Usichopenda kutendewa, usimtendee mwenzako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usichopenda kutendewa, usimtendee mwenzako

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mkwaruzo, Feb 28, 2011.

 1. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #1
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tumetoka mbali jamani. Japokua nchi yetu haina maendeleo yakuridhisha (ni moja kati ya nchi masikini) bali yapo mambo mengi ya kujisifia na kujivunia kuanzia mtu mmoja mmoja hadi kufikia taifa zima. Ninachotaka kukiongelea ni mfumo mzima wa utumiaji wa simu na
  ofa zinazopatikana kupitia maongezi (kupiga simu) na utumaji wa ujumbe mfupi wa maandishi ( short message service). Lakini kwanza acha niwakumbushe kuhusu kipindi cha nyuma kidogo wakati
  mtandao unaotumika ulikuwa ni mmoja tu (TTCL) na ikiwa wenye simu walikuwa ni wachache, nao katika kipindi hicho waliweza kuhesabika kama walivyokuwa wanahisabika wenye luninga (Television). Mawasiliano kwa wakati huo hayakuwa ya urahisi sana lakini yaliridhisha kiutumiaje kwa kiasi kikubwa. Kwani utumiaji wa simu kwa wakati huo ulitawaliwa na ustaarabu wa aina ya pekee. Mfano, kwa mtu aliyekuwepo
  ng'ambo (nje ya nchi) na akataka aongee na ndugu, jamaa au rafiki yake aliyekuwepo nchini ilimbidi apige simu siku ya/za kabla ili
  atowe taarifa ya muda na siku aliyokusudia kuongea nae huyo amtakae (mpigiwaji). Na katika kipindi hicho ilikuwa hakuna kutuma message.

  Mambo yalianza kubadilika baada ya kuingia simu za mkononi. Mwanzo aliyekuwa na simu hizo za mkononi (mobile phone) alionekana kuwa ni mtu mmoja kati ya watu wenye hadhi au kipato kizuri. Haikuishia hapo, mabadiliko yaliendelea kwa kadri siku zilivyozidi kusonga hadi kufikia leo hata watoto wadogo wanamiliki/
  wanamilikishwa simu.

  Kasheshe likaanzia
  hapo kwani sasa imekuwa tabu/kero kwa baadhi ya watu kumiliki simu. Au ndiyo limbukeni akipata.............? Imenibidi nitumie neno limbukeni kwasababu mtu ambaye ni mstaarabu hawezi kutumia simu ovyo ovyo.
  Unakuta mtu anakupigia simu usiku wa manane, ukimuuliza cha mno nini, eti anakusalimia.
  Kweli ndiyo ofa, basi ndiyo kufikia kukosa muda muafaka wa kumpigia mtu kwa kumsalimia au kwa shida zake ndogo ndogo? Huu ni ujinga.

  Basi huyo ana afadhali....
  kwani kuna huyu anaebip kwa private namba. Na wala siyo
  kusema atakubip mara moja kisha yakaisha. Sasa iweje au kujua namba ya mtu ndiyo imekuwa tatizo?

  Kana kwamba
  haitoshi, kuna na huyu anaekung'ang'aniza umpigie kutokana na staili yake anayokubip. Utaona anakubip zaidi ya mara 20. Ukiwahi kupokea, yeye kakata. Hata ukiamua kumpigia, unakuta namba yake ipo bize kwa kukupigia wewe. Sasa huyu anaeamua kufanya hivi, kama yeye kashindwa kukupigia, anaijua hali yako ikoje hata aamue kukufanyia hivyo? Sijuwi ni lini tutabadilika na kuacha upuuzi kama huu?

  Pia inanisikitisha kuwaona hawa dada zetu wanaoingizwa tabuni baada ya kuchukuliwa namba zao za simu na kuingizwa kwenye mtandao au katika magazeti eti wanatafuta wachumba. Wewe unaeamua kumfanyia mwenzako hivi, sijuwi unafaidika kitu gani? Jamani hebu tujistahi nasi tustahiwe, tusikuwe miguu na vimo akili zikabaki za kitoto.

