Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Kwa kutazama mambo kijuu juu, unaweza kushangaa kwanini Serikali ya Marekani ilidaiwa kukwamisha upelelezi dhidi ya Osama bin Laden pamoja na ile mitandao mingine ya ugaidi.
Ukweli ni kwamba familia ya George Bush ni mdau mkubwa katika biashara ya mafuta. Bush mwenyewe alianzisha kampuni yake ya kuchimba mafuta mwaka 1977 katika jimbo la Texas mjini Midland. Kampuni hiyo iliitwa ‘Arbusto Energy’.
Mmoja wa wawekezaji katika kampuni hiyo ni Salem bin Laden, ambaye ni kaka yake Osama bin Laden na rafiki wa karibu sana wa Mfalme Fahd wa Saudi Arabia.
Mwekezaji katika kampuni ya Baba George Bush ni kaka wa mtu aliyedaiwa kuwa alikuwa akitafutwa zaidi duniani kwa tuhuma za ugaidi—Osama bin Laden.
Waswahili husema hili ni “change la macho”.
Wakati Bush anatangaza kumtafuta Osama ‘akiwa hai au amekufa’ na kuahidi kitita cha dola milioni 25 za Marekani kwa atakayemletea kichwa cha Osama, Wamarekani wengi hawakujua kuwa kaka yake Osama, Salem bin Laden, ni mshirika mkubwa wa kibishara wa Rais wao—George Bush.
Uwekezaji wa bin Laden katika kampuni hiyo ulikuwa ni wa dola 50,000 za Marekani. Kutokana na kifo cha Salem bin Laden kilichotokea kwa ajali ya ndege iliyogonga nyaya za umeme barabarani Ijumaa ya Mei 29, 1988 katika mji wa Texas, maslahi yake katika kampuni hiyo yalichukuliwa na mfadhili wa al-Qaeda, Khalid bin Mahfouz, ambaye alikuwa tajiri wa Saudi Arabia aliyeishi Ireland hadi alipofariki dunia Jumapili ya Agosti 16, 2009.
Jonathan Beaty katika kitabu chake, ‘The Outlaw Bank: A Wild Ride into the Secret Heart of BCCI’, anaandika hivi: “Katika mwaka 1996, mkuu wa ujasusi wa Saudi Arabia, Turki bin Faisal, na Khalid bin Mahfouz walikutana mjini Paris (Ufaransa) na mwakilishi wa al-Qaeda.
“Walikubaliana kuendeleza mipango yao ya awali iliyoandaliwa kati ya familia ya kifalme ya Saudi Arabia na familia ya Osama Bin Laden, ambapo kwa kupewa fedha, al-Qaeda ilikubali kutoishambulia Saudi Arabia. CIA walionesha ripoti ya ndani inayoonesha wahisani wengi wa Saudi Arabia waliokuwa wakifadhili magaidi. Jina la Osama bin Laden lilikuwamo ndani ya ripoti hiyo.”
Kwa kulitazama na hilo, utakuwa umeona kuwa bin Mahfouz, ambaye aliwahi kutuhumiwa kuwa mfadhili wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda ambao Osama ambao anadaiwa alikuwa bosi wake alikuwa mwekezaji katika kampuni ya George Bush. Mwaka 1982, kampuni ya ‘Arbusto’ ilibadilishwa jina na kuitwa ‘Bush Exploration’, ikiwa ni mwaka mmoja baada ya mmiliki wake, George H. W. Bush, kuwa Makamu wa Rais wa Marekani chini ya utawala wa Rais Ronald Reagan.
Kampuni ya ‘Bin Laden Group’, ambayo awali ilijulikana kama ‘Bin Laden Brothers Construction’, ni mojawapo ya makampuni makubwa ya ujenzi katika Mashariki ya Kati.
Ikiwa na zaidi ya wafanyakazi 40,000 duniani kote, kampuni hiyo ina uhusiano wa muda mrefu na Serikali ya Marekani pamoja na familia kubwa za nchi hiyo, kama vile familia ya Bush.
Kampuni hiyo, ‘Saudi Binladin Group (SBG)’, ilianzishwa mwaka 1931 na Sheikh Mohammed bin Awadh bin Laden (1908-1967), ambaye uhusiano wake na mwanzilishi wa taifa la Saudi Arabia, Abdel Aziz al Saud, uliifanya kampuni hiyo kupata kazi nyingi za ukandarasi ikiwa ni pamoja na kukarabati misikiti ya Maka na Madina.
Mohammed, ambaye alikuwa na wake 22—au zaidi—na watoto 53—au zaidi, pia ni baba mzazi wa Osama bin Laden. SBG ndiyo kampuni ile ile iliyojenga uwanja wa ndege nchini Saudi Arabia kwa ajili ya kituo cha kijeshi cha Wamarekani wakati wa Vita ya Ghuba pamoja na mahandaki nchini Afghanistan, kwa msaada wa Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA), ambayo baadaye Wamarekani waliyalipua kwa mabomu yao wakati wa uvamizi nchini humo baada ya Septemba 11, 2001.
