wakukurupuka1
JF-Expert Member
- Feb 17, 2023
- 525
- 1,187
Basi kampuni ya Happy Nation limesababisha ajali jana usiku maeneo ya Ushirombo.
Basi ilo linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam kwenda Bukoba lilisababisha ajali kwa kugonga gari ndogo uso kwa uso na chanzo cha ajali iyo ni overtake sehem isiyo salama.
Dereva wa gari ndogo amepoteza maisha pale pale na hakuna madhara kwa abiria wa basi hilo.
===
UPDATE;
Basi la kampuni ya Happy Nation lenye usajili namba T 642 EBK likitokea Dar kuelekea Bukoba leo hii, limegongana na gari ndogo maeneo ya Ushirombo, Bukombe mkoani Geita.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa aliyekuwa kwenye gari ndogo ni Padre Fabian Bundala aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Jina Takatifu la Yesu Bukombe na Gombera wa Seminari ndogo Malkia wa Mitume - Ushirombo.
Padre Bundala alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, kutokea hospitali ya Wilaya ya Bukombe iliyopo Ushirombo.
Katibu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Kahama Pd. Abraham Maziku akitoa taarifa ya kifo hiki kwa Mapadre wa Jimbo hilo amesema utaratibu na siku ya mazishi vitatangazwa baadae.
---
TANZIA.
Kwa masikitiko makubwa napenda kuwataarifu kuwa Ndugu yetu Pd. Fabian Bundala amefariki dunia muda huu akiwa njiani kupelekwa Bugando, kutokea Hospital ya Wilaya pale Ushirombo. Baada ya kufika maeneo ya Geita hali ilibadirika ghafla na kulazimika kuomba msaada wa kitabibu hapo Hospital ya Geita, na wakati Madaktari wakihangaika kuokoa maisha yake, mpendwa wetu akatuacha. Tuupokee msiba huu kwa Imani kuu, tukimwombea huruma ya Mungu na msamaha wa dhambi zake, apumzike kwa amani mbinguni, amina.
Taratibu za mazishi yake zitatolewa baadaye.
Raha ya milele umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani, amina.
Pd. Abraham Maziku
(Katibu)
===
Paroko wa Parokia ya Jina Takatifu la Yesu Bukombe Padre Fabian Bundala amefariki kwa ajali baada ya gari yake ndogo kugongana na basi la Happy Nation maeneo ya Ushirombo wilayani Bukombe saa sita usiku wa Julai 6. 2023.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imeeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni umakini mdogo wa dereva wa gari dogo.
Akizungumza na Mwananchi jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP, Safia Jongo alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa sita usiku.
"Ajali ilitokea maeneo ya Ushirombo na kosa ni la dereva Padri aliyekuwa akiendesha gari dogo namba T575 CBC aliingia barabarani bila kuchukua tahadhari na kukutana na basi la Happy Nation iliyokuwa barabara kuu dipo ajali ikatokea.
"Majeruhi kwa hali ya nje alipata majeraha ya kawaida lakini inaonvesha alipata maieraha va ndani ambavo hayakuonekana," amesema RPC Jongo.
Taarifa iliyotolewa kwa niaba ya Askofu wa Jimbo Katoliki Kahama Mhashamu Christopher Ndizeye, Katibu Jimbo Katoliki Kahama, Padre Abraham Maziku alisema Padre huyo alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa hospitalini.
"Padre Fabian Bundala alivekuwa Paroko wa Parokia ya Jina Takatifu la Yes Bukombe na Gambera wa Seminari ndogo Malia wa Mitume - Ushirombo alifariki dunia akiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando, kutokea Hospitali ya Wilaya ya Bukombe iliyopo Ushirombo alikopewa matibabu ya awali," amesema.
Alisema mara baada va kufika maeneo ya Geita hali ilibadilika ghafla na kulazimika kuomba msaada wa kitabibu.
Hospitali ya Gita na wakati madaktari wakihangaika kuokoa maisha yake, alifariki.
"Tuupokee msiba huu kwa Imani kuu, tukimwombea huruma ya Mungu na msamaha wa dhambi zake, apumzike kwa amani," amesema.
Mwananchi