Ushauri wenu wajumbe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wenu wajumbe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Miken, Jun 4, 2011.

 1. M

  Miken Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poleni kwa majukumu wajumbe!!Naleta kwenu kisa changu mnisaidie mwenzenu.Nina mpenzi wangu ambaye tulikuwa naye kimapenzi kwa zaidi ya miaka 2.Akawa ameenda chuo UDOM na kwa sasa anakaribia kumaliza mwaka wa tatu.Tatizo ni kwamba tangia ameenda chuo amebadilika kitabia na kuwa anamind hata jambo ambalo sio lazima kukasirika,akiwa mwaka wa 1,nimewahi kuwa na wasiwasi kuwa kuna jamaa mmoja alikuwa mara kwa mara anafanya mawasiliano ya kimapenzi naye,nilipomwuliza kuhusu ile namba akadai kuwa ni rafiki yake wa kawaida na akafuta jina lake kwenye simu.Baadaye nikatumia ujanja kupata kujua uhusiano na huyo bwana ambaye pia amewahi kushika nafasi kubwa kwenye serikali ya Wanafunzi,huyu bwana inavyoonekana amekuwa nae karibu sana na nilipojaribu kuchunguza nikaambiwa mara kwa mara huenda kuvinjari pamoja mjini Dodoma.Kwa sasa tumekosana na huyu Mpenzi wangu japo sio kwa sababu hiyo na yeye anaonekana kutojali japo bado tunawasiliana.Naombeni ushauri wenu kama nimwache au la kwa sababu namegewa!!Mike
   
Loading...