Ushauri wenu tafadhali wana MMU

Sijui kwani wazazi wakishaguna nawe ukajipa moyo na kuendelea na mipango yako wengine imewacost lkn si lazima itokee kwako muombe Mungu tu. Nakumbuka ndugu yangu alitaka kuoa kabila flani alipomtajia mzee kabila la mtarajiwa akaguna na kusema hatofaa . Nilimueleza kwa mifano mzee na kumuelimisha mengi lkn hakubadili msimamo na ndugu huyu alioa , baada ya muda flani ile ndoa ikageuka ikawa ndoano mpaka leo kitanzi kinamning'inia ndugu huyo na kujinasua hawezi.
 
Matege
Mbona umeniita mimi sitoki Kanda ya Ziwa.
 
Last edited by a moderator:
MO11
Hahaaaaaaa ulijuaje umeona tunavopigwa vita mkuu tangaza nia basi mahari nitajilipia mwenyewe.
 
Last edited by a moderator:
Akili za kuambiwa pia kumbuka, aonywae mara nyingi akishupaza shingo huvunjika! Kaa chini fikiri na uchukue hatua.
 
Mama yako kukupa mifano 15, humu jf kuna nyuzi kibao za kuhusu hao watu, sasa nini zaidi unataka mkuu?
 
Maskini kumbe amejadiliwa huko hadi aibu mwe mwe mweeeeeee ukwama hebu mtoe ktk aibu hii let her go
 
Last edited by a moderator:
Mauza uza
Hakuna kitu kama hicho hapa duniani asilimia lazima ianzie sifuri hadi mia moja.
 
Last edited by a moderator:
Matege
Hapa umechemsha kwani nyani haoni lake.Huwezi kutuhumiwa ukawa wewe ni hakimu.
 
Last edited by a moderator:
Matege
Nia nishatangaza ila mambo ya kujilipia mahari maana yake unataka kunioa.
 
Last edited by a moderator:
Da Pretty
Hiyo ndio dawa ya waongo maana ni mabingwa wa kusahau
 
Last edited by a moderator:
Mtuwache na ndugu yangu miss chagga.
Kila wakati huwa nasema kabila halina umuhimu katika tabia na mwenendo wa mtu. Ila tunaishi kwa kutegemea tuliyojifunza kutoka kwa waliotutangulia (wazazi n.k.). Tunarithi mengi kutoka kwa wazazi au walezi wetu. Kama wazazi wako walikuwa wanadundana, nawe utaona kudundana kati yako na mwenzi wako ni jambo la kawaida. Cultural differences ndizo zinaleta matatizo katika ndoa mseto.

Mfano binti wa kichagga akiolewa; kwa wazazi wake wanapata mpagazi wa kuchuma kahawa. Hii ni tofauti na makabila mengine mfano Makabila kama ya wasukuma binti akiolewa anaondoka katika kaya ya wazazi wake na kujiunga na na familia ya mume wake. Sasa sikilizia mchagga akiolewa na msukuma hapo ni kijasho maana expectations za wazazi wa pande mbili ni tofauti. Wazazi wa kiume (kwa mfano wetu Wasukuma) wanaona kijana wao kaleta mpagazi katika ukoo na wazazi wa binti wanadhani sasa kahawa itachumwa na kyasaka. Hapo utaona utata unapojitokeza kwa familia ya huyu binti na kijana.

Kama watajenga nyumba, familia ya kiume itajitapa kuwa kijana wao amejenga na kuona ni haki yao kukaa ukoo wote na kuona familia ya kichagga (kwa mfano wetu huu) kutokuwa na haki. Kwa upande wa famila ya kichagga kwanza inasema binti yetu kajenga (siyo mwanaume) na ndugu wa binti wanaona wana haki hata ya kuirithi hiyo nyumba pindi binti yao akifariki. Wakati huo huo Wasukuma wanaimani kuwa mwanamke hajengi ingawa inawezekana ni binti alijitahidi kwa hata kutafuta kababu kakamjengea. Sitaki kuzungumzia suala la kijana (kyasaka) kujenga nyumba ukweni. Wasukuma wataona familia yao ina haki kuishi na siyo Wachagga. Kiuhalisia jaribu kufanya utafiti wa ndoa za mseto kama mfano huu uone ni upande upi unafaidi matunda ya ndoa hiyo.

Imani yangu ni kuwa ifike pahala ndoa iwe ni mtu na mke wake na watoto watakaowazaa, masuala ya familia zetu tuyawache.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…