Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 88,281
- 154,415
Hizo habafi hamuambiwi mengi.🤣🤣 Uko sahihi, ndiyo maana tukubaliane tusibaki kwenye mifano ya Wamarekani.
Huku Tanzania tunao mifano yetu kabisa. Reginald Mengi ni mmoja wao ameeleza mwenyewe kwenye I Can, I Must, I Will jinsi alivyotoka kwenye familia maskini Machame, akaenda shule bila viatu, mpaka baadaye akatengeneza biashara kubwa.
Said Salim Bakhresa naye aliacha shule akiwa na miaka 14 kutokana na mazingira ya familia na akaanza kujitafutia maisha kupitia biashara ndogo kabla ya kujenga himaya kubwa ya biashara.
Na Erick Shigongo ni mwingine ambaye safari yake ya uandishi na ujasiriamali inaweza kuwa sehemu ya mjadala huu.
Ujumbe ni uleule: mwanzo wetu haupaswi kuwa hukumu ya mwisho ya maisha yetu.
Reginald Mengi alisimeshwa na wauza kahawa wa Uchagani huko, akasaidiwa sana na mke wake na ukoo wa kichifu wa Shangali.
Bakhresa kasaidiwa na Karume kwa mabaya ambayo Karume aliifanyia familia ya Bakhresa.
Mwanzo wetu hautakiwi kuwa mwisho wa maisha yetu, lakini habari unayoisikia ni kubwa kuliko ulivyoisikia.