USHAURI WENU UNAHITAJIKA WAUNGWANA

joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,623
5,037
Habari zenu wana bodi,

Ni kwamba tangu utotoni Nilikuwa na tabia ya huruma kupita kiasi. Mfano mtu akipatwa na tatizo najikuta namhurumia sana mpaka inapelekea niumie sana kana kwamba tatizo ni langu.

Hii hali iliendelea kunisumbua sana ingawa niliona ni kitu cha kawaida tu.
Mpaka leo hii nina miaka 29 bado inazidi kunisumbua bado. Rafiki yangu au ndugu yangu akiwa na tatizo huwa nalifanya kama hilo tatizo ni langu. Japo siyo kwa kupenda bali hiyo hali huwa inakuja automatically.

Nimejaribu sana kupambana nayo ila nothing have been achieved. Je hii hali huwa inasababishwa na nini?

Mbali na hilo, tabia ya upole na ukimya kupita kiasi vimekuwa ni changamoto kubwa sana katika maisha yangu. Hii inapelekea niwe very selective katika marafiki etc.

Japokuwa watu huwa wanaenda mbali sana na kusema kuwa naringa Wakati mimi ni mtu poa na muungwana sana. Sipendi kelele wala msongamano na watu that's why nikiwa home huwa napenda kujifungia chumbani tu mwanzo mwisho. Pia huwa sipendi kampani ya marafiki. Mimi ni one ma army.

Kadhalika, huwa nakuwa selective katika mahusiano kwa sababu huwa sipendi mwanamke mcharuko kupita kiasi ila awe muungwana na ambaye anajua kuongea kwa ustaarabu. Ingawa huwa napata ugumu sana wakati wa kumtafuta mchumba but nikipata namba yake tu huwa hachomoi. Sijui ni kwa nini kwenye kuchati au kuongea kupitia simu niko vizuri kiasi hiki.

Watu wengine huwa wanasema ni udomo zege ila siyo kweli bali kila mtu nahisi amepewa namna ya kuweza kupambana na vikwazo mbalimbali katika maisha.

Waungwana wa JF, hili ni tatizo au?
Ni kitu gani hiki? Au hii hali inasababishwa na kitu gani?
 
Kadhalika, huwa nakuwa selective katika mahusiano kwa sababu huwa sipendi mwanamke mcharuko kupita kiasi ila awe muungwana na ambaye anajua kuongea kwa ustaarabu. Ingawa huwa napata ugumu sana wakati wa kumtafuta mchumba but nikipata namba yake tu huwa hachomoi. Sijui ni kwa nini kwenye kuchati au kuongea kupitia simu niko vizuri kiasi hiki.

Kweli uko vizuri hata kiuandishi, na kiukweki asilimia kubwa ya wanawake tunavutiwa na wanaume wa pole
 
Utakuwa una pepo lisilopenda uchanganyike na wana.

Cha kufanya tembelea nyumba za ibada kwa msaada zaidi
 
Kadhalika, huwa nakuwa selective katika mahusiano kwa sababu huwa sipendi mwanamke mcharuko kupita kiasi ila awe muungwana na ambaye anajua kuongea kwa ustaarabu. Ingawa huwa napata ugumu sana wakati wa kumtafuta mchumba but nikipata namba yake tu huwa hachomoi. Sijui ni kwa nini kwenye kuchati au kuongea kupitia simu niko vizuri kiasi hiki.

Kweli uko vizuri hata kiuandishi, na kiukweki asilimia kubwa ya wanawake tunavutiwa na wanaume wa pole
Kwahiyo ameshakuvutia?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom