Ushuhuda kilimo cha miti na hasa mitiki

Changamoto2015

JF-Expert Member
Oct 1, 2012
773
313
Tumesikia mengi kuhusu kilimo cha mitiki kwamba kinalipa. Tafadhali mwenye ushuhuda na hii biashara atupe abcd .....ya namna gani biashara hii inafanyika baada ya kupanda mpaka miti inapokuwa imekomaa.
 
Tumesikia mengi kuhusu kilimo cha mitiki kwamba kinalipa. Tafadhali mwenye ushuhuda na hii biashara atupe abcd .....ya namna ghani biashara hii inafanyika baada ya kupanda mpaka miti inapikuwa imekomaa.
Mitiki sio kilimo mkuu, ni uwekezaji.
Alafu ukiona mtu yeyote anasifia chochote kuhusu mitiki jua ya kwamba wazazi wake walikuwa na hekima na busara zenye utukufu na wala si akili za sisi tulio wengi humu ndani.
Mitiki ni uwekezaji for future, always future inalipa.
Kama unataka utatue changamoto usithubutu utakufa na presha shambani. Mitiki hukomaa 20yrs na kama ukipanda ardhi husika.
Naomba kuwakilisha.

Sent from my SM-T285 using JamiiForums mobile app
 
Kwa ujumla kilimo cha miti kinalipa ila utarajie faida baada ya miaka 15. Ukiamua kiwekeza katika miti ni vema shamba lisipungue heka 10. Kama utachana mbao ni vema zaidi kuliko kuuza miti.
 
Muhimu usikurupuke kupanda bila ya kutafiti kama hilo eneo miti ya teak itakua kwa matokeo mazuri, (hii ni kwa upandaji wa miti aina yeyote)
Muhimu sana kuzingatia site selection & class, kwamaana miti yako mwanzoni utaiona inakua vizuri, ikishafikisha miaka kadhaa utagundua miti yako hainenepi, hapo utakua umeshapoteza muda, unless uwe ulilenga soko la nguzo, tena sehemu nyingine usishangae hata usipate nguzo za maana.
 
Eight years old teak trees
moments_6c004b3e-cd19-413f-a55f-61da3e6a7410_hi_res.jpg
 
Niliwahi kusikia kuwa kuna benki zinatoa mikopo kwa kutumia mitiki kama dhamana, kuna ambaye anao huo uzoefu atusaidie?
 
Niliwahi kusikia kuwa kuna benki zinatoa mikopo kwa kutumia mitiki kama dhamana, kuna ambaye anao huo uzoefu atusaidie?
Mitiki hutumika kama dhamana ya mkopo. Lakini ni lazima uwe na biashara au mwajiriwa ikiwa kama namna ya kuweza kurejesha mkopo.
Kwa wilaya ya kilombero na ulanga kuna kampuni inaitwa kilombero valley teak co ltd, hawa wanatoa mikopo kwa wakulima kwa mashart ya kuja kuwauzia wenyewe.. hawa hawahitaji mkulima awe na biashara au kazi
 
  • Thanks
Reactions: PYD

Sawa mkuu. Je kuna bank ambayo unaijuainayotoa mikopo ya namna hii?
 
Back
Top Bottom