Ushawahi Kutapeliwa?

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Siku moja nilielekea Dar es Salaam, nilipofika kituo cha basi wakati huo ni Ubungo Bus Terminal akatokea kijana Msamaria mwema kabisa akaniomba Begi langu Anisaidie na mimi nikampatia.

Ila kwa kweli ni uzembe wangu kabisa maana yule kijana alikuwa anawahi Harafu mimi hata sikumwambia naelekea wapi. Hivyo mpaka leo hatujawahi Onana na huyo kijana
 
Kipindi nimemalizia chuo, nikaanza kutafuta kazi Kuna Mwalimu mmoja akaniambia kunandugu yake yupo Dar ni Afisa usalama anaconnection so naweza nikamtumia CV na nakala za vyeti sasa lijamaa kila likikaa muda linanipigia cm kuomba pesa tu, lilinipiga Kama laki nakitu na kazi hata kuitwa tu hata interview sijawahi itwa

Sent from my Infinix X652 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana mkuu ndio hivyo wangeni wanapenda kutumia vya watu kupitia uongo.
 
Mwezi ulopita nilikwenda kupanda bus la tanga pale kituoni nikakutana na teja nikafatana nalo mpaka standi. Likatupeleka kwenye bus la Simba mtoto likaniuzia ticket kwa 18,000 wakati bei halisi 13,000. Akaniomba na hela nikampa 2,000 mama..e yule

Lunatic
Kwahiyo badala ya teja kukupiga wewe ndio ulimpiga.
 
Siku moja nilielekea Dar es Salaam, nilipofika kituo cha basi wakati huo ni Ubungo Bus Terminal akatokea kijana Msamaria mwema kabisa akaniomba Begi langu Anisaidie na mimi nikampatia.

Ila kwa kweli ni uzembe wangu kabisa maana yule kijana alikuwa anawahi Harafu mimi hata sikumwambia naelekea wapi. Hivyo mpaka leo hatujawahi Onana na huyo kijana

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mwezi ulopita nilikwenda kupanda bus la tanga pale kituoni nikakutana na teja nikafatana nalo mpaka standi. Likatupeleka kwenye bus la Simba mtoto likaniuzia ticket kwa 18,000 wakati bei halisi 13,000. Akaniomba na hela nikampa 2,000 mama..e yule

Lunatic
Hapo hujatapeliwa mkuu,,kuna wnzio wanatoa 18 na bus hawalioni

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Muache tu huyo atavuna alichopanda maana Mungu huwa hadanganywi...atampa anachokistahili.
 
Nilikua nasikia watu wanatapeliwa simu wanawekewa sabuni,
nikawa nasema haiwezekani ukapewa simu alafu umrudishie akuwekee kwenye bahasha.
maana kwa staili hiyo wale wezi ndio wanabadilisha simu na kukuwekea sabuni bila wewe kujua.

sasa siku moja katika pitapita zangu kariakoo karibu na duka la sandaland pale nikakutana na
wale matapeli wa simu, ilikua tecno spark ile nakumbuka, mmoja akawa anasema
ana elfu ishirini tuu. yule aliye kua akiuza akawa anasema 25, nilipo kua nakatiza karibu yao
yule muuzaj akanambia huyu jamaa ana elfu ishirini mimi nataka elfu 25 tu, akilini nasema
yess hawa ndo wale matapeli subiri sasa niwaonyeshe

nikamwambia hebu lete hiyo simu, nikaangalia nikaikagua kama ndio yenyewe nikaridhika nayo nikaiweka mfukoni
nikamwambia sasa sikia hapa mimi sina pesa twende kwenye kibanda cha mpesa nikakutoleepesa yako

yule jamaa akakubali, sasa wakati tunaenda niliitoa ile simu nikawa naiangalia tena. yule jamaa akaniambia twende haraka
iyo simu nimeikwapua dukani hapo, polisi yenyew sio mbali sitaki kukamatwa hapa , nikamwambia kama unaharaka
chukua sim yako usinchoshe, akasema basi twende tu

tukafika kwenye kibanda nikatoa pesa , nikaangalia sim mara ya mwisho nikampa pesa jamaa nikaweka simu mfukoni
nikaenda kupanda basi, nikasema subiri niweke laini humu nianze kuitumia, aisee nilipoweka mkono mfukoni nakutoa.
sikuamini kitu nilichokua nimeshikilia mkononi mwangu, nilitumbua mimacho kama kobe. nikairudisha mfukoni maana
sikua na ujasiri wa kutupa ile sabuni mule ndani ya basi

nikabaki tu najichekea mwenyewe huku nikiamini atakua kanifanyia mazingaombwe, sio kwa umakini ule nilio kuanao.
basi kilicho fauta tu ni kuanza kuifikiria ile 25 yangu ningeinunulia vitu gani kama nisinge tapeliwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom