Ushauri wenu kwa wale wenye uzoefu na ujenzi

Gluk

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
1,856
2,953
Habari wanaJF
Kuna picha ya mchoro wa nyumba niliiona mtandaoni zaidi ya miaka miwili nyuma ukanivutia sana.
Na nikaona kuwa kanaweza kuwa kajumba ka kuanzia maisha wakati najipanga kupata nyumba ya ndoto yangu.

Lengo nataka kujua gharama ya kusimamisha boma na kupaua basi.
Kuhusu finishing nitafanya taratibu maaana sina haraka ya kutaka kuhamia.
Kiwanja kiko tambalale

Na km kuna fundi anayeweza kufanya kazi hiyo asisite kumwaga hapa details ili tupeane deal.
20200803_021131.jpeg
 
Sijapenda design mlango wa master kutazamana na jikoni. Sio sawa
Mkuu, mleta uzi ameomba msaada wa kuelezwa gharama na si idea za design au uzuri/ubaya wa design yake. Nadhani ameshafunga mlango wa discussion ya aina ya ramani kwa sasa anaomba msaada kujua gharama tu.

Wengi ambao hatujui gharama za Ujenzi tumekaa kimya tu.

Kwa kuwa nyumba ni yake na yeye ndio ameipenda hiyo ramani basi tuheshimu mawazo yake, subiri ujenge ya kwako kisha mlango wa master usitazamane na jikoni.

Sent from my SM-G973F using JamiiForums mobile app
 
Sio mbaya kumshauri. Maana hata akija fundi atamueleza baadhi ya vitu kabla hajamtajia bei. Au wewe unamaindi tukimpa mawazo kama haya? Basi atakupangisha kwenye chumba kimoja
 
Ungetuma floor plan yenye vipimo inakua ni rahisi kufanya makadilio.Hiyo picha uliyotuma ni vigumu kujua vyumba vyako vinaukubwa gani hivyo basi ni ngumu kukadilia gharama.Karibu pia tukujengee namba za ofisi ni 0756928360
 
Habari wanaJF
Kuna picha ya mchoro wa nyumba niliiona mtandaoni zaidi ya miaka miwili nyuma ukanivutia sana.
Na nikaona kuwa kanaweza kuwa kajumba ka kuanzia maisha wakati najipanga kupata nyumba ya ndoto yangu.

Lengo nataka kujua gharama ya kusimamisha boma na kupaua basi.
Kuhusu finishing nitafanya taratibu maaana sina haraka ya kutaka kuhamia.
Kiwanja kiko tambalale

Na km kuna fundi anayeweza kufanya kazi hiyo asisite kumwaga hapa details ili tupeane deal.View attachment 1525516
Kiwanja Kiko mkoa gani?
Umesema kiwanja ni tambalale. Je! Ni aina gani ya udongo upo hapo?

Kama unajenga dar, na unataka kujenga nyumba imara na Bora basi andaa 15m kwa boma na tshs 8-11m kupaua kulingana na aina ya bati utakayotumia. 0655173113 fundi mahiri wa ujenzi
 
Makadirio yako ni very realistic.
 
Boma na kupaua ile M 23 hadi 25! Mbona ghali sana?
Kiwanja Kiko mkoa gani?
Umesema kiwanja ni tambalale. Je! Ni aina gani ya udongo upo hapo?

Kama unajenga dar, na unataka kujenga nyumba imara na Bora basi andaa 15m kwa boma na tshs 8-11m kupaua kulingana na aina ya bati utakayotumia. 0655173113 fundi mahiri wa ujenzi
 
Mkoa ni dar

Nyumba kama hio, bila finishing, block za cement, pamoja na fundi, tayarisha za kuanzia Tsh. 50 milioni
Yani watu wa dar ndio mana hamuishi kuhamahama kwenye nyumba zakupanga,leo kimara kesho magomeni,hata kama hajaweka vipimo lakini kusimamisha boma na kupaua kama kunausimamiz mzuri 20m inatosha.
Gharama za ujenzi hutofautiana kila mkoa hili nalo ni vema likazingatiwa
 
Vipimo napenda iwe mita 8 upana kwa 12 urefu

Back
Top Bottom