Killing machine
JF-Expert Member
- Jul 24, 2022
- 2,397
- 3,447
Kipindi cha JPM, Tundu Lissu alipigwa risasi.
Kikwete, kwa ubavu na nguvu zake, alisaidia Tundu Lissu kuvuka mipaka na kwenda kupata matibabu nje ya nchi.
JPM akazuia watu kwenda kumtembelea Tundu Lissu.
Samia akapuuza zuio hilo na kwenda kumtembelea Tundu Lissu nchini Kenya.
Ghafla, JPM akafariki dunia na Tundu Lissu akarudi Tanzania kwa ruhusa ya Samia.
Ghafla tena, Tundu Lissu akawa na mgogoro na Samia.
Hatujakaa sawa, Tundu Lissu yupo mahabusu akikabiliwa na kesi ya uhaini, mara paap! Nchimbi anajiuzulu.
Wakati huo Tundu Lissu bado yupo ndani.
Kisha, kufumba na kufumbua, Tundu Lissu anaachiwa kwenye tuhuma za uhaini, lakini anafungwa kwa kosa la uchochezi.
Kesho yake, tusishangae kusikia ametoka kwa msamaha wa Rais Samia.
Mara paap! Tundu Lissu anakuwa Rais, Nchimbi Waziri Mkuu, au kinyume chake.
Baada ya hapo, tusishangae kuona baadhi ya watu waliopo sasa kwenye serikali wakijumuishwa katika serikali ya Tundu Lissu.
Na kwa siasa za Tanzania, huenda Tundu Lissu akawa anaiongoza CCM B, akishirikiana na Nchimbi, ingawa sijui kipindi hicho CCM B itakuwa inaitwaje.
Je, mtauliza kwa nini?
Kwa sababu sisi Watanzania tuna tabia ya kusahau haraka.
HII NDIYO SIASA!