🤣🤣 Uko sahihi, ndiyo maana tukubaliane tusibaki kwenye mifano ya Wamarekani.
Huku Tanzania tunao mifano yetu kabisa. Reginald Mengi ni mmoja wao ameeleza mwenyewe kwenye I Can, I Must, I Will jinsi alivyotoka kwenye familia maskini Machame, akaenda shule bila viatu, mpaka baadaye akatengeneza biashara kubwa.
Said Salim Bakhresa naye aliacha shule akiwa na miaka 14 kutokana na mazingira ya familia na akaanza kujitafutia maisha kupitia biashara ndogo kabla ya kujenga himaya kubwa ya biashara.
Na Erick Shigongo ni mwingine ambaye safari yake ya uandishi na ujasiriamali inaweza kuwa sehemu ya mjadala huu.
Ujumbe ni uleule: mwanzo wetu haupaswi kuwa hukumu ya mwisho ya maisha yetu.