Watu wengi huingia kwenye migomo mbalimbali kwa kukurupuka na matokeo yake ni kushindwa kufikia malengo yao.Watanzania wengi hasa walio kwenye ajira hutegemea mishahara na posho ambapo hawana hakiba ya kuendesha maisha yao hata kwa mwenzi mmoja.Hata huu mgomo wa walimu sidhani kama watafanikiwa kwa kiwango wanachotarajia kwani wengi hutegemea ajira tu na hawana namna ya kuenendesha maisha yao bila mshahara. Hii ndiyo maana ukifika tarehe za mwisho wa mwezi walimu hufurika kwenye mabenki ili kuchukua mishahara yao ili wasije wakaadhirika.Nashauri walimu pamoja na wafanyakazi wengine wajitahiti sana kuwa na vyanzo mbadala vya mapato ili wasitishwe na vitisho vya kuwafukuza kazi n.k. Ukiwa unategemea mshahara tu ni rahisi sana kutishwa na kama unategemea mshahara tu nashauri uwe mpole maana huna jeuri kwa mwajiri. walimu watakapofika kwenye mabenki na kukuta mishahara yao haijaingizwa nadhani kesho yake msimamo utalegea, ila wakijihadhari mapema na kuhakikisha wana vyanzo vya pesa vingine hilo halitakuwa tatizo.!!!
Ushauri wako una mawazo mgando, kwa sababu ya shida ndo uuze utu wako. Wewe na serikali kama mna ubia. Maana serikali inafanya hivyo kutulipa kidogo ili tushindwe kujitetea kwa vile hatuna chanzo kingine cha mapato.
Niwatie moyo walimu tusiogope vitisho. Na ielewke kuwa hakuna ukombozi bila maumivu. Leo Tanzania tuko huru baada ya baadhi ya watu kuweka uhai wao rehani. Tupambane si kwa ajili yetu bali hata kwa vizazi vijavyo.
Nimekumbuka wimbo wa Bahati Bukuku "Alipoianza safari------" Kabla ya mgomo wapo waliotutia moyo lakini wengine walitudhihaki eti hawawezi mara ooh hao ni vilaza, Leo tumeamua oh tulijua hawatafanikiwa----
Watanzania tuungeni mkono mgomo huu si muhimu kwa walimu tu bali kwa watu woote.
MAPAMBANO BADO YANAENDELEA ALUTA CONTINUA.
Huwezi kupigana vita wakati unanjaa pasipo na umoja pana unafiki "mtoto wa tajiri akionywa mtoto wa masikini tega sikio"Ushauri wako una mawazo mgando, kwa sababu ya shida ndo uuze utu wako. Wewe na serikali kama mna ubia. Maana serikali inafanya hivyo kutulipa kidogo ili tushindwe kujitetea kwa vile hatuna chanzo kingine cha mapato.Niwatie moyo walimu tusiogope vitisho. Na ielewke kuwa hakuna ukombozi bila maumivu. Leo Tanzania tuko huru baada ya baadhi ya watu kuweka uhai wao rehani. Tupambane si kwa ajili yetu bali hata kwa vizazi vijavyo.Nimekumbuka wimbo wa Bahati Bukuku "Alipoianza safari------" Kabla ya mgomo wapo waliotutia moyo lakini wengine walitudhihaki eti hawawezi mara ooh hao ni vilaza, Leo tumeamua oh tulijua hawatafanikiwa----Watanzania tuungeni mkono mgomo huu si muhimu kwa walimu tu bali kwa watu woote.MAPAMBANO BADO YANAENDELEA ALUTA CONTINUA.
Zingatieni haya jamaa kayaandika itafika mda hamjui hata pa kuelekea.