Wafanyakazi wa Vodacom na NSN mmejiponza wenyewe. Msitafute mchawi wenu. Ni nyinyi wenyewe. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanyakazi wa Vodacom na NSN mmejiponza wenyewe. Msitafute mchawi wenu. Ni nyinyi wenyewe.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NokiaSiemens, Sep 17, 2012.

 1. N

  NokiaSiemens New Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WanaJF,

  Kabla ya kusoma na kuielewa hii thread inafaa kwanza kupata muda kuipitia ile thread iliyoko hapa:

  www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/322444-vodacom-tz-kwafukuta.html

  Mimi ni staff wa NSN. Kwa sababu naona wenzangu mmelileta huku mtandaoni basi na mimi nimeamua kuleta ukweli ambao walioko nje ya Vodacom au NSN wanaujua.

  Kilichotokea ni kwamba siku ya Agosti 29, 2012 tuliitwa na management kwenye meeting kwenye Town Hall pale Mlimani City karibu na ofisi zetu.

  Tulichoambiwa na kwamba NSN imeamua ku-centralize baadhi ya technical activities kule India. Wote tunafahamu kwamba NSN ni international Company inayo-operate sehemu nyingi duniani kwenye biashara hii ambayo watanzania wengi hawaijui lakini sisi tunaijua inaitwa Managing Service (MS).

  Hiyo centralization itakachokifanya ni kwamba shughuli kama za Network Monitoring na Optimization zitafanyikia India ambako ndiko kuna technical centre kubwa.

  Tuliambiwa hivyo kama presentation na nafasi ya kuuliza maswali ikatolewa. Hakuna aliyepinga wazo hili au stratergy hii ya NSN. Kikai kikafungwa na hadi leo tunasubiri barua za retrenchment. Narudia, hatukupinga wazo hili palepale mkutanoi yaani mbele ya menejimenti. Kisha sisi wenyewe kama staff wazawa wa NSN hatukuwahi kufanya kikao hata kimoja kujadili nini tufanye kuhusiana na taarifa tuliyopewa.

  Sasa kama hatukupinga wazo hili na wala hatukukatazwa kuuliza maswali iweje leo tukimbilie mitandaoni na kuifanya issue kama vile tumeonewa. Mimi nasema hatujaonewa na haya yanayotokea ndani ya Vodacom na hasa NSN yako ndani ya uwezo wetu wala hatukuhitaji kabisa msaada kutoka nje ya NSN au Voda.

  Itakumbukwa kwamba kabla ya mwaka 2004 kulifanyika move kali sana ya kuwaondoa foreigners waliokuwa wame-dominate shughuli zote za Operations/Engineering hapa Vodacom. Move ile ilikuwa nay a wazawa watupu na ilifaulu vizuri na SIEMENS wakaondoka..

  Tulipowaondoa SIEMENS hatukuhitaji kurusha barua mitandaoni. Tulipambana kiume SIEMENS wakaondoka na wazawa tukachukua nafasi. Hebu tujiulize ni lipi ambalo linatokea hapa Vodacom au NSN ambalo sisi kama wazawa tukilisimamia lisitokee litashindikana. Hakuna hata moja. Tuliweza la SIEMENS na kwa hakika kama umoja ungedumu tusingeshindwa lolote.

  Unafiki baada ya kuwaondoa SIEMENS ndiyo uliotuponza. Ni move ngapi za kudai haki zetu tumezifanya humo ndani ya Vodacom lakini kabla hazijamalizika habari zina-leak na wazungu wameshajua mpango mzima na inakuwa rahisi kuusambaratisha. Hawa wazungu walikuwa wanapataje habari za mikakati yetu.

  Ni mara ngapi wazawa tumekuwa tukichoongeana kwa Dietlof yaani yule MD aliyeondoka wa Vodacom. Mtu ulikuwa ukiongea kitu kidogo tu tayari Dietlof kashakijua mapema na timu yake yote ya wazungu. Na waliokuwa wanachonga mdomo ni wazawa wenzetu, watanzania wenzetu. Si wazungu hata kidogo!

  Hivyo, kwa ujumla tulioko NSN na hata wenzetu walioko Vodacom, tusiwadanganye ulimwengu kwamba tumeonewa au kuna mpango wa kutuonea. Tulichokipata na tutakachokipata ni haki yetu tunavuna tulichopanda.

