Usidanganyike: Hakuna malaika anayekuja kutoa roho yako, dead man knows nothing

The more you learn the more you know, the more you know the more you forget, the more you forget the less you Know,so why bother to learn?

Nimesoma maelezo yako kwa umakini sana tena ule wa hali ya juu.Kama ulivyosema"deadma tells no tale"Hakuna aliye na uhakika kuhusu kifo na kujuwa nini hatma ya maisha ya binadamu mara baada ya kufa.Hivyo zote hizi ni nadharia you ingawa tunaweza kujuwa nadharia ipi ina ukweli na ipi ni uongo kwa ku hoji.

Umemkosoa mwenzio kwa kuweka/kutoa mafundisho ya uongo kuhusu kifo lakini na wewe umepita mulemule alikopita yeye kwa kusema uongo.

Hakuna,narudia Hakuna maisha baada ya kufa/kufariki.Ukifa umekufa Kama vile ambavyo kiumbe wengine wanavyokufa(wanyama&wadudu).
Ili tujuwe kuwa Hakuna maisha baada ya kufa lazima tunaangalie japo kwa uchache maisha/uhai umejengwa na Nini?

The reality we experience(uhai) is created by our consciousness and life and without those two elements(consciousness and life) it's just not there.
Sasa kwa maana hiyo hapo juu ni kuwa uhai umejengwa Katika Maeneo mawili makubwa ambayo ni ufahamu na maisha(mazingira).
Huu ufahamu umejengwa na ubongo.

Kiumbe kinapo kufa means na ubongo umeshindwa kufanya kazi hivyo hupoteza fahamu hivyo hawezi kuishi tena baada ya tukio Hilo.Maybe tu assume kuwa baada ya kuoza mwili, anaweza kupata mwili mwingine tena wenye ubongo mwingine tena....ha hahaaaa haha hapa napo kutazua maswali mengi bila majibu.

Hakuna maisha baada ya kifo.Ukifa ndo mwisho wako yaani kama ambavyo haukuwa kuishi sehemu yoyote kabla ya kuzaliwa ndo hivyo ukifa,you become a non existence.

The greatest enemy of the knowledge is not ignorance but the illusion of the knowledge.By Stephanie Hawking.

Nawaacha na swali: Does soul exist
Nakubaliana na wwe kabisa.... 100%.
 
As neuroscientis unaweza kuongeza nyama mkuu maana kifo kinaanzia huko kwenye nyuroni
Da vinci ntakuja kuelezea jinsi cerebral cortex inavyokua active 2 mpk 20 seconds after cardiac arrest... Na vitu vingine vingi maana a brain still functions kwa sekunde chache hata baada ya moyo wa mtu kusimama... Mkuu ntakuja aisee

This time i promise... Mambo yamenikaba sana hafu mkuu wengine tupo humu ku entertain bhana mambo ya shule tunayaacha huko huko

Ntakuja usiwaze
 
...................Ingependeza angekuja marehemu mmoja akatuthibitishia ulichoandika hapa otherwise utakuwa umeunga unga maneno tu,inashangaza sana kiumbe usiyeijua hata dakika yako moja mbele ni nini kitakutokea kisha uje kuzungumzia habari za kifo humu.
Mambo mengine aliyoandika Denvers Sir-Mimi,yako proved by the Bible,kwa hiyo yana ukweli kiasi fulani.
 
View attachment 1238409
Kuna jamaa huku kwa Zitto kabwe kwake kafunga vipaza sauti hua anaweka mawaidha na dua
kiislamu, ni jambo jema sana hili. Ila sasa katika mawaidha aliyoyaweka jana usiku saa 4 kaweka
mawaidha yanayohusu Kifo, kwakweli yale mawaidha yalinikosesha amani ya moyo maana
yalikua yanaogofya na kutisha hasa....Yalikua yanahusu Jinsi malaika wa mauti anavyokuja
kuchomoa roho. Nilikua interested zaidi hiyo sehemu ambapo Malaika anakuja kuchomoa roho,
na ndio kilichofanya niandike mada hii jinsi mimi navyo elewa dhana ya Kifo, sijui wengine
mnaielewa vipi..Mimi navyoelewa wakati wa kufa hakuna malaika Azrael wala kiumbe yoyote
yule anayekuja kutoa roho ya mtu...Lengo la mada hii sio kukashfu dini wala imani za watu, bali kuelimishana na kuelekezana bila kashfa.