Charles W. Freeman, mwanadiplomasia wa Marekani na mwandishi wa vitabu ambaye amezitumikia Wizara ya Ulinzi na Wizara ya Mambo ya Nje katika nyadhifa mbalimbali kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30 na ambaye wakati mmoja alikuwa balozi wa Marekani nchini Saudi Arabia, alisema: “Kama kumewahi kuwako kampuni yoyote katika nchi ya Saudi Arabia ambayo ilikuwa karibu sana na Serikali ya Marekani, basi kampuni hiyo ni Saudi Bin Laden Group.” Hiyo ni kwa mujibu wa gazeti ‘The Wall Street’ la Septemba 28, 2001.
Wayne Fagan, mwanasheria wa San Antonio ambaye pia alikuwa mwanasheria wa Salem bin Laden tangu mwaka 1982 hadi 1988, aliliambia gazeti ‘San Antonio Express-News’ kuwa mteja wake alikuwa “…rafiki wa karibu sana wa Serikali ya Marekani.”
Tangu mwaka 1968, Salem bin Laden alianza kuwa kiongozi wa makampuni ya familia ya bin Laden baada ya kifo cha baba yao aliyefariki dunia Jumapili ya September 3, 1967. Mohammed bin Laden alikufa baada ya ndege ya kampuni yake, ‘Beechcraft’, kuanguka wakati ikitua katika uwanja wa Usran, kusini mashariki mwa Saudi Arabia.
Ushirika wa George Bush na Salem bin Laden ulianza baada ya wawili hao kukutanishwa na mtu wa kati aliyeitwa James Reynolds Bath, ambaye awali alikuwa mkurugenzi wa Benki ya Kimataifa ya Biashara na Mikopo (BCCI) na ambaye pia awali alikuwa mmoja wa wanahisa katika kampuni ya Arbusto.
Bath alikuwa mshirika wa karibu sana wa George H. Bush na rafiki wa karibu sana wa George W. Bush. Wakati mmoja wote—Bush na Bath—walifanya kazi pamoja. Mara baada ya George H. Bush kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa CIA mwaka 1976, Salem bin Laden alimteua Bath, rafiki mkubwa wa Bush, kusimamia shughuli zake za kibiashara mjini Texas.
George H. Bush alitumikia wadhifa wa ukurugenzi wa CIA kwa siku 357 tu, kuanzia Ijumaa ya Januari 30, 1976 hadi Alhamisi ya Januari 20, 1977. Bath alisaidia hata kufadhili kampeni za Bush alipokuwa akigombea Jimbo la Texas. Na kama sehemu ya fedha hizo zinatokana na familia ya bin Laden, basi sehemu ya fedha zilizofadhili kampeni za Bush zilitoka katika familia ya bin Laden.
Wakati mmoja kulikuwa na madai nchini Marekani kwamba fedha nyingi ziliwahi kutolewa Saudi Arabia kwa ajili ya kugeuza maamuzi ya serikali ya Regan na Bush (Rais na Makamu wake). Madai hayo yalitolewa hadharani mwaka 1992 na William Howard “Bill” White, mwanasiasa wa Marekani na meya wa zamani wa jiji la Houston.
Kabla ya kuwa meya, Bill White alikuwa mwanasheria na mfanyabiashara, na alikuwa Naibu Waziri wa Nishati kuanzia mwaka 1993 hadi 1995 wakati wa utawala wa Bill Clinton.
Hata hivyo, madai hayo yalichunguzwa na idara ya serikali ya Marekani ya kudhibiti mtandao wa fedha haramu (FinCEN), lakini matokeo yake ikadaiwa kuwa madai hayo hayakuwa ya kweli. Ubishi huo ulifika hadi mahakama ya Texas mwaka 1992, na White alisisitiza kuwa kulikuwa na fedha za Waarabu zilizokuwa zikiwekwa katika akaunti za wanasiasa na wafanyabiashara wa Marekani.
Wakati Idara ya Sheria ya Marekani ikipitia kwa ‘makini’ ushahidi uliotolewa na White, nafasi muhimu sana katika idara hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Robert Mueller. Mtu huyu huyu, Robert Mueller, ndiye aliyeteuliwa na Rais George W. Bush kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI).
Uteuzi huo ulifanyika Jumanne ya Septemba 4, 2001—ikiwa ni wiki moja tu kabla ya mashambulizi ya ‘kigaidi’ ya Septemba 11. Na hiyo ndiyo FBI ile ile ambayo inaiambia dunia kuhusu kile kilichotukia Septemba 11, 2001, na ni FBI hiyo hiyo ambayo karibu kila kauli waliyoitoa ilikinzana na nyingine, na ni FBI hiyo hiyo ambayo hata baadhi ya maofisa wake wanadai kuwa inaficha ukweli wa kilichotukia badala ya kuufichua.
Kiongozi wa Idara ya Sheria ya Marekani, ambayo ilitupilia mbali kashfa kubwa ya BCCI, ambayo ilimhusisha Bush, pia alikuwa ni Robert Mueller. Kama hadithi ya Septemba 11 kuhusu ‘ugaidi’ wa Septemba 11 uliiamini, hata hizo nyingine utaziamini pia.
Source: Rai