  Leo mtu unaomba msaada mitandaoni wakati hujaonyesha hata chembe ya juhudi za kupambana, unadhani mitandao kama emails na mingine itatoa misaada gani?

  Ambao hamjawahi kupita Vodacom au NSN msitarajie kuna mzawa atamtetea mzawa mwenzake aliye kwenye menejiment post hata kama itakuwa ni kwamba anaonewa kwa kuchinjwa kama kuku. Naamini ataachwa achinjwe na wengine watasema "mwache akome hakuwa anajali wenzake".

  Ndicho kilichotokea zilipotokea tetesi kwamba Human Resource director aliye-resign mwaka jana ali-differ na MD wa sasa ndipo akaondoka. Wengi waliosikia tetesi hizi walifurahi kwenye koridor kwamba afadhali na wenyewe HR sasa yawakute. HR ilikuwa imeshapoteza imani kutetea wazawa hata walipoonewa dhahiri kiasi kwamba mtu ulikuwa ukiamua kupambana basi hufikirii kabisa kutetewa na HR. Miaka ya mwanzoni kuingia HR ulikuwa unatakiwa kubisha hodi na wakati mwingine unaambiwa piga simu hukohuko uliko. Eti siku hizi wanakaribisha watu!

  Hivyo kuandika barua na kuzituma mitandaoni hakuleti tija. Kwanza tujiulize nini kilisababisha tukawaondoa wasio wazawa yaani SIEMENS lakini baada ya SIEMENS kuondoka walioshika uongozi kwa wazawa wakawa wa kwanza kujilimbikizia mali na wengine wana majumba, wana hostels wanapangisha, wana shule kubwa kama ya Mh. Nimrod Mkono au za Mama Lwakatare!

  Wengi wenu ni watoto wadogo ambao maisha mmeyaanza juzijuzi tumewaona mlivyoyaanza kwa kuishi nyumba za kupanga tena kujibana uswahilini kama Tabata, Sinza, Mwenge na kwingineko. Leo mmekaa Voda/NSN mmefanya biashara ya kupata ten percent kwenye procurements. Mmefanya biashara ya kuandikisha minara kwa majina ya ndugu zenu.

  Na kwa sababu minara ya simu hupita maporini au vijijini ambako watu hawana elimu ya uraia basi huko mkawalipa watu kiduchu halafu hela ya kodi ya minara mnaingiza kwenye mifuko yenu mkatajirika mkajenga shule mkataka tuwaite wajasiriamali.

  Baadhi ya Vodacom staff au NSN imefika mahala hadi wanaogopa kupata misiba kwa maana ya kwamba misiba inaumbua na kukufanya ujulikane ulivyo. Kuna msiba mmoja mabosi wa kizungu walihudhuria na wakashtuka sana kuona mfiwa amejenga hekalu ambalo gharama zake hazielezeki kwa staff wa Voda. Inasemekana kwamba wazungu wale wakasahau kwamba wako msibani wakaanza kujadili ukubwa wa jumba lile na kujiuliza alikopata mfiwa pesa za kulijengea!

  Haikupita miezi miwili yule mfiwa akahamishwa idara akapewa "idara hewa" ya watu watatu tu wanaoripoti kwake. Huo ndiyo ukawa mwanzo wa huyo jamaa kuhama Vodacom, na kweli ndani ya miezi minane akaacha kazi na sasa hivi ana bonge la kampuni yake anaendesha biashara nisiyotaka kuitaja kwani wengi Vodacom/NSN mnamfahamu na biashara yake si siri mnaifahamu.

  Mwingine alifariki na baada ya kukaa mwaka mmoja kama meneja wa installation. Kifo chake kilifanya jumba lake lijulikane ambalo alilijenga akiwa ana mwaka mmoja na nusu tangu aupate umeneja huo.

  Sasa hii ni picha kidogo tu, tena ile ninayoifahamu. Bado ile nisiyoifahamu. Mimi sigombi kufika huko mnakokuita mafanikioni. Lakini kosa lenu ni kusahau mbinu iliyowafikisha hapo ilikuwa ni umoja na wala si usaliti. Umoja wa kuwaondoa SIEMENS na ule umoja wa kupigania wazawa apate nafasi za uongozi ndani ya Vodacom. Ni move iliyofanya baadhi wamuinue juu Romeo Khumalo yule MD wa zamani maana yeye ndiye aliyeweka wazawa wengi katika post za juu ndani ya Vodacom.

  Hivyo hoja kwamba wazawa wa Vodacom wanaonewa ni hoja dhaifu. Wazawa mmepewa nafasi tele kujaribisha talent yenu katika Vodacom. Je, mmefanya nini? zaidi ni kwamba mliopata nafasi mkaanza mashindano ya kuonyesha ni nani ana gari la kisasa, tena si moja. Mtu anamnunulia girlfriend wake gari la Tshs. milioni 30! Kumbuka ni girlfriend, si mke wake. Mke analo la kwake.

  Mkashindana kujionyesha na ni nani ana jumba ya kisasa. Tena jumba linajengwa mtu anahamia humo yeye na briefcase yake tu kwani kila kitu kimo na kipya!. Hebu tukushane. Kipindi hiki mnashindana kujenga mkawa wakali kama nini hamtaki kusemeshwa. Kiasi kwamba nimeshahisi kwamba mtu akiwa mkalimkali ndani ya Vodacom basi ujue huyo yuko katika kipindi cha kujenga nyumba au kusimamisha miradi yake. Anakusalimia mara moja tu anaitikia wakati ameshafika mita kumi zijazo. Kama mwanzoni alikuwa anapokea simu yako, basi sasa kila ukimpigia anajibu "nikobusy" na ikibidi hapokei.

  Mlipomaliza kushindana kujenga majumba mkaanza mashindano mengine. Mkaanza sasa kushinda investiments. Wapo ambao mwaka juzi walifikia hatua ya kushindana na matajiri wa nchi hii kugombania nafasi za kuteuliwa ubunge na walikosakosa kuupata. Wapo walioanza kufikiri kuanzisha kampuni kubwa za installations ya mitambo.

  Wengine wakaanzisha hoteli kubwa za kisasa. Wengine wakaanzisha kampuni za ku-supply computer tena tender za kampuni zao zikahisiwa kuwa zina-supply computer za Vodacom hadi wazungu wakashtukia na kuanza kusaka account zao kisiri.

  Wengine wakawa shareholders kwenye baadhi ya kampuni kubwa. Wengine saloon za wake zao au girlfriend zao zikawa ni zile ambazo bei ukitajiwa huamini. Baadhi wakawa matajiri kiasi kwamba hata wakawa wanatumia dawa za kulazimisha kicheko au smiling.

  Dada mmoja aliyekuwa Head wa dept. moja ya IT amefungua shule ya chekechea. Mwenzetu mmoja aliyekua NSN amefungua bonge la shule ya Sekondari huko Nyanda za Juu Kusini. Alikuwa radio Planning kwa muda mrefu kwenye ile idara inayojihusisha sana na kupanga mnara ukae wapi au ukae kiwanja gani.

  Mitandaoni tunalaani mawaziri eti wanaenda ku-spend likizo Ulaya. Mbona ndani ya Vodacom ni wengi wanaenda likizo Ulaya tena kila likizo kwa hela yao. Je, mnamsahau yule dada wa Human Resource ambaye ilipokaribia harusi yake aliona hapa Tanzania hawezi kufanya shopping hadi akapanda ndege kwenda Europe kufanya shopping ya nguvu huko.

  Mitandao na magazeti iliishia kumtangaza Mwamvita Makamba wakati humu ndani ya Vodacom wako wengi kupita maelezo kama yeye. Tena afadhali Mwamvita amezaliwa kwenye familia ambayo watanzania wote tunajua imeogelea kwenye hela. Hawa wengine ni watu ambao tumewaona juzijuzi tu wakijifunza kuendesha magari tena wakigongesha magari kila leo kwa uanafunzi wao wa kuendesha magari.


  Imefika mahala jamii inajua kwamba ukifanya kazi Vodacom au NSN basi wewe ni mtu wa kuongelea mamilioni. Mfanyakazi wa Vodacom au NSN kuombwa mkopo wa milioni mbili na ndugu au rafiki imekuwa ni kitu cha kawaida. Jamii inatuona kwamba wote tunazo. Kumbe sivyo bali ni wachache tu ambao kwa bahati au ujanja umewafikisha hapo.

