Ushuhuda; Uvumilivu unalipa

Ushuhuda; Uvumilivu unalipa

tax compliant

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2016
Posts
1,211
Reaction score
1,200
Hakika Mwenyezi Mungu ni mkuu.
Habarini za usiku wakuu, binafsi sijambo kabisa.

Niende moja kwa moja kwenye mada, miezi kadhaa nyuma nilikuja humu ndani nikiwa naomba kazi, mods watanisaidia kupandisha zile threads, baada ya kukosa kazi (NB, JF mdada anasaidika haraka kuliko mwanaume) niliamua kujitolea tu kuwasaidia watu bila malipo ya aina yoyote na hapa nilipata watu wengi tu ambao walikua na matatizo mbalimbali na kweli wengi tu niliwasaidia na waliopenda wao kwa hiyari yao walinipa kifuta jasho (nilikua natumia nauli yangu kumfuata mtu na wala sikuwahi kumdai mtu hata compensation ya nauli sababu niliahidi ni FREE, absolutely FREE) lakini nashukuru ni katika kujitolea huko nilimpata mtu aliyevutiwa na quality ya kazi niliyokuwa nafanya, kutunza muda, uaminifu na panctuality yaani kwa kifupi nilikua auditing firm inayotembea (sijisifii).
Nilifanya kazi pale muda kidogo nikaja nikapata majanga (mama mwenye ofisi alileta mapenzi kwenye kazi) mods mtanisaidia kupandisha na hii na nakumbuka nilikuja kuwaomba ushauri ila ebhanaeee badala ya watu kunishauri watu wakajaa PM kuomba namba ya yule mama😱🙁🙁 ila mwisho wa siku nikaamua kuacha kazi na nililipwa visenti vyangu hivyo nikaamua kuanzisha ujasiriamali huku mtaani, biashara ilikua ngumu mwanzo ila baada ya muda nikawa napata walau hela ya kula na pango maisha yanasogea.
Mwezi wa saba TRA wakatangaza nafasi za kazi, kwanza nilipoliona tangazo tu nikapiga sala ya nguvu sababu nilijua fika bila uwezo wa Mungu akili zangu si kitu na pia ningefeli ingeniwia vigumu kukubali matokeo (ukisali ukafeli unakuwa unajipa moyo kwamba pengine haukua mpango wa Mungu), niliomba nafasi zote nilizokua na vigezo na kati ya nafasi tatu niliitwa kwenye oral interview kwenye nafasi mbili (customs officer II na revenue officer II). Kufupisha masimulizi nilifanya interviews zote na namshukuru sana Mwenyezi Mungu despite the fact kwamba simjui mtu utumishi na wala sina ndugu huko TRA nimeitwa kazini na nategemea kwenda kuchukua barua yangu 26/10 hapo maktaba.

Kwanini nimeandika uzi huu?

1. Katika maisha ya kila siku kuna muda unaona vitu haviendi kama ulivyopanga ukizingatia tunakuwa na expectations kubwa sana tunapokua vyuoni, ukiona mambo hayaendi usikate tamaa, kuwa mbunifu, usiogope kufanya kazi bure na endelea kuamini kuna siku yote yatakua historia.
2. Hata kama unajiona una akili kiasi gani usije hata siku moja ku underestimate uwezo wa Mwenyezi Mungu. (kama unaamini uwepo wake).
3. Usikubali kuuza utu wako kwa ajili ya material things, jiheshimu, jipende na simamia kile ambacho unaamini ni sahihi no matter what might be the cost.
4. Ukifulia hutamwona yeyote pembeni yako, si rafiki si ndugu isipokua wazazi wako labda na marafiki kadhaa, tafadhali nakuomba ukifanikiwa usiwasahau waliokua nawe kipindi hicho (sisemi nimefanikiwa ila tangu jumamosi nimepata simu na sms za watu ambao nilishawasahau , classmates n.k na wengine ni ndugu wa ukoo hata siwajui).
5. KUKUKUMBUSHA USIKATE TAMAA.

Niwatakie muda mwema wakuu na mnisamehe kwa uzi mrefu.
 

Attachments

Hongera mkuu,,ss wale wanazi walotaka namba za mmama uliwapa? [emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
 
Hongera sana!!

yaonekana utakuwa kichwa sana

ule mtihani wa written ulukuwa balaa!!

Mungu akupiganie ukafanye kazi kwa weledi na haki bila rushwa wala mizengwe wala uvivu.
 
Hongera sana!!

yaonekana utakuwa kichwa sana

ule mtihani wa written ulukuwa balaa!!

Mungu akupiganie ukafanye kazi kwa weledi na haki bila rushwa wala mizengwe wala uvivu.
Asante sana mkuu, uvivu si jadi yangu hivyo ondoa shaka juu ya hilo@Englishlady
 
Back
Top Bottom