Ushirikina wakimbiza walimu Mbozi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushirikina wakimbiza walimu Mbozi

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 27, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,972
  Trophy Points: 280
  Ushirikina wakimbiza walimu Mbozi


  na Moses Ng'wat, Mbeya


  [​IMG] WALIMU 12 wa Shule ya Msingi Chindi iliyo wilayani Mbozi, Mbeya, wameacha kazi kutokana na madai ya kufanyiwa vitendo vya ushirikina. Habari kutoka shule hiyo iliyopo Kata ya msangano na kuthibitishwa na diwani wa kata hiyo, Omary Sinkara zinaeleza walimu hao wameondoka shuleni hapo katika kipindi cha miezi saba ya mwaka huu.
  Mwalimu Elia Ngaya ambaye ni miongoni mwa walimu walioacha kazi baada ya kufanyiwa vitendo hivyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa tatizo hilo limedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja licha ya wao kutoa taarifa kwa uongozi wa wilaya ya Mbozi.
  Akizungumzia kwa kina tukio hilo la kufanyiwa vitendo vya ushirikina vilivyopelekea yeye na wenzake kukimbia na kuacha kazi, Ngaya alidai wakiwa katika mazingira ya shule hupokea vitisho kutoka kwa baadhi ya wakazi wa kata hiyo hasa inapotokea kutoa adhabu kwa wanafunzi.
  Alisema miongoni mwa matatizo wanayoyapata baada ya kupokea vitisho kutoka kwa baadhi ya wazazi wa watoto shuleni ni kuanguka na kupoteza fahamu, kujisikia maluweluwe na wakati mwingine kujikuta macho yakipata giza wakiwa wanafundisha darasani.
  Aliongeza kuwa vituko vingine vya kishirikina wanavyofanyiwa ni wakati fulani kujikuta wakiwa wamelala nje na nyumba zao ambapo pia baadhi ya walimu waliwahi kujikuta wakiwa wamelala porini karibu na eneo la shule hiyo hali ambayo imezua hofu kubwa na wao kuamua kuacha kazi.
  “Katika mazingira kama haya huwezi kuwa mvumilivu na kuendelea kufanya kazi, maana kuna wakati unajikuta uko nje ya nyumba tena ukiwa uchi, vitendo hivi ni vyakidhalilishaji sana kuna mambo siwezi kuyasema hapa ni aibu kubwa,sijui itakuiwaje lakini sisi tumeamua kuacha kazi,” alisema Ngaya.
  Alisema tatizo hilo lilianza mwaka jana na kutoa taarifa kwa viongozi wa serikali ya kijiji na wale wa mila na hali ilitulia kwa muda,ambapo Desemba 17 mwaka huu walimu zaidi ya watano walirudiwa na tatizo hilo, hali iliyowalazimu kufanya maamuzi ya kuondoka shuleni hapo.
  Walimu hao walisema licha ya ofisa elimu wa wilaya hiyo, Gift Kyando, kupewa taarifa za walimu hao kufanyiwa vituko vya kishirikina wakiwa mazingira ya shule aliwatuliza kwa kuwaeleza watafute nyumba nje ya eneo la shule wakati ufumbuzi unatafutwa.
  Mratibu Elimu Kata ya Msangano, Elia Mwanyamba, alisema kitendo cha walimu 12 kuamua kuondoka shuleni hapo limewashtua na kwamba mbali na walimu hao lakini pia wahudumu wa zahanati iliyopo katani hapo nao wametishia kuondoka kufuatia kufanyiwa ushirikina.
  Aliongeza kuwa hadi sasa walimu wawili wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Vywawa kwa ajili ya matibabu baada ya wiki iliyopita kuanguka na kupoteza fahamu.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,972
  Trophy Points: 280
  Kwenye mazingira haya kweli elimu itafika huko vijijini au tutaishia kujengea popo nyumba za kulala na kujisaidia?
   
Loading...