Ushauri: Watoto wametugombanisha

hiram

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2013
Posts
267
Reaction score
394
Habari wanajamvi,

Aisee ugomvi wa watoto siyo wa kuingilia, kuna siku mwanangu Rizuge wa miaka minne alikuja kunishtakia kuwa amepigwa na mwenziwe Pizaulo ambaye umri unakaribiana. Mimi kwa hasira na uchungu wa mwana nikaenda kumzaba kibao yule mtoto wa jirani aliyempiga mwanangu.

Baba yake Pizaulo hakukubali na ikapelekea ugomvi mkubwa sana kati yetu sisi watu wazima, cha ajabu jana nimemkuta mwanagu Rizuge na mwenziwe Pizaulo (yule mtoto aliyempiga) wakicheza pamoja, yaani wakati sisi wakubwa hatuongei lakini wao washapatana wanacheza.

Je, sisi wakubwa tuendelee kuchuniana?
 
Rizuge vs Pizaulo, kama walipatana wenyewe kwa ridhaa na dhati ya mioyo yao pasipo kushurutishwa hakuna hakuna haja ya wewe third part kuendeleza chuki. Narudia Rizuge vs Pizaulo

Sent using Jamii Forums mobile app
 


WEWE NI WA KUFUNGA KABISA, UNAPIGAJE KIBAO MTOTO ASIYE KUWA WAKO? HUYO MTOTO ANGEKUWA WANGU MIMI WALA NISINGEKUFANYA KITU, NI KITUONI TU .. NA UNGEINGIA KWENYE SHIDA, MIMI SIWEZI PIGA MTOTO ASIYE KUWA WANGU, WATOTO WANA MAMBO YAO MENGI SANA .....
 
kwakuwa mtoto Pizaulo ni mkubwa sasa na anaelewa nini maana ya msamaha ukizingatia alishakuwaga muhuviri aombe radhi kitu kidogo tu
 
Inabidi tuwapeleke tanga tukawapatanishe... Mnazidiwa uwezo na watoto... Hahahaaaaaaaaa
 
WEWE NI WA KUFUNGA KABISA, UNAPIGAJE KIBAO MTOTO ASIYE KUWA WAKO? HUYO MTOTO ANGEKUWA WANGU MIMI WALA NISINGEKUFANYA KITU, NI KITUONI TU .. NA UNGEINGIA KWENYE SHIDA, MIMI SIWEZI PIGA MTOTO ASIYE KUWA WANGU, WATOTO WANA MAMBO YAO MENGI SANA .....
read between the lines.
 
Ugomvi wa watoto si wakuingilia...kinachotakiwa ni kuwakanya tu wasigombane ni dhambi...hahaha
Ila nikwambie..RIZAUGE hajapatana na PIZAULO kwa kupenda...basi tu wanafurahisha genge....RIZAUGE is not happy at all mpake aombwe msamaha kutoka moyoni
 
Watoto wanapigana ndani ya dk moja wanapatana wanaendelea

kucheza

tatizo wazazi wa siku hizi nao ni watoto hawana hekima wala busara
 
read between the lines.

Nimesoma, sio kuchuniana tu, ningehama hata hapo, siwezi kaa na mtu anayemwazibu mtoto wangu kijinga hivyo kwa ajili hiyo. Yani wewe umetumia judgement ya mtoto kuchukua action, ina maana Baba yake naye alipoenda mwambia angekuwa mtu mwenye tabia yako angekuja kukupiga wewe au mke wako? just imagine....
 
Ugomvi wa watoto si wakuingilia...kinachotakiwa ni kuwakanya tu wasigombane ni dhambi...hahaha
Ila nikwambie..RIZAUGE hajapatana na PIZAULO kwa kupenda...basi tu wanafurahisha genge....RIZAUGE is not happy at all mpake aombwe msamaha kutoka moyoni

Hata watoto wangu wawili huwa wanagombana, sasa unampiga yupi? this is so wrong .... ni WATOTO anyways.
 
ugomvi wa watoto si wa. kuingilia....hawakawiagi kupatana..
siku nyingine ukiona watoto wanagombana shika jembe ukalime.
tatizo babake pizaulo ni mtemi hajamfundisha mwanae tabia njema ye akikosea hajuagi kuomba radhi.

nakushauri ukikutana na hako katoto kwenye kona kazabue bonge la bao ila akikusemelea mi simo
 
Yaani watoto wamewazidi busara nyie watu wazima?
Ruksa Ku copy toka kwao.

Sent from my Compaq desktop-1997 Using Jamiiforums desktop app
 
kesi kama hizo siku nyingine usikurupuke na vibao
kipimo cha mkojo kilikuwa kinahusika hapo kwa pizaulo au ruzauge
 
At least umelijua hilo,mjifunze na msirudie makosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…