  Ukijionyesha kwenye jamii au mtaani kwamba huna mamilioni basi unasimangwa kwamba "ni uzubaifu wako kwani inajulikana Vodacom ni mahala pa kutajirika". Wanaosema hivyo vigezo vyao ni hawa Vodacom/NSN staff wanaowaona wanafungua shule za sekondari, wanakwenda likio Ulaya kwa pesa zao, wanakwenda kufanya wedding shopping huko Ulaya.

  Katika hali kama hii utateteaje mzawa wakati amepewa nafasi akaitumia hivi ninavyoeleza tena na zaidi ya hapa!


  Leo baadhi tutaondoka, kufukuzwa au kupunguzwa (retrenchment) toka Vodacom au NSN. Baadhi mnaanzisha makampuni ambayo hamuwezi kueleza fedha za kuyafungua milizikopa benki gani. Serikali imeacha mtajirike bila kuulizwa mlipata wapi fedha nyingi kiasi hicho. Lakini leo mnataka serikali hiyohiyo iwaulize work permit wawekezaji. Ili waondoke mukwibe fedha zaidi ili mneemeshe makampuni yenu na tender za installation mzawadie kampuni zenu.

  Kampuni za hapa duniani huanzishwa kwa kukopa benki. Vodacom tuliyofanyia kazi ilianzishwa kwa kukopa benki. Kwa sababu mnajua kampuni zenu za kisiri hazina msingi mzuri wa uwekezaji, hamkukopa benki kuzianzisha, mnataka tuwalinde kampuni zenu kwa kuzitetea mitandaoni kwamba ni za wazawa hivyo tupige marufuku kampuni za wageni! Acheni ujanja wa kitoto.


  Ok. Tuje kwenye jinsi tunavyochukulia mambo. Wanachotufanyia hawa wazungu na wahindi wa Vodacom na NSN ni kama mfano ninaouelezea ifuatavyo. Mtu anakuja anakushika kwenye paji la uso na wewe unakubali. Huoni kama ni tatizo. Kesho anakuja anakugusa kwenye pua. Maana yake ni nini? Maana yake amesogea chini zaidi ya pale pa jana. Bado huoni kwamba hilo ni tatizo, unaendelea kuchekeleana naye tu. Siku inayofuata anakugusa kwenye mdomo, bado unachekacheka naye kwamba si tatizo, tena wakati mwingine unamshangaa mwenzako anaye-react alipoguswa kwenye uso tu, unamuona si mvumilivu. Wewe umeendelea kumruhusu akuguse na sasa amefikia kukugusa hadi kwenye mdomo. Next time anakugusa kwenye shingo. Bado unaona ni sawa tu.

  Siku zinavyoenda anazidi kuteremka chini zaidi ya mwili wako na next time anakushika kwenye kifua. Achilia mbali kwamba anayeguswa ni mwanamke kwani kwa mawanamke hapa tayari ni mahala pabaya lakini kama ni mwanaume bado unaona hakuna tatizo! Next time anakugusa kwenye tumbo, unachekelea na kusema dawa ni kuishi naye vizuri! Eti dawa ni kumchukulia alivyo!

  Next time anakugusa kwenye kitovu! Mpaka hapo huyu mtu ameshajua wewe ni zezeta atakugusa kokote anakotaka na hutafanya kitu utaishia kuchekacheka, na kama ni kulalamika basi utalalamikia chinichini kimyakimya! Hivyo next time ambayo ni extreme point anateremka zaidi ya kitovuni anakugusa sehemu zako za siri!

  Je, hapo ndipo utasema kwamba amevunja sheria? Je, hapo ndipo utaanza kuandika barua wizarani kwa kutumia jina WAZALENDO na kopi kuieleka kwenye Jamii Forum kwamba jamaa sasa ananigusa hadi sehemu zangu za siri? Kama ulikaa kimya alipokugusa sehemu zote za mwili kwa nini asijione kuwa ana uhuru usiopingika wa kukugusa sehemu zako zote hadi za siri! Ndicho walichofanya hawa Vodacom na NSN kwetu. Wamevunja sheria nyingi na sisi tunakaa kuwachekelea kwa miaka tele.

