Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 59,809
- 140,806
Japo sijapata hasara kubwa ila ni ushuhuda tosha kwamba demu/msichana hakopeshwi hela bali anapewa kama sadaka!!Nakupa experience.
Wakati namtongoza hakuonyesha uroho wa hela,mara nyingi nikikutana naye alikuwa ni mtu wa stori za kujishughulisha kuongeza kipato.
Mwanzo alikuwa mgumu hata kukutana na mimi,ila mwanzoni mwa mwezi wa tatu akaonyesha utayari wa sitaki-nataka halafu akachomekea nimkopeshe laki 5 aongeze mtaji.
Kutokana na mishe mishe zake nilikuwa na imani huyu manzi angerejesha mkopo bila utata,halafu itakuwa kama nimemnyunyizia kuku punje za mchele kuelekea kwenye banda langu.
Siku moja kabla ya kumpa huu mkopo alinibusu shavuni na kunipapasa mgongoni nikajua hapa ndani ya wiki hii ninaweza kula mzigo.
Kesho yake nikampa tena nilikuwa nimeandaa mkataba tuandikishane asinidhurumu,ila alivyonilegezea sauti na macho nikajikuta nimesahau kumsainisha.
Sasa ni mwezi wa 6 hela sijalipwa na dalili hakuna,kila siku ananisimulia matatizo ya familia yake. Hata ule moto wa kumtafuna unakata maana ni dhahiri ile laki 5 nitakuwa ndio kama nimehonga tu.
Ewe kijana mwenzangu pokea huu ushuhuda kwamba manzi hakopeshwi hela,kama unampa basi usiweke kwenye taarifa zako za fedha.
Mwenzio niliingiza kwenye book keeping sasa ninashindwa jinsi ya kufuta entries