USIILIE KIAPO TABIA YAKO, NI HATARI SANA!!

USIILIE KIAPO TABIA YAKO, NI HATARI SANA!!

Tee Bag

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
7,220
Reaction score
5,627
USIILIE KIAPO TABIA YAKO, NI HATARI SANA!

KAMWE usithubutu kuapa kutofanya jambo fulani wakati ni tabia yako. Apa kwa kile ambacho unajua kimetokea tu, hivyo unaweza kujiapiza kutorudia na kweli hutarudia.

Ukiwa ni mwizi, kisha ikawa tabia yako, ukiapa kuwa hutarudia kuiba, ujue kifo chako kitatokana na wizi wako.

Kuna mwanajamii mmoja alikuwa jambazi. Baada ya matukio kadhaa alifungwa jela nchi jirani. Alipoachiwa na kurudi nchini alikula kiapo mbele ya wazee kwamba asingerudia tena ujambazi.

Wazee wakamwapisha kimila. Akachinjwa kondoo na kuambiwa airuke ile damu. Yule ndugu akaanza kuwa mtu wa dini. Hata hivyo, mwisho aliuawa kwa kuchomwa moto kwenye tukio la ujambazi.

Usiilie kiapo tabia yako. Sikuzani alijitambua tabia yake ni kutotulia na mwanaume mmoja. Alikuwa hivyo tangu kigori mpaka alipoolewa. Kwenye ndoa akawa anachepuka. Mume wake akamfumania. Sukazani akaomba msamaha, akala kiapo kutorudia. Aliapa kwa kushika kitabu kitakatifu. Baki ukijua, Sikuzani alifia chumbani kwa mchepuko.

Kaundime alikuwa hapendi watu. Alikuwa na roho mbaya na mchoyo kupita kiasi. Akina dada wa kazi walimkimbia kwa sababu alipenda kupiga ma'house girls. Alipata mimba. Kwa matatizo ya kiafya aliyokuwa nayo aliambiwa na daktari asifanye kazi ngumu.

Nyumbani kwao wakamnyima ndugu wa kukaa naye kwa sababu ya ukorofi wake. Hakuna aliyethubutu kumtafutia house girl, maana walimjua. Kaundime akaapa kwamba siku akipata house girl hatamnyanyasa wala kumpiga. Hivi sasa Kaundime yupo jela, kosa ni kumuua house girl wake kwa kumpiga na chupa ya soda kichwani.

Tumeusiwa kuwa kiapo si kitu cha kukiletea kimbelembele, na kama ni tabia yako basi ni haramu kuapa. Sempa alijipa hulka ya kutembea na wake za watu. Baada ya kubainika, akawa anasakwa na wanaume wenye pesa ambao walimtuhumu kutembea na wake zao.

Sempa akakimbilia kwa Pati kujificha. Pati akamwambia hawezi kumpa hifadhi maana anaweza hata kutembea na mkewe. Sempa akaapa mbele Pati kwamba hatarudia tena kutembea na mke wa mtu. Pati akamruhusu Sempa ajifiche kwake mpaka pale hali ingepoa. Niamini nikikwambia kuwa Pati alimfuma Sempa na mke wake.

Mwanaidi naye alizoea kubeba waume za watu. Akapata mchumba. Alimuuliza kama akimuoa angeacha kutembea na waume za watu. Mwanaidi aliapa. Leo mwaka wa tatu, sababu ya ndoa ya Mwanaidi kuvunjika ni kufumwa akiwa faragha na mume wa dada yake.

Tusipende kuapa. Tena, tusiziapie tabia zetu.

Ndimi Luqman MALOTO

FB_IMG_1531918603953.jpg
 
Ni kweli mfano mi hua najiapiza nikipiga punyeto leo au kesho basi siogi wiki ijayo.

Yanayonikuta daah kuna siku nitamkuta anaconda chumbani
 
~baki ukijua,Sikudhani Alifia chumbani kwa mchepuko

~Kaundime yupo jela,kosa ni kumuua house girl wake kwa kumpiga na chupa ya soda kichwani

~Niamini nikikwambia kuwa Pati alimfuma Sempa na mke wake

~Ndoa yao kuvunjika ni kufumwa akiwa faragha na mume wa dada yake
 
Kuvu ya kuapa wengi hawaijui kabisa, hivyo wana apa apa tu , wanachukulia kiapo chao kama kitu kisicho na maana, mwisho hufa au kupata mabalaa kibila hata kujua chanzo ni wao wenyewe
 
Kuna nguvu katika maneno, hata hivyo haturuhusiwi kuapa
 
Kila nkimaliza kupiga punyeto naapa kwa majuto kuwa sitoludia lakin amini siwez pata usingiz bila kuungurumisha Punyeto
Naichukia lakin ndo hivyo ACHA Ni Pambane Na Hali yangu
 
Kiapo kingine ni kutawala milele
 
Back
Top Bottom