Ushauri wenu kwa huyu binti

dimaa

JF-Expert Member
Jul 30, 2016
3,043
2,000
Habari zenu wake kwa waume,
Ni binti mmoja ivi ambaye tulikutana naye hapa DSM, tulikutana naye 2012, kipindi alikuwa akisoma shule ya kunduchi girls, likizo alikuwa akija kwa ndugu zake ambapo ndo karibu na home.

Kiukweli alikuwa yuko njema sana, mimi mwenyewe alinivutia sana, lakini kutona na hofu ya mungu sikumwambia kuhusu upendo wangu kwake na yeye vilevile alikuwa ni mtu wa dini sana kwa hiyo isingekuwa rahisi kumuasi mungu

Baada ya hapo tukapoteana kabisa, yeye akaenda chuo flani ivi iringa na mimi Moro, yeye ni kabila tofauti na mimi. Yeye kwa sasa yupo kwao mkoani. Kutokana na kipoteana mda mrefu nikaomba namba yake kwa ndugu zake wakanipatia nikamcall nikamwambia Mimi flani akanielewa, nikamwambia mbona umeadimika ivi?,

Akanambia likizi alikuwa anakuja, na alikuwa akifika hadi home na kuniuliza wakamwambia bado sijafunga chuo , ama likizo nimeenda kwa ndugu kusalimia. Akambia yeye kuna mwanafunzi wa huko kwao jirani yao aliwahi muulizia flani unamfahamu (yaani Mimi), akamwambia hapana.

Sasa ikatokea nikamuuliza vipi ushaolewa akasema hapana, nikamwambia nataka nikuoe akaguna , akasema ngoja afikirie. Nikawa namtafuta mimi tu , nikachoka nikampotezea na mimi. Akarudi kwa spidi mbaya mno. Sasa baada ya vile vitimbi vyake moyo wangu ukaghairi tena kumuoa.

Mara ya kwanza aliniuliza utanioa lini nikamwambia uwezekanao wa kukuoa ni mdogo sana, alilia sana. Jana tena kanipigia simu kanambia anatamani sana kuwa kwake hivyo basi nimuoe, nikamwambia uwezekano wa kukuoa ni 10%, kalia sana, kanambia anavyonipenda kama sitomuoa hatotaka tena kuolewa na mwanamme yoyote au atakaa zaidi ya miaka 3, ndo afikirie kuolewa tena.

Nishamwambia ukweli kuhusu mimi lakini bado tu hanielewi ,
Nitumie mbinu gani ili anielewe labda wakuu?
Manake ananikanganya kwelikweli.
Karibuni,


By
Dimaa.
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
43,844
2,000
Pole sana mkuu...Lakini si ameshasema hataolewa tena usipomuoa wewe..kata nae mawasiliano labda
 

Mkwawe

JF-Expert Member
Jun 10, 2016
1,935
2,000
Hapa kwa simulizi hii ndo nimeamini kwamba wasichana hawajui wanachokitaka
Ila nakushauri mpe nafasi na umchunguze kwa muda mrefu mienendo yake kama inakuridhisha
zaidi na zaidi moyo wako ndo unajua
usimkatae kwa kuwa mwanzo hakukubalia ila jipime kama unampenda kweli
[HASHTAG]#HappyAnniversaryToMeInJF[/HASHTAG]
 

Bandido-2

JF-Expert Member
Jan 12, 2013
263
1,000
umeandika mambo mengi ambayo sio ya Msingi...

sasa kama umeshamwambia humuoi sisi tushauri nn sasa??

kwanza hiyo 10% yann..?? ww mwambie kabisa humuoi na hakuna uwezekano wa kumuoa.. akikuganda nenda kwa mganga
 

muhomakilo jr

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
11,338
2,000
Yan hapo ndo ulitongoza hivyo? Ndo maana mnashea wake!
Si mpaka ajue kutongoza, haya maisha ya form 4 na form 6 ni umri wa kujifunza vitu vingi sana,kama hapo ulikuwa mzembe flani wanawake watakusumbua tu, eti jitu linafikia kujitoa uhai kisa, mwanamke kamkataa
 

nosspass

JF-Expert Member
Mar 7, 2013
5,187
2,000
utakuwa mvulana wewe........uliyosimulia hapa yote na ya kivulanana sio kiume-----MWANAUME.
 

South

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
3,494
2,000
Sababu iliyofanya utake kumuoa na iliyokufanya ukaghairi ni zipi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom