Ushuru wa mazao warejeshwa tena

Ushuru wa mazao warejeshwa tena

Ss Jr

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2018
Posts
577
Reaction score
451
Katika hali isiyokuwa inatarajiwa ushuru wa soko umerejeshwa bila kujali kiwango cha mazao/mizingo inayoletwa masokoni.

Kutokana na tamko la Rais kuwa wakulima ambao wataingiza sokoni mazao yao, kusafirisha mizigo ya mazao ambayo itakuwa chini ya tani moja hawatalipishwa ushuru, cha kushangaza Jana nikiwa kwenye soko nilimsikia Afisa mtendaji wa kata akitangaza kuwa kila mwananchi atakaye hudhulia sokoni na kiasi chochote cha mazao atatakiwa kulipia ushuru waTsh 500.

Sasa swali ni je, ni mazingira gani yaliyomkuta rais wa wanyonge hadi akaamua kuurejesha ushuru huu?

Je, ni picha gani inaonekana kwa watanzania kugeukwa ghafla na kuanza kutozwa ushuru huo, au ndiyo tuseme kuwa wanyonge wameisha Tanzania waliobaki wanapaswa walipe ushuru?

Je, kudanganya watu wazima ndiyo ukomavu wa kisiasa kwa ajili ya kujipatia vyeo/nafasi za kiuongozi?

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika.

Nawasilisha kwenu tujadili , matusi hayaruhusiwi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lawama zisizo na kichwa wala miguu aise sasa 500 tu fujo hivi

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Ok, ila ukiona mtu anatoa tahadhari ya kutusiwa, basi ujue yeye mwenyewe ndio mtukanaji mzuri, turudi kwenye mada, ni mazao gani unalima, maana yaweza kua huo ushuru ni wa wale wachuuzi wanaokaa sokoni na si wa mkulima!
 
Nimesema ushuru huo habagui kila mtu anayeingiza mzigo sokoni hata kama ni kilo 5 za mahindi au mkungu wa ndizi atalipa ushuru huo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok, ila ukiona mtu anatoa tahadhari ya kutusiwa, basi ujue yeye mwenyewe ndio mtukanaji mzuri, turudi kwenye mada, ni mazao gani unalima, maana yaweza kua huo ushuru ni wa wale wachuuzi wanaokaa sokoni na si wa mkulima!
Kwani Rais alisema walanguzi wa mazao chini ya tani moja walipe ushuru?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesema ushuru huo habagui kila mtu anayeingiza mzigo sokoni hata kama ni kilo 5 za mahindi au mkungu wa ndizi atalipa ushuru huo

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini nakumbuka katazo la ushuru la Mh Rais kwenye mazao kama lililenga kwenye issue ya kusafirisha tu, hakuwahi kugusia issue ya sokoni na ndiyo maana alikuwa anasisitiza kuwa we chukua tani moja peleka, kachukue tani moja tena peleka lakini habari ya sokoni hakuwahi kuizungumzia naona tusimuwekee maneno kinywani mh Rais wetu
 
Sawa acha niwe mdogo wako unielimishe

Sasa hivi jero tu watu ndio walaumu aliyakuwa hata ukipeleka mikungu ya ndizi hamsini ni jero tu
Hahaha, hii imekuzidi Uwezo ndogo wangu. Kaa pembeni wenye akili kubwa tupite. Sikushangai kwakuwa hata viongozi wako wakuu unafanana nao,hakuna wa kukurekebisha

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Katika hali isiyokuwa inatarajiwa ushuru wa soko umerejeshwa bila kujali kiwango cha mazao/mizingo inayoletwa masokoni.

Kutokana na tamko la Rais kuwa wakulima ambao wataingiza sokoni mazao yao, kusafirisha mizigo ya mazao ambayo itakuwa chini ya tani moja hawatalipishwa ushuru, cha kushangaza Jana nikiwa kwenye soko nilimsikia Afisa mtendaji wa kata akitangaza kuwa kila mwananchi atakaye hudhulia sokoni na kiasi chochote cha mazao atatakiwa kulipia ushuru waTsh 500.

Sasa swali ni je, ni mazingira gani yaliyomkuta rais wa wanyonge hadi akaamua kuurejesha ushuru huu?

Je, ni picha gani inaonekana kwa watanzania kugeukwa ghafla na kuanza kutozwa ushuru huo, au ndiyo tuseme kuwa wanyonge wameisha Tanzania waliobaki wanapaswa walipe ushuru?

