Ushauri: Watoto wa Bosi wawatia mimba watoto wa 2 wa mdogo wangu wa kike

UMASIKINI BWANA

JF-Expert Member
Oct 17, 2013
942
566
Habari zenu wana great thintkers,

Mdogo wangu anataka ushauri kwenu.

Yeye kaajiriwa kama mpaliliaji katika shamba la ekari 103 la miti pamoja na wenzie wengi.Tatizo watoto wa bosi ambao ni wasimamizi wa shamba wanawarubuni watoto wa kike wa mdogo wangu wanaosoma na wawili wameshatiwa mimba na kuwatelekeza, inaniuma lakini mdogo wangu anashindwa kusema kwakuwa kibarua kitaota nyasi.

Afanyeje?
 
Hakuna kazi nyingine? Mdogo wako ajifunze kuwa maskini jeuri hata kufa na njaa.
 
Mdogo wako akikomaa hata huo umasikini utamtoka na Kuacha kupalilia shamba la Mzazi mwenzie maana tayari ameshakua mkwe wa watoto wa boss inachotakiwa ajiongeze tu kupambanania haki za wanawe
 
Sasa anaogopa halafu atawezaje kusidia kulea hao wajukuu? Ni bora atafute kuda mzuri aombe kuongea na bosi wake na mkewe na kuwaeleza kilichotokea bila kukasirika wala kuwatishia kitu na kuomba msaada wao ikiwezekana. Nina uhakika tabia waliyofanya watoto wake ataweza kuwasaidia hao mabinti hata kwenda hospitali, ila waende wao ili asiende kuwatoa mimba hizo na kuwaharibu milele..ili hasipate mwanya wakupanga na daktari.

Nachofikiri ni Mzee huyo ataweza kuwa mtu mzuri na kutaka kuwasaidia hata kuwaondoa walipo na kuwaongeza kizaidi. Kuna kitu siku hizi wazee hawatupi wajukuu. Asali sana, na wataweza kuhudumiwa na baadae kuendelea na masomo yao.

Mengine inategemea huyo bosi yukoje, je ni mtu mkali au wa dharau asiogope, mtoto au mjukuu wanabafili tabia za watu.

Poleni na hilo, kiaina inasikitisha ila labda ndio wajukuu anaopewa ndugu yako.

Akiona wamekuwa wakali sana akiongea mao au kuwatishia basi aende haraka ustawi wa jamii, ili wawee kuwasimamia kwa lolote lile.
 
Back
Top Bottom