Ushuhuda: Nilikimbia Ualimu Kuepuka Matatizo

Pole sana. Ulichukua uamuzi wa maumivu. Sikulaumu kwa lolote. Kila mmoja atabeba mzigo wake. Sawa nami nina watoto wanahitaji kufundishwa, lakini lazima na mwalimu ale, avae, alale pazuri etc. kama havipo afanyeje! Hao wanasiasa watoto wao hakuna anayekwenda ualimu. UAMUZI SAHIHI
 
Asante Mpwa, niliumia sana mwanzoni niliteseka na kutengwa na baadhi ya wana familia kuwa nimeacha kazi, lakini ninavyoongea hivi leo, nashukuru MUNGU ninaweza kuwasaidia pia, maana kwa salary ya ualimu na mimi ningeishia kuomba omba!!!
 
Bora tuandae taifa la vibaka na wabakaji kuliko kuandaa taifa nyonge lenye watu waoga na wanafiki kama taifa letu. Jana nilimsikiliza Rais aliyetokana na Chama Cha Magamba (inasemwa eti hata mimi ni Rais wangu...) lakini kusema ukweli sikumuelewa. Alitumia muda mwingi kuudanganya Umma eti serikali yake haitathubutu kuwalipa watumishi wa Umma, wapatao laki tano hivi, kwa kutumia mapato ya nchi zaidi ya asilimia 80. Lakini alisahau kuwaambia ukweli wa mafisadi wachache tu nchi hii wanaomiliki ukwasi kuliko mali zote za serikali. Kusema kwamba serikali yake haitawalipa walimu ni sawa na kusema, liwalo na liwe! Si anajua watoto, wajukuu, wake, wakwamwana, mashemeji, vipusa...... wote wanasoma nje ya nchi? Na wale wanaosoma nchini sana sana watakuwa wanasoma Feza Schools ambako karo yake ni shilingi milioni saba kwa mwaka kwa mtoto wa chekechea. Kwa hiyo walimu wafundishe wasifundishe hilo ni shauri lenu maskini wakubwa!!! Hayo ndiyo niliyoyasoma akilini mwa mkubwa yule aliyekuwa anauma na kupuliza pale mbele ya wahariri wa vyombo vya habari!
 
Mpwa umesema ukweli kabisa
 
Siyo siri inasikitisha, ninao wadogo zangu (dada zangu wawili) ni walimu nikiangalia maisha yao yalivyo najiuliza, "hivi kama isigekuwa kazi za waume zao, hawa wadogo zangu wangekuwa na hali gani?", Inasikitisha siyo siri!!!!!
 
sasa imagine inakluaje kwa mwanaume? hali ni mbaya sana halafu umeoa labda mwanamke hana kazi
Siyo siri inasikitisha, ninao wadogo zangu (dada zangu wawili) ni walimu nikiangalia maisha yao yalivyo najiuliza, "hivi kama isigekuwa kazi za waume zao, hawa wadogo zangu wangekuwa na hali gani?", Inasikitisha siyo siri!!!!!
 
bro pole sana!! teachin ni kazi ngum hasa kwa hili linchi letu!! mi binafsi ningekushaur kama una weza ni bora uchek mishe nyingine kama biashara au kama unaweza rudi chuo ukachukua master au degree ya kitu kingine!!! pole sana na hayo ndo maisha ya hapa bongoland!
 
Mpwa nilishakimbia huko muda tu hebu soma mistari ya mwisho hapo
 
Hongera kwa kufanya maamuzi sahihi, ungezeeka kabla ya umri wako
 
asante kwa pongezi ila there is so much to be done urgently otherwise, hilo kundi linalipoanda huko chini litakua hatari sana kwa usalama wa Taifa
Hongera kwa kufanya maamuzi sahihi, ungezeeka kabla ya umri wako
 
kaka poa, ulichoamua ni sahihi lakini ni wachache wenye maono kama yako, na wengi ni waoga wa kufanya maamuzi magumu..
 
Asante Mpwa, niliumia sana mwanzoni niliteseka na kutengwa na baadhi ya wana familia kuwa nimeacha kazi, lakini ninavyoongea hivi leo, nashukuru MUNGU ninaweza kuwasaidia pia, maana kwa salary ya ualimu na mimi ningeishia kuomba omba!!!

Hapo ndio shida ilipo...
Familia hazituelewi na kuonekana unachagua kazi
Anaejua ugumu au uzuri wa kazi ni alieifanya sio anaekutegemea.
Hongera kwa uamuzi wa kijasiri
 
Hapo ndio shida ilipo...
Familia hazituelewi na kuonekana unachagua kazi
Anaejua ugumu au uzuri wa kazi ni alieifanya sio anaekutegemea.
Hongera kwa uamuzi wa kijasiri
yea yeah uko sahihi kabisa
 
Mpwa wangu MANI, Paloma zumbemkuu saudari na wengineo wengi....hivi ndivyo Mpwa wenu alivyoukimbia ualimu kwa uamuzi wa maumivu....mgumu kuliko, bado naupenda sana ualimu lakini si ktaika mazingira ya kujitesa.....

Pole sana mpwaa.
Kwa sasa unajishughulisha na nini? Au bado unaendelea na ualimu?
 
Pole sana mpwaa.
Kwa sasa unajishughulisha na nini? Au bado unaendelea na ualimu?
Hahahahaha animefungua kijiwe changu cha Gahawa pale kwa Mtogole Mpwa una visa wewe...mengine tutaongea nje ya jukwaaa bhana naogopa mtakuja kunikopa
 
Pole sana mpwaa.
Kwa sasa unajishughulisha na nini? Au bado unaendelea na ualimu?

Mpwa Elli anasema hataki kufundisha watoto ambao hawako tayari kusoma kutokana na sababu kadhaa wa kadhaa haswa vitendea kazi !
 
Last edited by a moderator:
Mpwa huo ndio ukweli bhana, yaani unawaonea huruma maana inafikia kipindi wewe Mwalimu unapata taaabu kubwa kweli kuelezea jambo na watoto wenyewe hawajala kitu wanaumwa njaaa, shule haitoi hata maji ilifikia kipindi hata vyoo vya shule havitumiki tena (serious)
Mpwa Elli anasema hataki kufundisha watoto ambao hawako tayari kusoma kutokana na sababu kadhaa wa kadhaa haswa vitendea kazi !
 
Masaibu ya walimu na hatima ya elimu ya Tanzania

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…