Usiizungumzie Teknolojia bila kuwataja hawa

Adil_101

Senior Member
Jul 26, 2022
110
339
Majuzi Alhamis wakati napita pita huko Quora,nilikutana na post iliyokuwa imeandikwa (katika mtindo wa swali) kwa maneno yenye weusi mkolezo, kilichonivutia na kuukonga moyo wangu, ni utamu wa swali hilo,hakika lilinifikirisha.

Basi bwana, swali lenyewe lilikuwa linasomeka hivi, “If the internet, computers and phones disappeared tomorrow, how would you spend your days?”

Safari ya mawazo yangu yaliyokuwa yakielekea katika kulisaka jawabu la swali hilo, ilitamatishwa na comment ya kwanza ktk post hio ...

… iliyokuwa imeandikwa na Macintosh Consultant (1990- Present), Mr Bradley Ditcher ambayo ilikuwa ikisomeka…
“Eating, Sleeping and doing jigsaw puzzles”.

Naamua kuliheshimu Jibu la Bradley, kwasababu alijijibia yeye kama yeye, lakini Uzuri wa swali husika ulinifanya niikumbuke ile habari ya “Fathers Of Technology”.

Kabla sijafika mbali, acha nitanabaishe mapema kuwa, naheshimu sana michango ya baadhi ya wanasayansi wakubwa katika nyanja mbalimbali zinazogusa maisha ya watu ulikwenguni kote, …. lakini sote si tunajua kuwa hata baharini samaki wapo wengi lakini anayesikika siku zote ni papa peke yake!!!, hivyo basi ni dhahiri kuwa kuna watu wana mchango mkubwa sana kwenye masuala mazima ya Teknolojia japokuwa hawasikiki na kupewa heshima inayostahili.

June ya mwaka 2012, jarida maarufu la masuala ya Teknolojia, “BizTechMagazine” lilichapisha makala iliyokuwa na kichwa kikubwa kilichokuwa kikisomeka, “Fathers Of Technology: 10 Men Who Invented and Innovated In Tech”.

Kwasababu jamii haiwapi-airtime ya kutosha, acha leo tuwape shout-outs kadhaa hawa wazee, Waliupigaga Mwingi.

Kabla haujazama kabisa katika hili wingu la huu uzi, yazingatie haya:-

1. Mpangilio wa namba katika kutaja orodha ya hawa jamaa, hauna uhusiano wowote na uzito wa ugunduzi wao.

2. Ugunduzi wa hawa jamaa, ni hususan, kwenye masuala mazima ya Information Technology (IT) tu.

3. Orodha hii ni kwa mujibu wa jarida nililokutajia hapo awali, na si vinginevyo.

Are you ready!!?, Haya sasa ni Muda wa Ku Flow na uzi Mwanana Kutoka Kwa "The one and only Adil"

1. Douglas Engelbart
(Human-Computer Interaction Whiz)
Chukua time yako, Nenda Google halafu u-search, “Who Invented Mouse?”, ukipata jibu, usione aibu Kurejea na kulisoma hilo jina vizuri, Muite Douglas Engelbart.

Lakini unajua nini!!?Ugunduzi wa Mouse, ilikua ni sehemu ndogo sana ya project ambayo yeye aliipa jina la “The oN-Line System”.

Katika tukio lile la 1968, pale Fall Joint Computer Conference, San Francisco, ambalo wengi. Wakaliona jina la “The Mother Of All Demos”, kwani ilikua ni ugunduzi wa NLS, ulio jumuisha vitu kama Packed video conferencing, networked collaboration, the mouse, hyperlinks na text editing into one presentation.

Vyote hivyo, yalikuwa ni matunda ya akili ya Douglas.

2. Norman Abramson (Wireless Hero).
Pale maeneo ya Hawaii (USA), sio tu ni pazuri kwa sababu uwepo wa fukwe hizo zinazopendeza katika kila mboni ya jicho la mtalii afikaye hapo ili kubarizi hususani katika nyakati za kiangazi, lah hasha.

Jambo jingine tamu kuhusu Hawaii, ni kuwa ndio pahala ambapo Wireless LAN Technology iligunduliwa na Norm Abramson, wakati alipokuwa ni Mwanafunzi “The University of Hawaii”.

3. Gerald A. Lawson
(Gaming Champion).
Gerald ndio mtu wa kwanza kutengeneza video game system (The first cartridge-based video game system), ambayo ilikuwa ikiitwa “The Fairchild Channel F”.

Baada ya ugunduzi huo tu, ndipo suala zima la video games likapata sura mpya katika ulimwengu huu.

Mifumo ya mwanzoni kabisa ya hizi video games kama ile ya The Atari 2600, The original Nintendo Entertainment System, The Sega Master System,yote ilikua ni kazi zake huyu Jamaa.

Inasemekana mwana alishindwa kwenda Mjini ipasavyo kwasababu ya rangi yake, kwani alikua ni Black Man, Hivyo wazungu hawakumpaga Mileage ya kutosha.

4. Robert Metcalfe
(Ethernet Impresario).
Kama Umeshawahi faidika na chochote Kuhusu Ethernet Cables, iwe ni aidha uli share files fulani, au kama uli jipatia internet access, chukua time yako kumshukuru ya Mzee, Robert Metcalfe.

Safari yake ya ugunduzi huo, ilianzia pindi alipokuwa alifanya Ph.D. research yake, pale University of Hawaii, ambapo alikutana na vijana wa Norman Abramson, na kutazama nini walikuwa wakifanya, Kisha Akaondoka na Ujuzi kidunchu, naku uhamishia kwenye Kampuni ya Xerox.

Na hatimaye, Mwaka 1975, Ethernet Patent ilizaliwa pale Xerox PARC Lab, huku akiwataja David R. Boggs, Charles P. Thacker, Butler W. Lampson kama co-inventors.

5. Tim Berners-Lee
(Web Master).
Ingekua haina maana kama tungezungumzia Teknolojia kwa Ujumla, halafu tukaacha kulitaja jina la huyu bwana, Tim Berners-Lee, Mgunduziwa World Wide Web (WWW).
Pale European Particle Physics Laboratory at CERN ndio chanzo cha haya yote.

Ambapo Berners-Lee aliandika Ki Memo kwa wakubwa zake wa kazi, akipendekeza kuwepo kwa “Global Hypertext System”, lakini wazo hili hapo awali lilidondokea Kwenye Masikio ya viziwi.

Baadae alipewa go-ahead, na kisha akakabidhiwa Computer chache za NeXT kwa ajili ya Practical, na hatimaye 1991, Berners-Lee akatuletea WWW duniani.

Nimeshachoka kuandika uzi huu, ila wagunduzi wengine pia ni kama Dr. Fujio Masuoka (Flash Man), Mgunduzi wa Hizi Flash, Ken Thompson (OS Virtuoso), Huyu ndio Mfalme, Operating Systems, Marty Cooper (Mobile Magician), na Jack Nilles (Telework Titan).

Nisamehe kwasababu sijapata muda mzuri wa kukuelezea hawa wa niliowataja mwishoni mwishoni walifanya nini, kwasababu nimechoka kuandika uzi huu.

Ila ninachoweza Kusema ni kuwa, “BizTechMagazine” sio wajinga kuwaweka hao jamaa kwenye listi, mimi pia sio mjinga mpaka nikakuletea huu uzi wa hawa jamaa, lakini wewe pia unaweza ukawa sio mjinga kwasababu unaamini kuna watu walitakiwa kuwepo hapo na haujawaona.

Sasa Mawazo ya kila mtu yaheshimiwe au sio?

Enewei, Ninachoweza Kusema Ni Kuwa, hawa miamba ni wali jenga msingi mkubwa sana kwa ajili ya hao wengine unaodhani walikuja kuendeleza hii tasnia kwa Upana wake huo, Em Mfikirie huyo Mzee ambaye alitengeza OS, alipinguza mzigo kiasi gani kwa watu kama kina Zuckberg!!?

