Mchumi90
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,159
- 1,450
Tumsifu Yesu Kristu (TYK)
Ndugu wanajukwaa niwatakie heri na Noeli. Tunasherehekea kuzaliwa kwa mfalme wa amani Yesu mwana wa Mungu.
Leo katika sali yangu katika moja ya parokia, nimeona na kujifunza haya.
::
1. Hakuna nguo mpya.
Watoto wengi hata watu wazima kwa mwonekano tu nguo walizovaa sio mpya. Hii ni ishara kwamba mifuko imetoboka na sio kama ilivyokuwa zamani watu kumeremeta.
::
2. Akina dada hawajasuka nywele.
Dada zetu zamani walikuwa wanapendeza kweli na nywele zao. Leo nimeona asilimia kubwa wamechana na kufunga nywele na ni kavu kweli. Aiseee kweli vyuma vimekaza.
3. Upande wa sadaka nadhani mapadre ndio wanajua, kwa hiyo siwezi kulisemea.
:
:
Nimewaza sana kwa kweli. Hali ya uchumi si rafiki kwa wananchi wetu, sidhani hata kama pilau litalika kama zamani.
WITO WANGU:
TUTAFAKARI KAMA TAIFA TUMEKOSEA WAPI NA TUSIFANYE MAKOSA TENA.
Ambao hamjaalikwa karibuni sana kwangu kuna vibia kidogo, maana na mimi nimeshindwa kwenda kwenye sensa Moshi.