Siku za hivi karibuni tumeshuhudia hali isiyokuwa ya kawaida kwa Mbunge Zitto Kabwe. Amekuwa akiibuka na hoja za hapa na pale dhidi ya serikali ambazo mwisho wa siku vyombo mbalimbali vya serikali vimekuwa vikizikanusha kuwa hazina ukweli wowote bali ni uzushi tu unaolenga kuichafua serikali. Hata hivyo ZZK amekuwa akionesha hali kama ya kutaka “kutunishiana misuli” na serikali.
Kwa upande mwingine ZZK ni Kiongozi wa ngazi ya juu kabisa ndani ya chama cha ACT-Wazalendo. Tumeona chama hicho kikimeguka vipande vipande baada ya viongozi waandamizi ndani ya chama kukihama chama hicho, na wengine wakijiuzulu nafasi zao za uongozi kutokana sababu mbalimbali.
Katika hali hii ZZK hawezi kuwa salama kabisa kisakolojia, ni lazima tu atakuwa na muweweseko. Ni lazima tu atakuwa anamtafuta mchawi nje ya chama chake, bila kujitathmini ndani kwanza. Ni lazima ataibuka na hoja zinazovuta hisia za watu hata kama hazina ukweli ili mradi tu kukifanya chama hicho kiendelee kusikika masikioni mwa watu, licha ya kwamba kinaonekana kabisa kwamba kina-undogo “natural death”.
Hivyo ushauri wangu kwa Rais JPM ni kwamba ampotezee kabisa ZZK kwa hoja zake za uzushi, kwani kama ataonekana kubishana naye, ataendelea kumpa “kiki” na hivyo kumpa umaarufu asiostahili. Aidha, kwa kuwa ZZK anaoneka kabisa kwamba anataka ku-intensify mgogoro na serikali, kuna uwezekano mkubwa akawa anajiadaa kwa movie moja matata. ZZK anaweza kuwa anajiandaa kwa movie ya “kujiteka” ili mwisho wa siku watu waseme kwamba, kwa sababu ZZK alikuwa na mgogoro na serikali basi serikali inahusika na utekaji huo; na pindi arudipo uraiani atakuwa ashapata kiki za kutosha zitakazo mwongezea “political mileage” lakini pia akiwa ameichafua serikali. Ni wakati wake Rais JPM kuwajibu watu wa aina ya ZZK kwa vitendo katika kufanya mambo makubwa yanayogusa maisha ya Watanzania wengi, kwani watu wote wenye nia njema na nchi yetu, hawawezi kubeza juhudi zake za kutaka kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wote.
Benmpo