Dhana ya Kifo.
Kwanza kabisa viumbe vyote vimeumbwa katika mifumo miwili ambayo ni Mortals na
Immortals.
Mortals ni viumbe vyote ambavyo vinaweza kufa mfano binaadamu,
wanyama,mimea nk...Immortals ni viumbe wote ambao wanaweza kudumu maisha yote kama
haitatokea wakauwa Wanaojulikana zaidi ni jelly Fishes na baadhi ya bacteria...Futurist na
wanafalsafa mbalimbali wanasema kwamba binaadamu wa karne hii ya 21 baada ya miongo
kadhaa anaweza kufanikisha kuwa katika mfumo wa Immortal kutokana na maendeleo
makubwa ya teknolojia na hasa kwenye madawa na matibabu..pia Extending of life span will be
possble
mpaka kufika miaka 170. usibishe SOMA.

Kifo: Kwa upande wangu naweza fafanua kifo ni kitendo cha Roho kuuacha mwili huu wa nyama
na kwenda Dimmension nyingine na mwili kubaki duniani,mwili utabaki duniani ili kukamilisha
circle ya kwa kuoza na kuruhusu viumbe wengine kutokea...Mtu anapokufa anaanza kufa kiungo
kimoja kimoja mwisho kabisa ubongo ndio unamalizika, kinachotoka katika mwili wa binaadamu
ni roho (Soul). Kwenye computer kuna chip inaitwa BIOS Chip hii kazi yake ni kubeba taarifa zote
za kompyuta husika..Hivyo Roho ni kama Bios Chip, Roho ndio inabeba taarifa zoote
zinazokuhusu wewe ikitoka inaondoka nazo, mwili unabaki unaharibika. Ndio maana Vitabu vya dini vinasema Mungu anahukumu Roho sio mwili,kwakua mwili unakua hauna kazi tena.

Hakuna kiumbe yoyote anayekuja kukutoa roho sijui anakuja kuivuta kuanzia kwenye kidole cha Mguu HAKUNA. Maisha ya binaadamu ni kama jenereta lililowekewa mafuta, mafuta hayo yatafika muda fulani yaishe yakiisha tu basi Jenereta litazima. Tuchukulie Mwili ni Jenereta,
Mafuta ni Muda (Time), Sasa iko hivi kinachofanya mwili ufe ni muda! Though time seem to be
Illusion but it is Virtual Real.Muda ndio unafanya kiumbe fulani afe, Ndio maana Wanasayansi
wanafanya kila njia kufanikisha kwenda kinyume na muda kwa kutumia Time Travelling (Ref:
Time travel,itakua suruhisho la kifo). Duniani tumewekewa muda ili tuweze kufanya shughuli
zetu za kila siku kwa kuufuata, Pia mwili wa binaadamu umewekewa Muda fulani ukifika tu basi
roho yako haina budi kuuacha mwili, sasa hapo haijalishi Roho yako itauacha mwili kwa kutumia
njia ipi. Ndio maana wanasayansi wanaona wakifanikisha kutengeneza Time travelling Machine
watakua wanaweza ku-loop from one point to another point with a different Time.

Sasa iko hivi baada ya process ya mtu kufa ikimalizika Roho inakua enda kwenye eneo
linalofahmika kama After death au Eternal Realm,Roho ikiwa eneo hilo inakua kwenye mfumo
wa Spirituality. Kwenye eneo hilo Time is Timeless, Roho ikiwa hapo haiwezi kufa tena,roho
haiwezi kuzeeka wala kukua maana Hakuna Muda. muda upo kwa binaadamu tu...Ndio maana
mtu akifufuka leo hii atajua kua alikua tu kalala muda mfupi uliopita. Usidangnyike eti kuna
malaika hua anakuja kaburini anaanza kukufanyia mahojiano na kukupa mateso.Hakuna kitu
kama hiko Deadman knows nothing, Deadman tells no Tale.

Malaika ni Roho, kapewa uwezo wakubadilika kwa kuvaa umbo lolote lile analotaka kutokana
na majukumu husika aliyopewa, anaweza kubadirika mwanamke au mwanaume au kiumbe
yoyote. Yesu ni Roho, alipokuja duniani alivaa umbo la kiume, Ukifa roho yako inakua kwenye
mfumo wa Immortal, ndio hapo sasa roho yako ikiwa convicted to hell or Heaven itaishi
Daim
a..maana Huko muda hau-exist.

