikiwa mlango wao wamafanikio mm ndio ninafunguo yao 😢
 
Yapo mambo katika maisha yana huzunisha sana na kukatisha tamaa haswa ila sio wote watakaoelewa maisha unayopitia thanks God kuna watu bado wana moyo wa kusaidia.Kwa niliyoyapitia ni kusudi la Mungu kuniinua kuniweka mahala pa juu
 
Yapo mambo katika maisha yana huzunisha sana na kukatisha tamaa haswa ila sio wote watakaoelewa maisha unayopitia thanks God kuna watu bado wana moyo wa kusaidia.Kwa niliyoyapitia ni kusudi la Mungu kuniinua kuniweka mahala pa juu
Tushirikishane tu ndugu hata kama ni private
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…