  Acha tukome na tukienda kampuni zingine tutazingatia umoja na kusimamia ukweli. Kama ni kujinyenyekeza basi tumejinyenyekeza vya kutosha na hiki kinachotutokea ndicho zawadi yetu.

  Kama ni sheria tumewaacha jamaa wamepindisha sheria na ni kama vile tuliwasaidia. Leo hata tukisema wafuate sheria na tukawashinda bado mioyoni mwao watakuwa wanashangilia kwamba wametuvuna vya kutosha. Hakuna tofauti na kumwambia mtu afuate sheria ya kula muwa wakati keshamaliza kutafuna muwa wote na hahitaji tena ganda la muwa ambalo wewe sasa eti ndilo unaliwekea sheria.

  Mitandao haisaidii. Kama mitandao husaidia basi ona jambo hili tulivyolichukulia. Tumeambiwa matayarisho ya kupunguzwa kazini August 29 yaani mwezi mmoja kabla ya retrenchment ambao ni September 30, 2012. Leo ni wiki mbili tangu tuambiwe na bado wiki mbili tupokee batua za kupunguzwa. Hivyo, woga wetu si nafasi kuchukuliwa na wageni kama wanavyotaka wengine dunia ielewe. Kama ni suala la wageni basi NSN na Vodacom zinawageni wengi tangu mwaka 2000 zilipoingia hapa nchini.

  Kumbe, woga wetu ni kupunguzwa kazi kunakoanza September 30, 2012. Lakini tujiulize je, tunastahili kupunguzwa au la. Hili tunalijua sisi wenyewe watu wa nje hawajui na hata wakiongea wanaongea kwa kubahatisha. Kupunguzwa tutapunguzwa tu kwa sababu tunajua financially NSN iko katika hali mbaya.

  Sasa tuje kwenye ukweli halisi wa sisi kutaka kupunguzwa. Nimeanza topic hii kwa kueleza shughuli za NSN kuwa centralized kule India. Wanaoliripoti hili mitandaoni wanataka ionekane kama ni la ghafla na hakuna mtanzania aliyeshirikishwa. Ukweli wote tunaujua lakini tunataka kupiga siasa mitandaoni ili tuhurumiwe na watanzania wenzetu wasiojua tunachojua.

  Mambo yalianzaje? Suala la remote technology kuhamia India halikuzuka ghafla. Watanzania wenzetu tena waliomo humuhumu NSN walifahamishwa jinsi inavyofanya kazi na baadhi wakapelekwa India kuona inafanyaje kazi technology hiyo. Sitaki kutaja majina humu lakini watanzania watatu walipelekwa India kuiona technology hiyo. Wakaridhika nayo itumike ku-monitor network kutokea huko India. Je, wote tujiulize? Ripoti ya hawa watanzania wenzetu iko wapi. Mbona hatukusikia kupingwa kwa jambo hilo wakati ule?

  Kumbuka kwamba kila technology tunayoleta lazima tuifahamishe Vodacom. Management ya Vodacom wakiwemo wazawa wakafunga safari hadi India. Wakaiona technology hiyo, wakaikubali itumike. Mbona hakukuwa na malalamiko.

  Kwa hiyo hili jambo limekuwa approved na watanzania wenzetu walioko Vodacom na NSN na kamwe tusilete porojo za kuwasingizia wazungu au wahindi kwamba wanachukua ajira zetu.

  Najua wanaweza kuja wachangiaji kusema nina wivu kwa niliowataja. Ukweli ni kwamba sijamuona mtu wa kumuonea wivu kwa sababu watu wenye fedha kubwa tumeanza kuwaona tangu tulipoanza kupata akili ya utoto na hawa wengi hawana hata miaka 15 kazini. Ni watoto mno kwa ulinganifu wa maendeleo duniani tunayoyaona kiasi cha kuwaonea wivu. Tunawaandika mitandaoni kwa sababu wameona huko ndiko kimbilio. Wasingeandika wala tusingekuwa na habari na nao na wala nisingejishughulisha na Jamii Forum.

  Najua leo hii post itakuwa gumzo kwenye corridor za Vodacom. Kwa tabia yetu tutaulizana na kupelelezana, kuhisiana kwamba nani aliyeandika hii. Issue si kwamba ni nani kaiandika au kina nani wameshirikiana kuiandika.Issue ni uhalisi wa kilichoandikwa. Hata huyo aliyeandkia hiyo barua kwenda wizarani kuwashitaki foreigners hatumjui na hivyo barua ile haina uhalali wa kuitwa barua ya staff wa NSN. Ni mtu kaandika kaituma mitandaoni basi.

