Usihuzunike, haupo peke yako

Usihuzunike, haupo peke yako

Nima Imma

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2015
Posts
2,467
Reaction score
3,698
Hellow wapendwa ,
Poleni na majukumu

Leo nimejisikia tu vyema kuandika hili jambo mana huenda kuna anayelia lia huko akidhani yuko peke yake /dunia imemtenga

Jibu ni HAPANA , amka , hauko peke yako wewe dada mwenye miaka 33 ambaye hauna mtoto

Hauko peke yako ww uliyeambiwa hauna uwezo wa kuzaa tena ,achilia akili na maneno ya kuambiwa amini tu hakuna mwanamke Mgumba na utazaa
Hauko peke yako ww uliyekwenye ndoa yenye mitihani mingi isomalizika ,unaogopa kumove on ati utaonekanaje , Inuka hapo ulipo wengine pia tulishakimbia hivyo vifungo vyenye funguo ya kifo

Songa mbele
Hauko peke yako ww uliingia hasara kubwa na kuanguka kiuchumi wala usiogope kuanza kwenye chumba kimoja na kufanya biashara nyingine ndogo za kukuinua hapo ulipo amini nakwambia jipe muda na malengo utatoboa upya ,wanaokucheka hawatakusaidia hata buku la chai , hivyo hawakusaidii kitu kukamilisha ndoto yako
Hauko peke yako ww kaka ambaye umefukuzwa kazi na kukimbiwa na mpenzi wako , halikuwa fungu lako mshukuru Mungu anakupa aliye bora(vigezo vya traaaakko kubwa vinakuchelewesha)

Hauko peke yako ww mbunge uliyepatwa na aibu ya voice note! Watu wanamavideo na waliyakana live kwamba yameeditiwa
Hauko peke yako Zero Iq waz la biashara ya elfu 50 na watu wakakuona miyeyusho hata kitaani tunaonekana miyeyusho live ila ndo tunapambana tunatoboa

Hebu endeleeni na nyie kwenye comments
Huenda ukamfariji mmoja wapo

IRISE AND SHINE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ubaya hata ukiwa hauko peke yako ila matatizo bado ni yako na hayapo kwa kila mtu. Tujifariji tu
 
sawa lakini kujiona hilo ni la kwako mwenyewe litakuinua na kupigana zaidi ila ukiangalia wengine ili ujifariji. utakaa nalo muda mrefu
Kila mmoja na alivyo mm nilivyoona uwezekana wa kuzaa ni mdogo sana niliumia mnoo
Walonizunguka wote wanawatt hivyo nikaingia kwenye social media nikaunda na grup la wahanga tu ,aisee ni wengi sana na shuhuda zile nikajikuta napiga kifua na kusema yangu madogo na kuipokea hyo hali na sasa hivi hata unisimange na kunitukana nacheka tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe siko peke yangu ninayeuwaza mchepuko kwa utamu kila nikifuta number najikuta tena nimeusave[emoji23][emoji23][emoji23]

sent from toyota Allex
 
Kujifariji sawa, ila kama linatatulika ni Bora zaidi kutafuta ufumbuza kuliko kubaki nalo likikuumiza, na Kama halitatuliki kibinadamu basi ni Bora kuomba Mungu alishughulikie, hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu baba, hakuna, ila inategemea na Imani yako. Kamwe usikate tamaa, mwombe Mungu kwa Imani atafungua kizazi na utaitwa mama, shirikiana na waombaji watakaoweza kubeba mzigo/hitaji lako kwa Imani.
Kama una Imani nitafute nikusaidie 'kimaombi', na usije ukakariri kuwa umeshaombewa sana hapana, Ibrahimu na mkewe Sara waliomba kwa miaka 25 ndo Mungu akawajibu, na mifano mingine ipo mingi tu kwenye biblia na mengine halisi katika mazingira yanayotuzunguka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila mmoja na alivyo mm nilivyoona uwezekana wa kuzaa ni mdogo sana niliumia mnoo
Walonizunguka wote wanawatt hivyo nikaingia kwenye social media nikaunda na grup la wahanga tu ,aisee ni wengi sana na shuhuda zile nikajikuta napiga kifua na kusema yangu madogo na kuipokea hyo hali na sasa hivi hata unisimange na kunitukana nacheka tu

Sent using Jamii Forums mobile app

pole ndugu yangu ila usife moyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom