Ushuhuda: Hivi ndivyo nilivyoshuhudia maandamano ya Kinondoni na jinsi watu walivyopigwa risasi

isupilo

JF-Expert Member
Jan 25, 2015
303
1,254
Niliyashuhudia maandamano ya wafuasi wa CHADEMA na viongozi wao kuelekea ofisi za Mkurugenzi kudai form za kiapo ambazo mkurugenzi alikuwa amezikatilia mpaka saa 12 jioni.

Nina ofisi yangu maeneo ya Kinondoni Mkwajuni.Nikiri wazi kuwa mimi ni mmoja wa waliopigwa mitama na polisi nikiwa nje ya ofisi yangu baada ya polisi kutawanya waandamanaji na kuanza kukimbia hovyo.Walipiga na kusomba kila waliyemkuta,kijana wangu wa kazi(msaidizi ofisini kwangu) walimsomba kwenye defender,mpaka nilipoenda kumkomboa kwa kutoa kitu kidogo.

Wengi tusio na hatia kama Aqwilina na ambao hatukuwa sehemu ya maandamano ndio tulipigwa na kudhalilishwa pasipo sababu.Hatukuwa na sababu za kuanza kukimbia sababu sio sehemu ya waandamanaji na tulikuwa kwenye anuani zetu za kazi.Jeshi la Polisi,pamoja na mazuri yake yote,kutulinda sisi raia na mali zetu,linaelekea kupoteza uweledi na kujua mbinu za kukabiliana na raia wasio na silaha bila nguvu na silaha za moto.

Ninawasikitikia baadhi ya jamaa zangu walio na ofisi jirani yangu,waliosombwa Jumamosi,mpaka sasa wapo ndani na "wamebambikiwa" kesi ya kuwapiga "mawe" polisi.Sijawahi kusimama mahakamani,safari hii nitaenda kuwa shahidi wa hawa ndugu zangu.Hakika sio kila aliye jela ni mhalifu...

Wengi wa mafundi "welding" walio pembezoni mwa barabara ya Kawawa pale Mkwajuni wapo ndani,na wengine wamepigwa na polisi wakiwa sehemu zao za kazi.Mama mmoja jirani na ofisi yetu aliyekuwa nje ya ofisi yake,alipigwa risasi ya mguu,na wala sioni vyombo vya habari vikiamuandika wala kumuhoji.Dada mdogo,alidondokea jirani na ofisi yetu baada ya kupigwa risasi ya kwenye paja.

Gari nyingi zilizokuwa zimeegeshwa,zimeharibika kwa matundu ya risasi.Eneo letu la ofisi,tumeokota maganda ya risasi zaidi ya kumi.Haikuwa bahati mbaya,Polisi walidhamilia kuuwa,hasa wale waliokuwa mstari wa mbele kuongoza maandamano.

Baada ya hali kutulia,tukiwa tumejifungia ndani na baadhi ya majeruhi walioomba kusitiriwa,tuliwapa huduma ya kwanza majeruhi wa risasi wanne,ambao hali zao zilikuwa mbaya kwa kuvuja damu,wote wa majeruhi hao walikuwa ni walinzi binafsi wa viongozi wa CHADEMA(kadili ya maelezo yao) ambao risasi zilizowakuta zilikuwa zimeelekezwa kwa viongozi wanaowalinda.

Ukisimama nje ya ofisi yetu,unaiona barabara kwa chini,hivyo toka waandamanaji wakiwa Studio,tuliwaona wakija kwa wingi,huku wakiwa wamenyanyua mikono juu,wakiimba nyimbo.Sauti za "Tunataka Form zetuuu" zilisikika.Walipovuka kituo cha Mwendokasi Mkwajuni kuelekea bondeni mpakani na Magomeni,gari za polisi kama sita zikatokea kwenye barabara ya mwendokasi.

Polisi wakaziba njia ya mwendokasi,na barabara ya kutoka Kinondoni kwenda Magomeni.Waandamanaji walitumia njia ya UDART,na walihimizana kutotumia njia ya magari ya kawaida kuepusha foleni.Baada ya dakika kadhaa,akashuka polisi na kipaza sauti,akasema "Rai inatolewa kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano,wananchi msitishe maandamano ambayo ni batili...Tii sheria bila shuruti,kutotii amri hii ya Serikali,ni kulazimisha jeshi la polisi kutumia nguvu".

Waandamaji wakaendela kuimba "Amani...Amani...Amani....Tunataka haki yetu....Tunataka haki yetu",wakiwa wamenyanyua mikono juu kama mateka.Polisi mwenye kipaza,akasema kwa niaba ya amri jeshi mkuu,naamuru mtawanyike kwa mara ya mwisho,laa sivyo nguvu itatumika.Haikupita muda,risasi zikarushwa hewani.Sababu ilikuwa magharibi kubwa yenye kiiza,moto wa risasi hewani uliwatisha watu,sie pia tukapatwa na taharuki,tunakuja kufumbua polisi washafika wanapiga watu hovyo na sie tusio walaa na khatia.Nimeona sehemu polisi wanasema walipigwa mawe,sijui mawe toka kuzimu??

Hapo ndio vurugu zilipoanza.Polisi wakaanza kufyatua risasi kuelekea walipo viongozi wa maandamano,nakumbuka kuona Mbowe kapigwa mtama na mlinzi wake akatembela magoti mpaka mtaroni.Akakimbizwa nyumba ya Mama mmoja ambapo sijui alitoka saa ngapi.Bila unafiki,risasi zile ziliekezwa walipo kina Mbowe na wenzake,na hata kama wachunguzi watakuwa makini,watajua kwanini walioumia kwa risasi ni wale waliokuwa upande wa kushoto kuelekea Kinondoni,na wale wa upande wa kulia hawakudhuliwa na risasi.

Upande wa kushoto kama unaelekea Kinondoni toka Magomeni ndio upande wenye nyumba,ambao viongozi wa Chadema na walinzi wao walikimbilia baada ya risasi kurushwa,ndio upande ambao daladala aliyopanda marehemu mwanafunzi ilikuwa inapita.Na baada ya kukimbia,polisi mmoja anaonekana na cheo alipita anasema akiwa na vijana wake wenye silaha za moto "ukiona hao wahuni piga za miguu".

Na swali kubwa wanaulizana,kwani Mbowe kapita wapi,kaelekea wapi??Zile risasi za walinzi wanne(kama kweli ni walinzi kama walivyotuambia) zilikuwa ziwalenge kina Mbowe na kundi lake.Sasa sijui hawa kina Mbowe waliponyokaje zile risasi.Na tunaomba polisi waache kututisha haya maeneo kutaka kujua nani aliwaficha viongozi wa CHADEMA ndani ya nyumba yake.

Sijasomea mambo ya upolisi,wala sijui mbinu za kukabiliana na waandamanaji,mie ujuzi wangu ni ufundi mchundo tu,lakini sikuona sababu ya jeshi kutumia nguvu kiasi kile.Hawa watu wanapita wanaimba,gari ikipita wanaipisha,wanaimba nyimbo "Amani Amani...Tunataka haki zetu" unawapiga na risasi za moto kwanini??

Mtu unamkuta ameshika grenda ofisini kwake,anaunganisha vyuma vya kitanda apate riziki yake,hana mpango na maandamano,unaanza kumpiga mateke ya miguuni,mara kofi...anaacha grenda ipo kwenye moto anakimbilia ndani kujiokoa,wewe polisi unakuwa na akili kweli au matope??Polisi wanapora simu,wanapiga makofi watu huku wanachomoa wallet...Sasa huu ndio ulinzi wa raia na mali zake kweliiii??

Mtoto wa miaka 10 au 15,ambaye anafuata tu maandamano sababu ya zile hamasa na nyimbo,kama vile wale watoto wanaofuata mdundiko,na yeye unamkuta,unampiga makofi,unamnyanyua juujuu na unamtupia kwenye defender.Huyu mtoto,chini ya miaka 18,anakuwa na kosa gani?Huu uonezi una faida gani?Kuna watoto walilazwa ndani tena mchanganyiko na watu wazima usiku kucha,mpaka wazazi wao walipoenda kuwatoa kesho yake.Yanayookena kwenye magazeti na mitandaoni,ni kidogo sana ukilinganisha na unyama mkubwa uliotokea K'ndoni siku ya ijumaa.Hii ndio utawala bora??

Yalipowatokea kina sijui Ben Saanane,tulisema aaa hao nao wamezidi kuisema serikali.Ikatokea kwa Lissu tukasema huyo naye ana uadui sana na serikali na polisi,amekufa yule dogo wa Hananasifu kwa kina Abbas Tarimba,tunamjua na U-Chadema wake na jinsi anavyoikosoaga serikali vijiweni,sasa wanakuja na makofi,risasi na mateke kwa sisi wafundi mchundo,sasa ni sisi tumewakosea nini??Yaani kosa letu kubwa hasa ni nini???Tulikuwa tunayasikia kwa jirani,sasa yameingia mpaka kwetu...Mungu tusaidie.

Halafu mtu anasema maendeleo hayana chama,mara tumtegemeze Mungu,kutwa kucha kumtaja Mungu...Hivi huyu Mungu anapenda marisasi?Mungu anapenda mama aliye ofisini kwake nje amejikalia apigwe risasi?Huyo Mungu wenu ni yupi?Halafu wenye dhamana bado tu wapo ofisini...Najua na leo mtakuja tena kututisha kama jana,mje tu,tushachokaaaaa!!!!Ujinga mtupu...
 
Wapi taasis za diniii?...nchi inapotea,mbona hamzungumzi?
Nchi inaomboleza,haki za msingi kikatiba zinapokwa,mchana kweupe wizi wa kura unaonekana,bila aibu kwa maslah ya kikundi kidogo cha watu,"miungu watu"..
Tanzania inalia kwa ndani,woga na hofu kuu vimetawala,tabaka la watawala haliambiliki,halijali,linachotaka linafanya,halikubali kukosolewa,liko sahihi kwa kila kitu.
Sheria zinavunjwa,nani aulize?..nani ahoji?nani aitwe mchochezi?..mihimili ya bunge na mahakama ni kama haipo,vurugu tupu.
 
Poleni sana, jeshi la polisi baada ya weledi kuomba msamaha bado wanaanza kuwasakama viongozi cdm, ili kujenga mazingira wabambikia kesi mauji! Tumieni busara mtaamsha wengi walio lala.
Hivi waliomba samahani ?
 
Back
Top Bottom