Maoni yangu.
Dunia imebadiriki,vizazi vimebadirika..inawezekana kipindi hiki vizazi vya Millenial generation (watu waliozaliwa kuanzia 1982 mpaka 2004 na Generatiion Z (watu waliozaliwa kuanzia 2005 mpaka leo hii) inawezekana ndio vizazi vilivyo elimika na kustaarabika zaidi kuwahi kutokea hapa duniani kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia pamoja na mabdiriko ya kimazingira...Hivyo Peoples are not fools anymore, Viongozi wa imani za kidini inabidi wabadili
approach wanazotumia katika kuwarudisha watu kundini. Tusiwatishie watu kwa mambo ya kufikirika kama hayo ya Malaika kuja kukuvuta roho wakati hata huyo anayekuhadithia hajawahi
kupata hata Near Death Experience kiufupi hata yeye kahadithiwa na mtu aliyehadithiwa.

Hizi dini kubwa mbili duniani ndio zinaongoza kua na wafuasi mambumbumbu ndio maana hata ugomvi wa sisi kwa sisi hauishi.ELIMU ELIMU ELIMU. Ukingalia kwa makini unaweza ona Zile imani tunazoziona hazina maana kama Budhism,Taoism,Atheism,Induism nk wao wanaongoza
kwa kua watu wapole na wanahekima sana wajua kwa nini? Kwao hawana mipaka kwenye elimu, kichwa kitupu ni sawa na debe tupu..kichwa kilichojaa vitabu ni sawa na debe lenye maji
ndani. unaweza pima yupi mpiga kelele.

Kwa wenzetu hasa mabudha wao husoma kila kitu,falsafa, fizikia,Spiritaul
enlightment,astronomy, biolojia nk nk ndio maana ukimkuta budhist mahali hua wako very
smart upstairs, au Monk wa Shaolin wako very smart mno maana wao hadi Martial arts
hujifunza na wanaijua vizuri mno...Wachawi nao wanajua mengi mno maana wanasoma vitu ambavyo viko beyond the limit (uchawi ni sayansi isio songa mbele, conservative) sie
tunajisome vitu kufuata mtaala .

Huku kwetu kwa Dini ya waroma Huku tunatembea na Psychology,Philosphy na Theology..Angalau huku mambo sio mabaya maana hvyo vitu vitatu vinawasaidia kuwaunganisha watu kwa kutumia akili zaidi..ila kwa dini kutoka kwa warabu kidogo huko hali ni
mbaya hasa kwa wafuasi wa bara la afrika, wao elimu ahera tu! elimu dunia kwao haramu
angalau sasa hivi wanabadirika ndio maana wakiambiwa kuna jamaa hua anakuja kubeba roho
na vitisho vingine vingii wao huamini. Jamni tuwekeze kwenye elimu.

Learn, Learning never exhaust the Mind,and knowledge will keep you Free and Peace
-Vers
Kuna ukweli kiasi fulani kwenye bandiko lako mkuu,so it is helpful as a source of knowledge in some aspects.Hata hivyo yapo maeneo ambayo huko sahihi.Kwa mfano umesema vizazi vya miaka ya hivi karibuni vimestaarabika zaidi kuliko vizazi vya zamani.Sio sahihi.To me vizazi vya zamani vilikuwa vimestaarabika zaidi kuliko vya sasa. Mkuu sio siri,watoto wa leo hawana adabu,si kwa wazazi tu,bali hata kwa watu wengine wakubwa. It is simply a rotten generation.Halafu what you call development
is actually an illusion disguised as development.The whole thing is designed by the Devil to cheat,so that people do not realize the danger facing them.

Mkuu maendeleo sio vitu,maendeleo ya kweli ni lazima yalete upatikanaji wa chakula kingi na bora sio GMOs etc kwa mfano;maji safi,salama na mengi,maji ya leo yamejaa sumu;nguo bora sio za plastic,tena with chemicals;hewa safi sio iliyokuwa polluted kama tuliyo nayo leo;afya bora kwa watu,sio health system ya medication ambazo ni sumu tupu;amani;hope;mazingira yasiyo na hofu au woga nk.nk.Tuonayo sasa ni kinyume kabisa na hayo,kwa hiyo ni under development,sio development.

Sikubaliani na wewe pia kwamba life can be extended to beyond 120 years by the so called scientists,because that is the limit set by God himself as stipulated in the Bible.Mungu aliamua kupunguza maisha ya mwanadamu kwa kuwa ameshindwa kuishi sawa sawa na jinsi Mungu alivyokusudia.Kwa maana nyingine ni kwamba mwanadamu amemtenda Mungu dhambi.Nuhu aliishi miaka 960,but that will never be repeated.Sasa ukiishi sana sana mostly ni 70 years,80 ni bonus!Ni kweli the so called scientists are trying to extend life,but they will never suceed.Gods decision is final.

Hizo ni sehemu chache tu ambazo nimeona bandiko lako lina shida,there could be more,sija concentrate sana kulisoma.Mungu akubariki.
 
