Ushauri wenu tafadhali wana MMU

ukwama

Senior Member
Joined
Aug 6, 2014
Posts
136
Reaction score
83
Salaam ndugu zangu wana MMU.

Nimekuja hapa mbele yenu ili mnipe ushauri nipo kwenye hali ya sintofahamu maji yamezidi unga ugali naona unaenda kuwa mabuja.Hii inatokana na jana kumweleza mama yangu mzazi adhima yangu ya kumtambulisha kwake my beautiful Onyinye baada ya huu mfungo wa kwarezima.

Mama yangu yupo Kijijini pande za Ukanda wa Ziwa,mara baada hiyo habari mama alifurahi sana na alisema anashauku ya kumwona mkwe wake akanipongeza na kunikaribisha nyumbani .Pia alinitania kwa kunambia kwa jinsi anavonijua ninavyopenda kutoa kasoro wanawake lazima huyo atakuwa ameshushwa tukacheka tukafurahi.

Kimbembe kilikuja pale aliponiuliza kabila la huyo mkwe wake me kwa madaha na kujiamini nikamwambia ni mchaga maskini nilihisi mama yangu akiwa amenyong'onyea, akajibu kama umempenda vizuri nami sikusita nikamwuliza mama mbona umebadilika akanambia hamna tatizo mwanangu akaniuliza tangu ujuane naye ni muda gani nikamjbu mwaka na nusu sasa mama.

Akasema ok ila ilo kabila mwanangu lina tatizo akanipa orodha ya watu wasiopungua 15 nnaowafamu wa maeneo ya nyumbani waliooa wanawake wa kichaga na mwisho wakaangukia pua na wengi wao walibeba na watoto na mali zote za mme pia akanieleza kuwa kwa upande wao kwao ndoa ni raha tu upande wa shida hawapo.

Nilijaribu kumweleza mama mazuri ya Manka wangu ikiwa ni pamoja na yeye kumcha Mungu,anaheshima na hana chembe ya ubinafsi I can declare hata kwenu my Manka ni mtu safi hana hzo tabia.Mama alinijibu kwanza oana naye ndo utajua.Baada ya malumbano ya muda mrefu baina yangu mi na mama kwa shingo upande akakubaliana na mimi lakini in reality mama hajamkubali mkwe wake.

Sasa issue iko hapa my Manka nilishamwambia ajiandae kwenda kutambulishwa na nampenda sana in a way I don't know if I loose her what will happen in my life without her na Mama nampenda sana. If I see my self without Mama hata Manka tusingejuana nampenda sana na niliapa kamwe sitakuja kumkosesha raha na amani sitaki afadhaike nanpenda sana mama.

Please advise me ndugu zangu nipo njia panda.
 
Maneno huumba ndo zote zina ups and down sasa kama ndoa yako kabla tu haijaanza wewe na mama yako mmeanza kum judge huyo dada kabila lake bora usimuoe sababu lolote litakalo jitokeza mama yako atakwambia 'tulikuonya' na wewe uta feel 'my fault sikusikiliza'.
 
Lazima ilivutiwa na weupe wake. Maana watu wa kanda ya ziwa hasa wasukuma wakikutana na wanawake weupe wanakuwa kama zezeta.
 
Your mum is right 1000%, hilo kabila ukipata shida ya ajira au pesa ndo mwisho wa ndoa yako.nina experience nao hao watu, wenyewe kwa wenyewe wanawezana lakini sio ww wa huko kanda ya ziwa utatemwa mchana kweupe siku ukiwa apechelolo,...fuata ya mama please!!
 
Kampeleke akikataliwa tafuta mwingine maana waafrika tunaoa kwaajili ya familia zetu!
 
Last edited by a moderator:
Ndgu Yng Mama Yk Anakupenda Sn.Mm Nakushauri Katika Makabila Yt Oa.Ila Husioe Mchaga, Mpare, Mrangi, Au Mzalamo.Ukioa Makabila Hayo Kazi Unayo.
 
Ndgu Yng Mama Yk Anakupenda Sn.Mm Nakushauri Katika Makabila Yt Oa.Ila Husioe Mchaga, Mpare, Mrangi, Au Mzalamo.Ukioa Makabila Hayo Kazi Unayo.

we una lako jambo.. mtoa mada kama umependa oa tu wachaga hatuna shida. kama unataka maendeleo oa uchagani
 
Upofu wa mapenzi usitufanye tusizione busara za wazazi wetu,mahaba huja na kuondoka kama misimu ya hali ya hewa lakini mapenzi ya kweli ya wazazi wetu hubaki milele vifuani mwao kwani siku zote tunaishi ndani yao na furaha yao ni kuona maisha yetu yanastawi.Hata siku moja usiruhusu watu wa kupita maishani mwako wakutenganishe na wazazi wako wapendwa hapa duniani.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…