  Afadhali ya wote hao, hawa naweza kuwapa namba 1 kwa
  kituko chao. Huamua kutembea na ma-hand bag makubwa ili kubebea simu za ndani ambazo ni wireless kusudi apate kudanganya anapopigiwa. Utasikia "ndiyo nimeamka sasa hivi na nilikuwa naelekea bafuni kukoga". Kumbe yupo mtaa wa saba kufuata umbea/mabwana. Hivi niulize, hawa
  huwa hawajuwi kuwa za mwizi arobaini? Ninachotaka
  kuwakumbusha ni kwamba siku ya ukweli kudhihirika, uongo hujitenga. Napenda
  nikuambie wewe msomaji wa thread hii kuwa, siku utakayopata nafasi ya kueleza hisia zako juu ya kitu chochote kile, hakikisha unaitumia vizuri nafasi hiyo. Nami kwa kutumia
  nafasi hii sitopenda kuwasahau hawa wenye tabia ya kuchukua simu za watu na kusoma message au kuingia
  katika gallary kuangalia vilivyomo au hata kujitumia katika simu zao, na wabaya zaidi ni hawa wanaozifanya simu za wenzao kuwa ndiyo kitega uchumi cha wao kupata muda
  wa maongezi (credit) kwa kujirushushiya pesa bila ya ridhaa ya mwenye simu. Jamani hii ni haki?

  Huyu mwengine kwa kutojua umuhimu uliyotimia wa kuwa
  na simu, huwa hazipi
  umuhimu simu anazopigiwa sawa na zile anazopiga yeye eti kwasababu namba iliyompigia (iliyotumika) ni ngeni kwake bila ya kujali huyo mtu anaweza kuwa ni mtu wa karibu kwake au kuna umuhimu fulani kiupande wake kwa kupokea simu hiyo.

  Na si jambo la kushangaza kusikia mtu kanuniwa eti kwasababu ya kutaka amfahamu mtu wa upande wa pili (aliyepiga simu). Kwa ufinyu wa mawazo, huyo aliyepiga simu baada ya kuulizwa 'wewe ni nani', huchukia na kujiona hajapewa umuhimu hadi kufikia namba yake kufutwa katika simu ya yule aliyempigia bila ya kuangalia kuwa simu ni kifaa kinachoweza kuletahitilafu aidha ikawa kioo (screen) hakiwezi kuonyesha maandishi yoyote yale au laini ya simu ilipotea na ikabidi kuchongesha laini nyengine yenye namba sawa na ile iliyopotea (swaping). Binafsi naweza kumpigia simu mtu anayenijuwa kwa namba yoyote ile na akanitambuwa bila ya kuniuliza kuwa mimi ni nani. Ila mimi siyo rahisi kwangu kuweza kutambua sauti za waliowengi hadi inanibidi nimuulize mtu aliyenipigia simu kuhakikisha kama ndiye yeye au laa japokuwa katumia namba yake ya kawaida. Na watu kama mimi wapo wengi tu.

  Mwisho ni kwa hayu anaeweka picha za ngono/uchi (pornograph) katika simu yake wakati anajuwa kuwa hawezkumnyima mtu simu hiyo. Cha kusikitisha zaidi unakuta mtu huyo anakuwa msambazaji mzuri wa picha hizo, kama vile kaajiriwa.

  Wengine wanadiriki kuplay (picha hizo za ngono) katika kundi la watu na kuwasikilizisha sauti za miguno ya kimapenzi hata wale wasiyotaka. Tunaelekea wapi jamani? Au huu ndiyo
  ustaarabu wa utandawazi? Kama ni dada/kaka yako aliyepigwa picha akiwa uchi, ungediriki kuisambaza/kumrushia mtu?

  Kweli teknolojia imekuja wakati tukiwa bado hatujajipanga na ndiyo maana tunaitumia vibaya zaidi kuliko inavyotakiwa. Wala siyo kama nimekusudia kuwafundisha jinsi ya kutumia simu, la hasha.
  Nilichokusudia mimi ni kuvitaja vile vinavyoweza kukukera ima wewe au kumkera mwenzako pindi anapofanyiwa. Sidhanikama kuna shule maalum inayofundisha watu ustaarabu bali ni sisi wenyewe kukumbushana kwa mule tunamofanya mambo kinyume na (maadili) inavyotakiwa. Basi ni wajibu wetu kubadilika.
   
 2. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  anayenikera zaidi ni yule anayebip kwa praiveti namba
   
 3. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Anayetusikiliza sauti za miguno ya mapenzi ndiye anayenikera zaidi. Kwanini asitumie headphone kama kukaa sehemu ya peke hawezi. Basi usiombe akawa na simu ya mchina, kama upo pembeni na mtu unayemheshimu, bora usepe
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Feb 28, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kaaaazi kweli kweli!!
   
 5. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Too long. Next time you should summarize.
   
 6. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #6
  Feb 28, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hilo hata mimi nimeliona, imebidi niende break nitarudi kuendelea kusoma!!!:A S 13:
   
 7. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #7
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hata mm nimeliona hilo but ndo nilikuwa nimeshaitayarisha. Kwa kuwapunguzia usumbufu, nimejitahidi kuweka paragraph ila baada ya kuipost, sijuwi hata wapi zilipopotelea. Hili nalo ni tatizo, kama vipi liwasilishwe kunako husika.
   
 8. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #8
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Fupisha kidogo bana nimeshindwa kumalizia kusoma
   
 9. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #9
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  usijali dr
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Posts ndefu kwenye jukwaa la MMU Zinanichosha.
   
 11. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #11
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi hata sijaisoma hiyo thread....maana duh...wengi concentration span yetu ndogo kweli kweli.

  ila kwenye hicho kichwa cha habari mi sijakubaliana nacho. Sio kila KITU ambacho we hupendi kufanyiwa basi na wengine hawapendi.....mi nafahamu vitu vingi sana ambavyo wasichana wanapenda kufanyiwa na kitu hicho hicho ukimfanyia mwanaume inakuwa ugomvi.
   
 12. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #12
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kumbe na wewe umeona huku hatutaki hadithi ndefu bana straight forward mchezo unakwisha.

  Mie sijamaliza kusoma kabisa
   
 13. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kama umeona ni kuwa nimejiunga juzi tu ktk jf. Hivyo makosa madogo madogo kama haya ndiyo yanayotoa nafasi kwenu nyinyi ya kunipa muongozo wa kile kinachotakiwa hapa. Kwaiyo hali hii haitojitokeza tena kupitia mm. Then nimeona kuwa lengo halifikiwa coz badala ya kucomment kwa hata hicho kidogo mlichnkisoma, mnacomment zaidi ktk ukubwa wa thread.
   
 14. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Usijali utazoea tu.
   
 15. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hata kama hujaisoma, nakushkuru kwa kunielewesha juu ya kosa lililopo ktk tittle. Ni kweli kuwa kuna kitu unaweza kuwa huchukizwi nacho kikitendwa juu yako ila mwenzako anachukizwa nacho. Thnks alot
   
 16. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna point nitaibold na kuchangia kesho mob haina option nyingi
   
 17. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Uselfishness unatucost sana.
   
 18. Nailyne

  Nailyne JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kila kitu kina faida na hasara, so hayo unayoeleza ni madhara ya technologia ya simu za mkononi! computer, tv, hizo zote ni technologia ambazo zina madhara mengi tu kwa jamii inayozitumia, kwa kifupi mtu anatumia simu yake ya mkononi kwa vile atakavyoona yeye inampendeza, na kinachompendeza mwingine katika kutumia simu yake kinaweza kusikupendeze wewe! mwingine kubeep kwake ni sawa either kutokana na kipato chake kidogo au mahusiano yenu, shangazi yangu kule kijijini akitaka kuongea na mimi ananibeep mi twanga tunaenda hewani na haijawihi kuwa kero kwangu coz najua hali ya kifedha ya shanagzi yangu! lakini mimi nikitaka kuongea na baba yangu nam beep yeye anatangwa, hivyo hivyo suala la pornograph si hata kwenye tv na computer watu wanaangalia hizo picha za ngono? hizo blue movies si zinauzwa kila kona huko mitaani? vipi kuhusu porn kwenye internet ? hata hapa JF si kuna jukwaa lina hayo mambo mkuu?
  kwa maana hiyo kwa sababu kuna hizo kero basi tusitumie simu, tv, computer etc etc? hiyo ndio teknologia na madhara yake, hiyo ni side effect ya teknologia ya simu za mkononi.., huwezi kuzuia matumizi ya simu kwa sababu watu wanabeep,au wanawatch picha za ngono, au wanaaamua kutembea na simu za mezani ili waseme uongo.., ni sawawa na kusema nyumbani kwako hutaweka tv kwa sababu kuna vipindi vinavyoonyeshwa haviwafai watoto wako, au hutatumia servise ya internet kwa sababu utatumiwa picha za ngono! ni suala la jamii yenyewe kujua ni kinawafaa na nini hakiwafai na pale ambapo control measures zinaweza kuchukuliwa hilo pia lizingatiwe!!
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Mar 1, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Title haina kosa, soma habari yote ndio utaelewa!
   
 20. Desidii

  Desidii JF-Expert Member

  #20
  Mar 1, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 1,212
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Hizo red huwa sipendi kabisa hiyo tabia umenifanya nisome taratibu na kuelewa.

  Naongezea kuna wengine eti huwa hawapokei Private namba sijui wanaogopa nini sababu namba za nje ya nchi huwa zinaandika private namba or unknown. Unaacha kupokea mpaka umfahamishe kwa sms ni wewe ndo apokee
   
Loading...