Wewe unajifanya una science halafu umepotoka.
Kama mwanasayansi nikuulize, JE ROHO IPO?
Does the SOUL EXIST?

Kama unaamini kuna roho, hayo mafundisho mengine yote nayo ni imani vile vile. So calm down.

Mbona we unaamini Malaika ni roho na wanaweza kujigeuza umbo lao. Kisha unaamini Yesu ni roho alikuja kwa umbo la binaadam. Logic ndogo tu, if A =B, and C=B then A= C. Kwa hiyo Yesu naye ni Malaika. (Soma vizuri maelezo yako). Kwa sababu hii, Yesu si Mungu ni malaika. Does it make sense?

We unaamini Mungu ana utatu. Kwa Muislam haiingii akilini. Pia Atheist anakuona juha vile vile.

So kila kitu ni imani. Waachie wenye imani yao.
 
Hivi vitisho ndiyo vilinifanya nihamehame dini kutafuta penye afadhali,kumbe kule nilikoingia ndiyo kunatisha zaidi

Siku ya kwanza tu swala ya asubuhi muadhini anaita watu wakaswali alisema
"Kitanda chako ndiyo jeneza lako,nikavuta shuka mpaka kichwani,jamaa akaendelea na hilo shuka ulilojifunika ndiyo sanda yako,waislam amkeni

Dah sikulala tena ile siku,nakumbuka asubuhi ndiyo nikapata akili ya kujua michezo yao baada ya kuanza kuhoji na.kusoma

Angalau sasa nimekata minyororo ya dini niko huru sana na amani.
 
Wewe unajifanya una science halafu umepotoka.
Kama mwanasayansi nikuulize, JE ROHO IPO?
Does the SOUL EXIST?

Kama unaamini kuna roho, hayo mafundisho mengine yote nayo ni imani vile vile. So calm down.

Mbona we unaamini Malaika ni roho na wanaweza kujigeuza umbo lao. Kisha unaamini Yesu ni roho alikuja kwa umbo la binaadam. Logic ndogo tu, if A =B, and C=B then A= C. Kwa hiyo Yesu naye ni Malaika. (Soma vizuri maelezo yako). Kwa sababu hii, Yesu si Mungu ni malaika. Does it make sense?

We unaamini Mungu ana utatu. Kwa Muislam haiingii akilini. Pia Atheist anakuona juha vile vile.

So kila kitu ni imani. Waachie wenye imani yao.
Mimi hakuna sehemu nimeponda imani ya mtu ila nimeponda uzushi na vitisho tunavyopewa baada ya mtu kufa..
 
Kuna ukweli kiasi fulani kwenye bandiko lako mkuu,so it is helpful as a source of knowledge in some respects.Hata hivyo yapo maeneo ambayo huko sahihi.Kwa mfano umesema vizazi vya miaka ya hivi karibuni vimestaarabika zaidi kuliko vizazi vya zamani.Sio sahihi.To me vizazi vya zamani vilikuwa in a much better situation kuliko vizazi vya leo. What you call development is actually an illusion disguised as development.This is designed by the Devil to cheat,so that people do not realize the danger facing them.

Maendeleo sio vitu,maendeleo ya kweli ni lazima yalete upatikanaji wa chakula kingi na bora sio GMOs etc.;maji safi na mengi;nguo bora sio za plastic;hewa safi sio iliyojaa sumu;afya bora kwa watu;amani;hope;mazingira yasiyo na hofu au woga nk.nk.Tuonayo sasa ni kinyume kabisa na hayo,kwa hiyo ni under development,sio development.

Sikubaliani na wewe pia kwamba life can be extended to beyond 120 years by the so called scientists,because that is the limit set by God himself as stipulated in the Bible.Mungu aliamua kupunguza maisha ya mwanadamu kwa kuwa ameshindwa kuishi sawa sawa na jinsi Mungu alivyokusudia.Kwa maana nyingine ni kwamba mwanadamu amemtenda Mungu dhambi.Nuhu aliishi kwa miaka 960,but that will never be repeated.Ni kweli the so called scientists are trying to extend life,but they will never suceed.Gods decision is final.

Hizo ni sehemu chache tu ambazo nimeona bandiko lako lina shida,there could be more,sija concentrate sana kulisoma.Mungu akubariki.
Ahsante sana mkuu.
Ila mkuu sio kwamba wataongeza miaka kwa njia hiyo hapana bali watatengeneza dunia ambayo itakua rafiki kimazingira ili mtu aweze kuishi miaka mingi pia unoreshaji mkubwa wa dawa na matibabu.
...
Vizazi vya leo nasema viko civilized zaidi kuliko vingine kutokana na jinsi dunia ilivyopiga hatua kubwa kwenye Teknolojia na Uboreshaji wa maisha..Hivyo basi upatikanaji wa taarifa na elimu sio kama zamani. Wengi wameelimika ndio maana ukiwaambia eti kuna kupigwa marungu kaburini watakuona juha
 
Pia the out of body experience (The OBE illusio) n is one of these sensory deceptions, and arises in the brain’s temporoparietal region

Nkipata muda nitakuja mkuu
Tunasubiri mno mkuu uweze kutuelimisha..
 
Da vinci ntakuja kuelezea jinsi cerebral cortex inavyokua active 2 mpk 20 seconds after cardiac arrest... Na vitu vingine vingi maana a brain still functions kwa sekunde chache hata baada ya moyo wa mtu kusimama... Mkuu ntakuja aisee

This time i promise... Mambo yamenikaba sana hafu mkuu wengine tupo humu ku entertain bhana mambo ya shule tunayaacha huko huko

Ntakuja usiwaze
Entertain while educating..hvyo ndio inapswa..
Nafahamu moyo ndio hufa kwanza afu ubongo unakua unabaki unafanya kazi chache kwa muda then nao unastop..Ndio maana kuna muda mtu anaweza piga chafya.
Nasubiria utuletee nondo zako mkuu..
 
1 - "Lengo la mada hii sio kukashfu dini wala imani za watu, bali kuelimishana na kuelekezana bila kashfa."
2 - ".ila kwa dini kutoka kwa warabu kidogo huko hali ni
mbaya hasa kwa wafuasi wa bara la afrika, wao elimu ahera tu! elimu dunia kwao haramu
angalau sasa hivi wanabadirika ndio maana wakiambiwa kuna jamaa hua anakuja kubeba roho
na vitisho vingine vingii wao huamini."

Ndugu unakwama wapi na unaonekana mtu mwenye ELIMU ila unajikanyaga tu, au nieleweshe maana ya kukashfu, halafu imani ya mwingine sidhani kama inapunguza kipato chako, elimu yako bado inakuzidi
Sina shida na imani za watu ndio maana hakuna sehemu nimesema wanaabudu isivyotakiwa..ila kwenye swala la kutisha watu hapo kidogo sikubaliani nao..mimi kama binaadamu nayejitambua
 
The more you learn the more you know, the more you know the more you forget, the more you forget the less you Know,so why bother to learn?

Nimesoma maelezo yako kwa umakini sana tena ule wa hali ya juu.Kama ulivyosema"deadma tells no tale"Hakuna aliye na uhakika kuhusu kifo na kujuwa nini hatma ya maisha ya binadamu mara baada ya kufa.Hivyo zote hizi ni nadharia you ingawa tunaweza kujuwa nadharia ipi ina ukweli na ipi ni uongo kwa ku hoji.

Umemkosoa mwenzio kwa kuweka/kutoa mafundisho ya uongo kuhusu kifo lakini na wewe umepita mulemule alikopita yeye kwa kusema uongo.

Hakuna,narudia Hakuna maisha baada ya kufa/kufariki.Ukifa umekufa Kama vile ambavyo kiumbe wengine wanavyokufa(wanyama&wadudu).
Ili tujuwe kuwa Hakuna maisha baada ya kufa lazima tunaangalie japo kwa uchache maisha/uhai umejengwa na Nini?

The reality we experience(uhai) is created by our consciousness and life and without those two elements(consciousness and life) it's just not there.
Sasa kwa maana hiyo hapo juu ni kuwa uhai umejengwa Katika Maeneo mawili makubwa ambayo ni ufahamu na maisha(mazingira).
Huu ufahamu umejengwa na ubongo.

Kiumbe kinapo kufa means na ubongo umeshindwa kufanya kazi hivyo hupoteza fahamu hivyo hawezi kuishi tena baada ya tukio Hilo.Maybe tu assume kuwa baada ya kuoza mwili, anaweza kupata mwili mwingine tena wenye ubongo mwingine tena....ha hahaaaa haha hapa napo kutazua maswali mengi bila majibu.

Hakuna maisha baada ya kifo.Ukifa ndo mwisho wako yaani kama ambavyo haukuwa kuishi sehemu yoyote kabla ya kuzaliwa ndo hivyo ukifa,you become a non existence.

The greatest enemy of the knowledge is not ignorance but the illusion of the knowledge.By Stephanie Hawking.

Nawaacha na swali: Does soul exist
Yes soul it does..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom