Jehovah Shamah
Member
- Aug 29, 2016
- 18
- 10
Umeumbwa kutimiza kusudi fulani la Mungu lakini hujawahi kulitimiza ndio maana una hasara. Hasara siyo kwenye biashara peke yake, kuna watu vichwa vyao vina hasara tangu wazaliwe, kichwa haijawahi kujiongeza kwasababu imepata hasara. Anaishi kwa hasara, nyumba yake ina hasara, mipango ina hasara, hasara kwenye masomo, hasara ya kupoteza marafiki kila siku, huna mpango kwasababu una hasara. Kumbuka usipopanga umeshapanga kushindwa. Umeshahama takribani kila nyumba unasema, wanakuroga, kila ukifanyacho hakifanikiwi! Hata ungepelekwa Ulaya hauwezi kufanikiwa. Hata ulale na Biblia kichwani au msahafu hauwezi kufanikiwa. Umesoma lakini bado una hasara. Hasara ukoo mzima, tatizo kama hilo wanalo wengine kwenye familia yenu.
TATIZO SIYO NCHI TATIZO NI MAWAZO NA KWA HAKIKA TATOZO SIYO MAWAZO TATIZO UMEACH KUSUDI AMBALO MUNGU ALIKUUMBA KWALO. HEBU KUMBUKA ULIPOTEZA WAPI MUELEKEO NA LINI KISHA URUDI.
TATIZO SIYO NCHI TATIZO NI MAWAZO NA KWA HAKIKA TATOZO SIYO MAWAZO TATIZO UMEACH KUSUDI AMBALO MUNGU ALIKUUMBA KWALO. HEBU KUMBUKA ULIPOTEZA WAPI MUELEKEO NA LINI KISHA URUDI.