Za asubuhi wana MMU.
Jamani nilichokiona jana nimeshindwa kukiamini ila inabidi tu niamini.
Kuna rafiki yangu ana mpenzi wake kiukweli walipendana yaani hata mimi niliyapenda mapenzi yao hadi wakaanza kufanana, ila yule msichana amesoma hadi form 4 akapata zero na jamaa yeye aliishia la saba kwa hiyo maisha matamu hapo.
Shetani mbaya sana kutokana na uzuri wa msichana kuna babu mmoja ambaye ukweli pesa anazo akija ni full mashauzi kila siku gari mpya za hatari sana suti zisizogusika na mengineyo! kamposa msichana na hatimaye amemuoa.
Siku ya ndoa vijana wa karibu na rafiki yetu tulipata kazi ya kujitolea maana ilibidi tulipwe jamaa kataka kuanzisha bonge la vurugu harusini na alivyo kipande kumzuia shughuli pevu.
Ila hatimaye ndoa imefungwa mke kachukuliwa jamaa kabaki analia kama mtoto gheto.
Jamani pesa nimeivulia kofia.
likikukuta wewe unafanya nini maana jamaa anataka ushauri jinsi gan atamrudia mpenzi wake.
Nawasilisha