Usidharau biashara za kifamilia wakati zimekulea!

Curvyminx

Senior Member
Nov 29, 2016
179
221
Je? Uko kwenye kazi ambayo huipendi? Yaani upo upo tu unasubiri saa 11 jioni ifike usepe na tarehe 30 ulipwe? Je? Ni kitu gani kinakujia kichwani mwako mwanzo kabisa ukisikia makampuni haya....Nike, Volkswagen, Louis Vuitton, Samsung, Tata, Foxcon, Ford...au za nyumbani basi...Azam Bakhresa, Manji, Mo...?

Izo zote ni kampuni za kifamilia yaani family owned businesses. Nina uhakika ushavaa viatu vya Nike, ukanunua simu ya Samsung au Iphone, computer za Dell, HP au Apple, ukanywa whisky ya Hennessy, perfumes za mtoni- Christine Dior, Kenzo bila hata kujua anyway yote hayo ni kazi za branding, Azam, Mo, Manji products ndio usiseme wote tumekula hizi!

Inabidi tufikirie jinsi ya kuongeza thamani katika biashara za kifamilia. Kuna wengine wazazi wana tengeneza keki za kufa mtu na kupamba ukumbi matata, wengine wanafuga kuku wanakusomesha unaenda kutafuta kazi benki. Si vibaya ila izo biashara tatu tu nilizotaja unaweza kutengeza mshahara wa mwaka mzima huko benki ndani ya miezi. Think of innovation ya kuongeza kwenye hizi biashara lakini waTanzania wamekuwa wakidharau biashara za kifamilia kama hazina maana wakati zimekusomesha. Mwingine anakuuliza kwani hii biashara ya familia nayo kazi?

Ukweli ni kwamba opportunities Tanzania zipo nyingi ila swala la infrastructure ni issue ya siku ingine.

My 2 cents.
 
We jamaa una akili wewe... Mungu akutie nguvu mawazo haya uyaweke kwenye vitendo.
 
Mkuu umeongelea upande mmoja wa shilingi wazazi wengi wanavunja moyo sana watoto wao kwa maneno yao mfano biashara hii ni yangu na mke wangu tafuta yako au hizi ni Mali zangu tafuta yako. Mtoto ananza kujiona sio sehemu ya hizo mali kwa hiyo anajiweka mbali. Kitu kingine wazee wetu wengi sio wote hawambiliki ndugu yangu unaweza kwenda na wazo zuri lakini mtu anakuambia hayo ni mambo yenu vijana hata kwenye biashara mtu anataka kuleta uzazi kwenye kazi. Kwahiyo mtu anaona ni bora nikimbie mbali hayo makampuni uliyoyataja watoto wanaandaliwa mapema kabisa kuchukua nafasi kwenye kampuni, angalia wenzetu wahindi na warabu wanawaanda watoto wao kuona biashara za familia ni zao so mtoto anajua nikizingua hapa najihujumu mwenyewe. Kwa hiyo mtoa mada nafikiri umenielewa.
 
Wazo lako ni zuri mkuu ila kwa jamii zetu nyingi hususani za wazazi wa kitz wamekuwa na tabia mbovu, unakuta wazazi wana vimiradi vzr tu ww unavipigua mahesabu ukimaliza kusoma jinsi utakavyoviendeleza ili kukuza mtaji na kukuza biashara ila ukinaliza masomo tu utamsikia mzee nimekusomesha ili ukaajiriwe usinipe usumbufu tena.

Kwa hiyo wazazi wengi wa kiafrika wanawaandaa vijana wao kuajiriwa sio kujiajiri ama kusimamia miradi ya familia

Pia vijana wengi wa kiafrika wana tabia za kupenda sana vileo, sifa, starehe, ngono n.k hivyo huwakatisha wazazi tamaa na kuwafanya wasiaminike kukabidhiwa miradi ya familia
 
Wazee wengi hawatuamini Vijana kutokana na Mazingira yetu ya kujifunzia Kuwatia hofu
Lakini sisi vijana ndo injini ya mafanikio yao hao wazee wao bila sisi hawawezi sisi bila wao Vurugu
Nimeajiriwa na familia yangu Kuendesha duka lililokuwepo miaka 29 kabla sjazaliwa Na linasonga Front kwa kasi huku likiongeza ajira kwa watu wengine kadhaa.
Wazee wana mawazo mazuri lakini hawana uwezo wala nguvu ya kuitangaza na kuendana na mizunguko ya kibiashara sasa hapo ndipo vjana tunapposhika usukani na kuongoza mafanikio ya mawazo yao ya kukataa kuombwa hela kwa kuanzisha biashara kama hizi za familia.
Ni nzuri kweli zimetukuza tumekua kimawazo, kifedha, kiharakati na kibiashara
Kupitia biashara hizi hizi tumekuzwa kujitegemea na kujituma Kufikia mafanikio.

Tutafanya kila kitu kwa Ajili Yako.
Hatutafanya chochote katika Maisha yako

Ni wewe tunaekuamini sasa kutunza biashara hii kama tulivyowaamini waliokutangulia na wakafanikisha uwepo Wa biashara hii hadi sasa imefika wakati wako
Ni wewe sasa ndiye umeshika dhamana ya familia yetu Tumekuamini, Tunakuamini Kwa weledi ulokua nao UtatufikushA mahala Na sisi tujivunie Uwepo wako Katika familia hii. (Sauti ya Mjomba wangu Maganiko Kaguku)
Ikiniusia juu ya biashara hiyo.

Namshukuru mungu miaka kadhaa niliokuwepo nyumbani Nimefanya kitu.
Bado ipo Na itakuwepo mpaka Mwisho Wa Dunia.
 
Nimekupata vibaya mno! Siku hizi wazazi wanabadilika kidooogo. Ila ndio wapo wazazi wachoyo, hawaangalii mbali, anakwambia katafute zako kwahiyo biashara inakufa na yeye! Very very selfish alafu tunawaangalia wahindi tunawaita wezi na mengineo wakati wamejipanga from the beginning! Ni kweli wazazi wajifunze kuwaongeza watoto katika biashara ili waelewe pesa inatoka wapi na inatengenezwa vipi kwasababu hii ndio maana kuna biashara chache sasa hapa Tanzania utakazosikia zimedumu miaka 20,30 mtu anakufa na idea zake. Its sad. Kuna philosopher mmoja alisema, makaburini ndio sehemu tajiri kuliko kote, kwasababu, pale kuna watu wamezikwa na ideas/innovation za kila aina.
I guess, wazazi wa leo tuna majukumu extra, si tu kumvalisha, kumsomesha, kumlisha mtoto bali kumjenga kiakili and kumtayarisha kwa maisha ya baadae.
 
Wazo lako ni zuri mkuu ila kwa jamii zetu nyingi hususani za wazazi wa kitz wamekuwa na tabia mbovu, unakuta wazazi wana vimiradi vzr tu ww unavipigua mahesabu ukimaliza kusoma jinsi utakavyoviendeleza ili kukuza mtaji na kukuza biashara ila ukinaliza masomo tu utamsikia mzee nimekusomesha ili ukaajiriwe usinipe usumbufu tena.

Kwa hiyo wazazi wengi wa kiafrika wanawaandaa vijana wao kuajiriwa sio kujiajiri ama kusimamia miradi ya familia

Pia vijana wengi wa kiafrika wana tabia za kupenda sana vileo, sifa, starehe, ngono n.k hivyo huwakatisha wazazi tamaa na kuwafanya wasiaminike kukabidhiwa miradi ya familia

nimesikitika ghafla, kuna mzee mmoja alikuwa ana shule, akamuweka mwanae receptionist, kumbe wazazi wakilipa fees kwake mtoto hazifikishi, anakula. Ila cha kusikitisha, ni mzazi alisikika anasema "afadhali aibe mwanangu kuliko kuibiwa na mtu baki", dah, nilisikitika sana, huyu mtoto anavunja biashara na mzazi hajui amfanyaje mwanae. So, yes, wapo vijana wanaoaminika na wasio.
Na pia ukiwa unasimamia mradi/ biashara ya familia, lazima biashara ikulipe.
Yaani hapa lazima uwe mkali hakuna cha mtoto wala mzazi, whether umenilipia school fees or not, biashara lazima ikulipe mshahara. You have to be tough Mzee akuelewe nyumbani mtakuwa Baba na Mwanae, kazini ni kazi. Ila wazazi wengine...safari bado ni ndefu.
 
Wazee wengi hawatuamini Vijana kutokana na Mazingira yetu ya kujifunzia Kuwatia hofu
Lakini sisi vijana ndo injini ya mafanikio yao hao wazee wao bila sisi hawawezi sisi bila wao Vurugu
Nimeajiriwa na familia yangu Kuendesha duka lililokuwepo miaka 29 kabla sjazaliwa Na linasonga Front kwa kasi huku likiongeza ajira kwa watu wengine kadhaa.
Wazee wana mawazo mazuri lakini hawana uwezo wala nguvu ya kuitangaza na kuendana na mizunguko ya kibiashara sasa hapo ndipo vjana tunapposhika usukani na kuongoza mafanikio ya mawazo yao ya kukataa kuombwa hela kwa kuanzisha biashara kama hizi za familia.
Ni nzuri kweli zimetukuza tumekua kimawazo, kifedha, kiharakati na kibiashara
Kupitia biashara hizi hizi tumekuzwa kujitegemea na kujituma Kufikia mafanikio.

Tutafanya kila kitu kwa Ajili Yako.
Hatutafanya chochote katika Maisha yako

Ni wewe tunaekuamini sasa kutunza biashara hii kama tulivyowaamini waliokutangulia na wakafanikisha uwepo Wa biashara hii hadi sasa imefika wakati wako
Ni wewe sasa ndiye umeshika dhamana ya familia yetu Tumekuamini, Tunakuamini Kwa weledi ulokua nao UtatufikushA mahala Na sisi tujivunie Uwepo wako Katika familia hii. (Sauti ya Mjomba wangu Maganiko Kaguku)
Ikiniusia juu ya biashara hiyo.

Namshukuru mungu miaka kadhaa niliokuwepo nyumbani Nimefanya kitu.
Bado ipo Na itakuwepo mpaka Mwisho Wa Dunia.

All the best!
 
Yaani la muhimu nililoliona ni hiyo christan Dior perfume basi. Hizo zingine porojo tu, ukiwa zanzibar zinakuwa urojo.
 
Nyie hamjakutana na wazee ma bandidu nyie hasa hawa wazee wetu wa kichagga.

Mzee wa Kichagga atakusomesha mpaka Ulaya au States of America kama hela anayo ila biashara yake hugusi na ukiomba mtaji uanzishe yako hakupi hata Tsh 100. Wengi wao ni wakuda sana.

Usilolijua litakusumbua ndugu. Mi nakumbuka mtaji wa biashara yangu ya kwanza ni Bi. Mkubwa ndio alinipa + a bit of my savings...namuheshimu sana my Mom for that cz ilinifanya hata nikaheshimika. Mdingi baadae sana kuona noma ndio akaanza kunileta karibu. Hela unakuta anayo ila cent 5 ya kufungua biashara hakupi. Baas tu.
 
Unakumbuka mmiliki wa ilizokuwa hoteli za JB Belmont? Huo ni mfano tu.

Waafrika sisi, ukifa na business yako imekufa. Wazazi wanatuandaa tuwe waajiriwa hata kama wao wamejiajiri.
 
Back
Top Bottom