Lakini pia, hii ni Upande wa Technology tu, usichanganye na Mambo ya Sayansi hapa.

Listi hii ni Upande wa wanaume tu, ila unapaswa kujua pia Kuna Listi ya “Mothers Of Technology”, ambayo nitakuletea soon.

Kama ambavyo unaweza ukaongeza majina ya wengine hapo chini Kwenye sehemu ya comment, ambao unadhani wali deserve kuwepo kwenye hii listi.

Kauzi Ka Adil, Si Kame Flow!
Picha Zipo kwa mpangilio Wa Events.
IMG_20230422_121721.jpg
IMG_20230422_122426.jpg
IMG_20230422_122524.jpg
IMG_20230422_122621.jpg
IMG_20230422_122651.jpg
IMG_20230422_122727.jpg
IMG_20230422_122843.jpg
IMG_20230422_122937.jpg
 
Umetaja watu halafu umewacha William Shockley, John Bardeen na water Brattain ambayo walibuni transistors.

Transistor ndio msingi WA computing devices zote tunazotumia sasa.

Halafu MTU Kama Robert Noyce inverttor WA integrated circuit kitu ambacho kimesaidia vifaa vya kompyuta kuwa ni vidogo mpaka vingine tunatembea navyo kama smartphone.

Hivyo vyote ulivyovitaja visingewezekana bila gunduzi ya transistor
 
Hivi umesoma kilicho andikwa mpaka mwisho au unajiletea critques zako zisizo na msingi...
.
Kama umesoma mpaka mwisho basi ungekutana na maneno haya hapa
.
"Kama ambavyo unaweza ukaongeza majina ya wengine hapo chini Kwenye sehemu ya comment, ambao unadhani wali deserve kuwepo kwenye hii listi."
.
Ila tatizo kuwa ni hujasoma, soma mpaka mwisho then ndo utoe critiques na sio kujiropokea bila kujua kilichoandikwa.
 
🚮🚮
 
View attachment 2596083View attachment 2596084View attachment 2596085View attachment 2596086View attachment 2596087View attachment 2596088View attachment 2596089View attachment 2596090
Kompyuta zilikuwepo miongo kadhaa nyuma kabla ya internet. Internet ndiyo kila kitu. '
Kwa hiyo hapa inaamanisha kuwa aliye-revolutionize matumizi ya teknoloji ni mmoja tu; Tim Berners Lee. Smartphones are just versions of computers; vitu ambavyo vimekuwepo hata kabla mimi na wewe hatujazaliwa

Mwaka 1992. Tim Berners Lee aligundua internet (www). Ethernet cables nazo pia ziliwahi kuwepo kabla ya internet na ndiyo maana watu walikuwa wana uwezo wa ku-share files
 
Umetaja watu halafu umewacha William Shockley, John Bardeen na water Brattain ambayo walibuni transistors.

Transistor ndio msingi WA computing devices zote tunazotumia sasa.

Halafu MTU Kama Robert Noyce inverttor WA integrated circuit kitu ambacho kimesaidia vifaa vya kompyuta kuwa ni vidogo mpaka vingine tunatembea navyo kama smartphone.

Hivyo vyote ulivyovitaja visingewezekana bila gunduzi ya transistor
Swali hapa ni je, kama internet isingekuwepo leo, vifaa hivi vingekuwa na msaada kwako kama ilivyo leo? Kumbuka kuwa mada inayoongelewa hapa ni kama iinternet isisngekuwepo.....
 
Ndiyo, kuanzia gari, ndege, meli, rada, satellite, missile, refrigerator, washing machines, oven, air conditioner, Mita za umeme, redio, TV, treni nk zote hizo zina IC ambazo msingi wake ni transistor.

Hata tafiti za ARPA(sasa ni darpa) za intaneti ziliwezekana sababu gunduzi mbalimbali za semiconductor. Halafu ni wapi kuwa inayozungumziwa hapa ni intaneti Tu maana kichwa cha mada kinazungumzia Teknolojia.
 
Back
Top Bottom