Ushawahi kupewa msaada wa gari (lift) ukakosa uhuru?

Alva

Senior Member
Joined
Dec 1, 2017
Posts
119
Reaction score
127
Siku ya kwanza.
Niende moja kwa moja kwenye maada, Je ushawahi kupewa msaada wa gari yaan "lift"?...
Nakumbuka ilikua mwaka 2008 kipindi hicho nipo kidato cha 4, majira kama haya yaan kipindi cha mvua.

Siku moja natoka tuu mida ya asubuhi mvua hiyo nayo inanyesha, mvua ilikua kubwa sana kiasi kwamba hakuna gari la abiria pale kituoni,Ghafla kuna gari ilipaki pale kituoni nikaitwa nikaona bahati iliyoje hii[emoji28]...
Kuchungulia ndani namuona msichana ambaye ni jirani yetu pale mtaani akiwa na mama yake, nikaambiwa panda twende, bila kusita nikaingia ndani ya gari,

Nilifarijika sana maana ile mvua ilikua ni balaa, pia huyu binti alikua akisoma jangwani nami nilikua Azania,hivyo tulitenganishwa na ukuta tuu, hivyo nilipata moyo zaidi kuona nitafika shule salama Salmin..

Baada ya kama km 20 hivi nikaona gari limekua kimya sana, ni vema nikaanzisha maada ili tusahau safari, nikaanza kumsifia yule binti kwamba ni mfano wa kuigwa pale mtaani kwetu, hana mambo ya ajabu ajabu kama wadada wengine[emoji28]...
.
Yule mama alipunguza mwendo wa gari akageuka nyuma kunitizama, mama wa watu macho yalimtoka akafura kwa hasira[emoji849]... hakuongea neno lolote mpaka tunafika shule,

Nilipatwa na maswali mengi sana, nilifanya kosa kuanzisha ile maada? Kwanini yule mama alibadilika ghafla kwa wajihi wake? sikupata jibu, nikakausha tuu.

Siku ya 2
Baada ya usafiri kua shida sana kutokana na mvua, tuliambizana na wenzangu tutembee kutoka Tandika mpaka Temeke huenda tutapata gari,
Mdogo mdogo mpaka Temeke pale karibu na hospitali ya Temeke, abiria kibao wamejaa ghafla gari aina ya defender la polisi likapaki pale,
Mwenzetu mmoja akatoa wazo tupande lile gari maana ni mali ya uma, pia kama gari ni la uma basi litatufikisha safari yetu kutoka Temeke mpaka Azania , kumbe kweli gari lilikua linaenda muhimbili bhana baada ya kumsikia askari aliyekua nyuma kule kama sisi[emoji28], bahati iliyoje hii
Baada ya kufika mataa ya VETA dereva alinyoosha moja kwa moja mpaka karume, tukaomba kushuka wakagoma, askari mmoja akawaomba basi tukashushwa pale boma, safari ikaanza kutembea kupitia mchikichini mpaka Azania...
Toka siku hiyo sikuwahi kuomba msaada wa lift,
 
Aaaaaaaaaah iyo ni kawaida kwenye strugle za maisha wala usijali mdogo wangu ama wewe hujawahi kufukuzwa na ndugu kisa umesahau kufata chakula chs mbwa wake mkuuu
Aisee haya maisha tunapitia mengi sana
 
Mara nyingine mwenye gari ndio anakosa uhuru. Mpewa lift anaanza kuongea na simu mwanzo wa safari hadi mwisho, kabla ya kuongea kapunguza kabisa sauti ya redio.
 
Siku ya kwanza.
Niende moja kwa moja kwenye maada, Je ushawahi kupewa msaada wa gari yaan "lift"?...
Nakumbuka ilikua mwaka 2008 kipindi hicho nipo kidato cha 4, majira kama haya yaan kipindi cha mvua.

Siku moja natoka tuu mida ya asubuhi mvua hiyo nayo inanyesha, mvua ilikua kubwa sana kiasi kwamba hakuna gari la abiria pale kituoni,Ghafla kuna gari ilipaki pale kituoni nikaitwa nikaona bahati iliyoje hii[emoji28]...
Kuchungulia ndani namuona msichana ambaye ni jirani yetu pale mtaani akiwa na mama yake, nikaambiwa panda twende, bila kusita nikaingia ndani ya gari,

Nilifarijika sana maana ile mvua ilikua ni balaa, pia huyu binti alikua akisoma jangwani nami nilikua Azania,hivyo tulitenganishwa na ukuta tuu, hivyo nilipata moyo zaidi kuona nitafika shule salama Salmin..

Baada ya kama km 20 hivi nikaona gari limekua kimya sana, ni vema nikaanzisha maada ili tusahau safari, nikaanza kumsifia yule binti kwamba ni mfano wa kuigwa pale mtaani kwetu, hana mambo ya ajabu ajabu kama wadada wengine[emoji28]...
.
Yule mama alipunguza mwendo wa gari akageuka nyuma kunitizama, mama wa watu macho yalimtoka akafura kwa hasira[emoji849]... hakuongea neno lolote mpaka tunafika shule,

Nilipatwa na maswali mengi sana, nilifanya kosa kuanzisha ile maada? Kwanini yule mama alibadilika ghafla kwa wajihi wake? sikupata jibu, nikakausha tuu.

Siku ya 2
Baada ya usafiri kua shida sana kutokana na mvua, tuliambizana na wenzangu tutembee kutoka Tandika mpaka Temeke huenda tutapata gari,
Mdogo mdogo mpaka Temeke pale karibu na hospitali ya Temeke, abiria kibao wamejaa ghafla gari aina ya defender la polisi likapaki pale,
Mwenzetu mmoja akatoa wazo tupande lile gari maana ni mali ya uma, pia kama gari ni la uma basi litatufikisha safari yetu kutoka Temeke mpaka Azania , kumbe kweli gari lilikua linaenda muhimbili bhana baada ya kumsikia askari aliyekua nyuma kule kama sisi[emoji28], bahati iliyoje hii
Baada ya kufika mataa ya VETA dereva alinyoosha moja kwa moja mpaka karume, tukaomba kushuka wakagoma, askari mmoja akawaomba basi tukashushwa pale boma, safari ikaanza kutembea kupitia mchikichini mpaka Azania...
Toka siku hiyo sikuwahi kuomba msaada wa lift,
Alva mimi kote nimekuelewa ila hapo kwenye gari ya polisi naomba muendelezo tafadhali nimenunua popcorn nyingi naomba malizia hapo chief tafadhali
 
Polisi walighairisha safari ili watukomoe, safari yao ilikua ya muhimbili ila baada ya kugundua sisi pia tunaenda huko wakabadili route , tulishushwa boma,
Kwa hapa Tz ukiwa na uniform za wanafunzi ni ulinzi tosha aisee
 
Nilipewa lifti tukakutana Na mwenye gari njiani akasimamisha swali kwa Dreva huyu nani? Ohoo tunakaa nae mtaa mmoja. Bossi piga chini gari yangu si ya kubeba abilia piga chini. Kama masihara nikashuka wakatembea mtu na bosi wake.
Hahahaha daah pole sana mkuu
 
Kuna dada alikuwa akinipatia lift kwenye baiskeli yake
Kipindi tunasoma sekondari form one
Akinipakiaga nilikuwa nakosa amani
 
Back
Top Bottom