  Tungedumisha umoja uliokuwepo wakati tulivyowaondoa SIEMENS leo hii tungekuwa tunaongea habari ya kwamba technical issues na technical post zote zingeshikwa na wazawa. Siajabu sasa hivi tungekuwa tunanong'ona jinsi ya kuhakikisha au kujenga hoja kwa post ya Managing Director (MD) kuwa mzawa na huenda angeshakuwa mzawa. Lakini hata kwa post hiyo tunakumbuka mzawa aliishika kwa muda. Ni yule Idrissa Rashid aliyetoka BOT akaenda TANESCO.

  Fundisho ambalo baadhi ya wachangaiaji wameshalieleza ni kwamba watanzania msidhani kwamba mtakomboka kwa kujitosa mmojammoja kufanya usaliti halafu ukajenga majumba Mbezi Beach au Tegeta na kuanzisha kampuni za installations. Wazungu wanatugawa hivyo wakijua mwisho wa siku hata hao wanaojipendekeza kwao wanapigwa chini na hakuna wa kuwatetea.

  Hebu leta wazo kwamba tunataka kuanzisha move ili MD wa Vodacom awe mzawa na technical director awe mzawa. Hutaungwa mkono hata kidogo na hata mimi sintaunga mkono kwa sababu aliyeumwa na nyoka akiona unyusi anashituka. Kwanza hata atakayeropoka wazo hili ni ishara kwamba ameshajitenga kabisa na wazawa wenzake hajui tunawaza nini.

  Staff tulioko mazingira ya Vodacom tukipewa kupiga kura ili MD wa Vodacom awe mzawa basi watanzania msishangae staff wengi tukaamua kupiga kura ya HAPANA. Tutapiga wazungu waendelee kututawala hapa Vodacom kuliko kutawaliwa na hawa wabongo wenzetu. Ingekuwa hatujawahi kuwapa cheo kama cha ME au HOD kama tulivyowapa basi tungejikuta kweli tunapiga kura kuwapa wawe ma-MD.

  Lakini baada ya kuwaona watanzania wenzetu wakipewa vyeo vya ME (U-director wa Dept.) na cheo cha HOD basi tumesema imetosha na hatutaki kusikia au kudanganywa kwamba kuna wazo la mbongo anafaa kuwa MD wa Vodacom. Ninaweza kuwa au tunaweza kuwa tunakosea kusema hivi, lakini wabongo wenzetu hawa wametufikisha tuwaze hivi.

  Ndiyo maana humu ndani ya NSN au Vodacom tumeparaganyika na hatutaki tena kusikia move au mkakati wowote wa kudai msalahi yetu kama wazawa au vyovyote. Unafiki umejaa kupita maelezo. Ndiyo maana hata hiyo barua iliyopelekwa wizarani kuwashitaki foreigners walioiandika walijua wazi wakitushirikisha wengine itapingwa kwamba ni unafiki. Ni kweli ingekosa kuungwa mkono na ndiyo maana walioiandika wameona nji ya mkato ni kutafuta kuungwa mkono kwenye mitandao kama ya Jamii Forum ambako hawajui kinachoendelea humu ndani ya NSN na Vodacom.
  Asanteni.

   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Hizo abbreviation zinasumbua ku-connect dots.

  Pamoja na kasoro hiyo, umejieleza vizuri sana.
   
 3. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Poleni ila wingi wa wageni hata katika mabenki pia ni dhahiri shahiri kua ni kizazaa, Kuna Benki1 iko hapa JM Mall ni ya Kikenya na wakuu wa idara muhimu wote ni kutoka Kenya. Wanampenda mfanyakazi muoga na mnyonge asietaka kuhoji haja malipo yake mwenyewe. HR ni mhindi ila ana certificate ya usecretary, Head wa Credit ni Mkenya na ana Diploma tu na walioko chini yake wana hadi Masters.
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  NSN NA VODA ni kitu kimoja? Maana unaongelea kama ni wamoja, hebu nifafanulie kwanza
   
 5. mchambuzixx

  mchambuzixx JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 1,294
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  sio voda tuu hata makampuni mengine ni kheri atawale mzungu kuliko mtanzania mwenzetu katka hiz kampuni coz watanzania wana roho ya kwanini roho mbaya
   
 6. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Vodacom, KAZI NI KWAKO!!!

