THE BEEKEEPER
JF-Expert Member
- Feb 23, 2024
- 1,549
- 7,523
Umeenda kusalimia ukweni, ilipofika usiku ukapewa mahali pa kulala
Usiku wa manane ukabanwa na haja ukaamua uende uani, njia ya kwenda uani inapita jikoni, kama ujuavyo vyoo vyetu vya nje
Katika kuhangaika kupapasa mlango ukaparamia vyombo vikaanguka chini (HILI SIO TATIZO)
TATIZO NI HILI
Ukiwa kwenye harakati ya kuvipanga vyombo ghafla taa inawashwa na unakutana uso kwa uso na mama mkwe (HILI NI TATIZO ILA SIO KUBWA)
TATIZO KUBWA NI HILI
Mama mkwe anakuona umeshika mwiko na sahani, mfuniko wa sufuria uko chini na sufuria ya wali iko wazi , ndio mama mkwe anaamua kuongea kwa upole SASA "BABA KAMA HUKUSHIBA SI UNGESEMA "?