Je, kudanganya watu wazima ndiyo ukomavu wa kisiasa kwa ajili ya kujipatia vyeo/nafasi za kiuongozi?

Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki Afrika.

Nawasilisha kwenu tujadili , matusi hayaruhusiwi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtendaji wa kata? Duuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lakini nakumbuka katazo la ushuru la Mh Rais kwenye mazao kama lililenga kwenye issue ya kusafirisha tu, hakuwahi kugusia issue ya sokoni na ndiyo maana alikuwa anasisitiza kuwa we chukua tani moja peleka, kachukue tani moja tena peleka lakini habari ya sokoni hakuwahi kuizungumzia naona tusimuwekee maneno kinywani mh Rais wetu
Sio kweli mbona ulikuwa hautozwi kwa mazao isipokuwa kwa wauzaji wa bidhaa za viwandani. Kama unabishi kwamba hakukataza tafuta clip zake usikilize kwa makini bila shaka utakubaliana na mimi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa acha niwe mdogo wako unielimishe

Sasa hivi jero tu watu ndio walaumu aliyakuwa hata ukipeleka mikungu ya ndizi hamsini ni jero tu

Sent using my iPhone using jamiiforum app
Ujuwe,ninyi mlio wengi mnatetea bila kuona factors zinazosemwa? Nitakuelimisha, na wewe utawaelimisha wenzako japokuwa ni ngumu sana kuwaelimisha.

1. Shida siyo 500,Bali urudishwaji wa wa hiyo 500. Kama aliondoa hadharani, arudi hadharani atuambie kwanini anarudisha,tutalipa bila kung'unika.

2. Kuhusu kununua korosho, alipoona wakulima wanapunjwa,maamuzi yake alitakiwa ayapeleke bungeni yajadiliwe na kufanya mchakato wa kupata pesa za kununulia.
Kafanya maamuzi hadharani kachukua hatua peke yake,amekwama sasa anashindwa kuliambia taifa kilichokwamisha, hata taifa na wakulima kupata hasara.

Mambo mengi yahusuyo uendeshaji wa nchi yanafanyika kiholela tu,bila kufuata taratibu za kisheria tena na mtu mmoja. Watu wanajitahidi kushauri kwa upendo wanachuliwa ni wahaini na wachozezi

MADHARA YAKE NDIYO HAYA.

Wale waliokuwa wanashauri kwa upendo wakazimwa kwa nguvu ya dola, WANAGEUKA KUWA WAZOMEAJI MNAPOSHINDWA.

WATU HAO HAO WANAWEZA HATA WAKAFANYA HUJUMA ZA KUSUDI ILI MSHINDWE NA MUPATA AIBU.
KWENYE HILI HATA CCM WAMO. Kule kwetu kuna msemo unasema hivi, AHEKERELA UNGARA KUMOYU KWA TIMBA. Tafsiri yake ni kwamba, anacheka kicheko cha KAA, lakini moyoni ana chuki.

Ukikutana na mdudu KAA, utaona anakufurahia kwa kutanua mikono utaamini anakupenda, akulaki. PELEKA MKONO UONE.

Kundi hili limebeba watu wengi, maaskari, wakulima, bodaboda, watumishi wa uma,wabunge wengi hasa wa ccm na wasukuma pia, na kadha wa kadharika.

RAI YANGU:
Hata kama mmechelewa,lakini mnayo nafasi ndogo mwaweza itumia.
1. Rudini kwenye utawala wa Sheria,unaofuata na kutii katiba ya nchi.

2. Ifungulie demokrasia mlikoifungia ili muijuwe nguvu ya adui yenu ndani na nje ya ccm.

3. Viachieni vyombo vya habari viwasaidie kufichua maovu na kuwakosoa ili muone mnapokosea.

4. Viacheni vyombo vya ulinzi na usalama viwatumikie watanzania na siyo ccm,kwakuwa hata hao wanaowakosoa ni WATANZANI.

5. Ziacheni taasisi mbili mbali zitoe elimu ya uraia ili muongoze kwa raha.
Wengine watakuja kutoa elimu.

MWISHO:
AMANI NI ZAO LA HAKI.
KWANZA HAKI KISHA AMANI
NCHI HAIJENGWI NA MAAMUZI YA MTU MMOJA

Fact

Back
Top Bottom