  Nyie mwala, sie twaliwa.
   
 7. s

  sindo Senior Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  umeeleza vizuri sana
   
 8. s

  sindo Senior Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kwetu ni Majungu na kukwazana, kila apatae cheo anafikiria mujijenga, itakuwa ngumu kujali maslahi ya wengine hata kidogo
   
 9. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,325
  Likes Received: 2,320
  Trophy Points: 280
  Nimeisoma yoote na sijabakiza kitu.........Ndio maana hata kwenye Siasa kuna wanafiki chungu nzima. Nafikri ni Tanzaniaville hii
   
 10. s

  sindo Senior Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 135
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Big UP sana tu muwasilishaji maanaumeeleza kila kitu bila kuficha huwenda wengine hapo ndani hawakuyajua hayo naamini sio wote waliitwa kwenye mkutano
   
 11. Radhia Sweety

  Radhia Sweety JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 4,448
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Ungefupisha maelezo yako. Si kila mtu ni mpenzi wa kusoma maelezo mareeeeeefu yasiyokuwa na umuhimu kwake.
   
 12. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Daah!
  Poleni bwana,ila msichoke kuendelea ku fight.
   
 13. morphine

  morphine JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 2,566
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  umesikika mdau
   
 14. Silly

  Silly JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 508
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  mkuu, umeanza kwa nguvu zote..ila point is made, wazawa tuna matatizo yetu na sio Voda/NSN tu bali ni kila sekta utakokwenda ametoka mdhungu kaja mzawa, ni koloni mamboleo..tutafika tu..
   
 15. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,641
  Likes Received: 2,065
  Trophy Points: 280
  Kazi kwelikweli, tunahitaji kubadilika watz maana ukiona watu wanapenda kuwa chini ya wazungu badala ya wazalendo hapo ujue pana kazi, hii yote ni kwa sababu ya ubinafsi mtu alikipata anakaba kila sehemu wakati motisha kwenye kazi inasaidia kuleta mori wa kazi lakini badala yake wazalendo wanachongeana kwa wazungu
   
 16. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Story nzuri ila ni ndefu kwa wavizu wa kusoma, kama kuna mtu anaweza summarise tutashukuru
   
 17. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #17
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,600
  Likes Received: 1,676
  Trophy Points: 280
  Inaelekea sio kitu kimoja, NSN wamepewa tenda ya kumonitor na kusimamaia MITAMBO ya VODA, Kifupi VODA wame OUTSOURCE shughuli yote ya MITAMBO kwa NSN.
   
 18. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,351
  Likes Received: 2,693
  Trophy Points: 280
  Ukitaka kumficha jambo mbongo muwekee kwenye maandishi kama hivyo...
  Zaidi hayo mkuu mleta huu uzi nadhani idea ya kupunguza wafanyakazi kwa NSN haijaanzia Bongo...Last year kwenye mwezi Novemba nilisoma article moja kwamba NSN itapunguza wafanyakazi wake katika ofisi zake zote.
   
 19. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #19
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  Kulikua na haja ya ku_reply maelezo yote hayo? Tumia kichwa kufikiri na si kufugia nywele tu.
   
 20. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #20
  Sep 17, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,407
  Trophy Points: 280
  ┬ĽManaged Service aka Outsourcing
  Lakini wakifanya retrenchment si mtalipwa hela? Mbona mwanzo wakati mnatoka voda kwenda nsn mlilipwa mishaara mi5? Msiogope nsn maisha sio voda tu,huyo tajiri aliyeacha kazi voda akaanzisha kampuni si ndio huyo mwenye MAKTECH?
  ┬Ľnaungana na wewe bora watawale wazungu maana wabongo wakipewa nafasi yani ni manyanyaso tu,ufitini ubabaishaji tu,kuna wengine wanafanya juu chini wakufukuze kazi alete ndugu yake! Full **** bora wazungu waendelee kuwa Directors,HOD,Snr Managers,CEOs etc
   
Loading...