USHUHUDA: Miaka 3 bila ya kuugua

USHUHUDA: Miaka 3 bila ya kuugua

Soyuncu

Senior Member
Joined
Nov 20, 2019
Posts
193
Reaction score
228
Habari zenu wakuu polen na hii pandemic ya covid -19 hope mambo yanaenda poa.

Leo nimekuja na ushuhuda wangu bwana ikiwa nina miaka 3 na miezi kadhaa bila ya kuugua au kuumwa.. Ugonjwa wowote ule... ( Alhamdulillah)

Kama kumbukumbu zangu zilivyo kwenye diary yangu mara ya mwisho mimi kuumwa ilikua 03.02.2017. mpaka sasa tarehe 14.04.2020. Kwa maana nimetimiza miaka 3 na miez 2 na siku kadhaa..

Haya Ndio ninayofanya
1. Mazoezi
2. Sivuti sigala
3. Sinywi pombe
4. Sex ( safe )
5. Nakula sana matunda
Sometimes mida ya usiku naandaa tu sahani ya matunda ( but nikiwa na show na shemeji yenu ugali mkubwa LAZIMA uhusike)

6. Nazingatia maelezo ya afya
Kama kulala ndani ya chandarua, Kunawa mikono baada ya kutoka chooni, kuacha choo katika mazingira safi..

7. Shabiki mkubwa sana wa vyakula vya asili
Toka nimezaliwa mpaka sasa sijui nyama za kopo zinakuaje, samaki za kopo zinakuaje, siijui PIZZA wala BUGGER.. In short sio shabiki wa JUNKY FOOD.

Mafuta yangu ya kula natumia ya alizeti nimekosa sana natumia mawese.. Sikumbuki mara ya mwisho kunywa soda ni lini.. Chips napiga ila kwa kutoa hamu tu Nikila chips pemben Kuwe na msosi mwingine kidogo wa kujazilizia!! Tumbo in short chips + Zege nakula kutoa hamu tu.. Na Nikila napitiza hata miezi 6 kuja kula tena..

8. Nakunywa sana maji
Maji kwangu kama mafuta tu kwenye gari kwangu kunywa maji sio mpaka nihisi kiu.. Asubuhi nikiamka kabla ya kupiga mswaki au baada nakunywa Lita na nusu.

Niongeze kitu hapo kwenye mazoezi

Guys nimekua addicted wa mazoezi aiseh!! Siku nikimisi huwa siwi comfortable.. Kabisa. Mazoezi nafanya kwenye kiwanja cha mpira sijaona umuhimu wa kwenda gym wakati hatua kadhaa na ninapokaa kuna uwanja mkubwa tu wa mpira wa miguu..

Mazoezi yapo mengi sana ila naanzaga na jogging kwanza kuzunguka uwanja.. baada ya hapo yanafata mazoezi ya viungo.. & tumbo

PUSH- UP
Ni Zoez Zuli sana kwa sababu Una deal na Uzito halisi wa mwili wako. Binafsi kabla sijaanza kufanya mazoezi kupiga PUSH UP 3 ilikua kazi ngumu sana kwangu.. Ila kwa sasa napiga push up 30 bila ya kupumzika. Nilijifunza kuanza kupitia zile push za magoti ( kneel push- up)..

Licha ya kuto kuugua faida nyingine ninazo zipata kupitia mazoezi..

1. Sex
Hahahhaa aaah hapa bwana kuna balaa performance during sex inakua juu sana.. Hili shemeji yenu mwenyewe shahidi ila tu siwezi kusema mambo ya faragha ya shemeji..yenu hapa wala kumwambia yoyote yule.. Sijui kitandani anakuaje..!! Hata kama sijamuoa..

2. Mavazi
Kama unafanya mazoezi mwili wako Utaji shape vizuri sana ( kama ulikua mnene) so nguo zitakukaa vibaya Mno tofauti na mwili wako ukiwa irregular kuna nguo utazitamani ila utaishia kuziangalia tu..( hiki ndicho kitu ninachokipenda zaidi kwenye mazoezi mwili Una ji shape vizuri)

NB: Licha ya hayo yote ninayofanya ila naendelea kumshukuru mungu kwa kunipa SIHA njema..

Hizo za hapa chini ni baadhi tu ya route zangu kila siku asubuhi na jioni kumbuka

1mile = 1.609 km
Screenshot_20200414-194651~2.jpeg
Screenshot_20200414-185720~2.jpeg
Screenshot_20200414-191551~2.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwambie Mungu azidi kukupa uzima sio wewe tu ni pamoja na generation yako.

Kwa uliyoongea mengi kama kweli unafuatilia, ni sawa kuugua ni issue kwako.

Una damu group gani pia.
 
Hongera mkuu, mimi nakumbuka mara ya mwisho kuumwa ilikuwa 1999, niliumwa malaria, na hii ilikuwa periodic karibu kila mwaka kuanzia 1997,1998 na hiyo 1999.Nilikuwa nakaa hata mwezi na nusu bila ya kwenda shule.

Ukubwani pia wakati niko Secondary zile seasons za malaria zoote just after "kipindi cha masika na vuli" sijapataga kuumwa pia.

Kilichonishangaza zaidi, kuna mwaka wakati niko secondary advance level,wenzangu bwenini chamber wakapataga tetekwanga, nikauliza kwa mama yangu kama nilishawahi kuumwaga huko utotoni ila akaniambia hapana, so nikawa nasubiri turn yangu ya tetekwanga maana ilikuwa watu wanapasiana bwenini ila sikuipata , yaani mpaka leo sijaelewa.

Namshukuru mwenyezi mungu kwa kweli, naendelea kumuomba pia haya mengine atupitishie mbali.


Alexander The Great
 
Yeah Ndio chief wengine wanaenda mpka miaka 5,9,7 kidonge awaijui mimi nafanya mazoez kwa sababu mwil wangu Una nature ya unene.. Nikijisahau6 kidogo tu nanenepa hatali.. Kitambi kama chote
Duh..mbona muda mchache sana mkuu?
Mm sifanyi yote hayo ukiweka mbali shugul zangu za kioa siku na sijui habari hizo za kuugua kwa miaka 8+ hapa hapa mujini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom