Ushauri wangu kwa Sumaye na Lowassa

nkisumuno

JF-Expert Member
May 22, 2012
208
72
Kwa pamoja naomba niwashauri yafuatayo:

Kwa kuwa wote mmewahi kuwa viongozi wa juu ndani ya CCM nawashauri bakini kwenye siasa lakini suala la kugombea Urais acheni, kwanza mmelitumikia Taifa kwa kadri mlivyoweza,mmetenda mema na mapungufu mengi kama wanadamu. Tanzania ina watu wengi wenye sifa waacheni nao waonyeshe uwezo wao.

Sumaye, umekuwa kiongozi kwa muda wa miaka 10,mmefanya mambo makubwa pamoja na mambo makubwa kuna mapungufu mengi ikiwa ni pamoja kuuza nyumba za serikali,kubinafisisha viwanda vyetu na mengine mengi wewe ukiwa waziri mkuu leo hii pamoja na mapungufu hayo ambayo yameleta usumbufu mkubwa kwa Taifa hivi leo unataka leo ugombee urais? Nakushauri kaa pembeni ukishauri serikali bila kujali itikadi ya chama.

Lowassa, Umekaa katika uongozi kwa muda mrefu umefanya mengi mazuri hasa ulipokuwa waziri wa ardhi. Ulipokuwa waziri mkuu ulifanya mengi mazuri kwa kuwa mfuatiliaji mzuri lakini kuna mambo mengi ambayo leo hii yamo mioyoni mwa watu kwa kuingiza Taifa pabaya hasa mkataba wa Richmond, mara ukataka mvua za kutengeneza. Hiv husikilizi hotuba za Nyerere kuwa anayependa sana kwenda ikulu hatufai? Pumzika waachie watu wengine wewe umefanya inatosha tuwape nafasi na wengine.

Mwisho, mkumbuke watanzania si wale wa kununuliwa na kofia na vitenge.

Kwa wale ambao bado wanamtazamo finyu ule ule nawaasa waache kusafisha watu waliochafuka.
 
F.Sumaye ni wazir mkuu pekee aliyekaa madarakan kuliko wote tz!Ni sifa kubwa sn na heshima kubwa kwake,yanini kuingia kwenye malumbano yote hayo ya urais?Awe mshahur tu inatosha!
 
Haya mapambano (aka ushauri) hakika yana mashiko tatizo ni moja tu! Ni sehemu ya mapambano ya makundi pinzani ya wasanii (membe group)Vs Mafisadi (Lowasa group) na Zilipendwa ( Six group)! Ni vema kwamba nkisumuno amekuwa wazi kwamba yeye ni Wasanii group (Kibaraka wa Membe group)! Keep it up if you are sure with the results! :hatari:
 
fisadi lowasa ndiye ataiua kabsaa ccm, mwenzie jk keshaichimba kaburi yeye anakuja kuizika. M4C 4rever
 
Sumaye anataka urais kwasababu jk aliichukua ngurudoto na kuifanya iwe ya wanamtandao, lowasa anataka urais kwa matakwa ya rostam, ndio maana membe akasema maadui zake watakimbia nchi 2015 kwani m4c lazima kieleweke, viva chadema
 
Wote wanapoteza muda wao tu. Mbinu walizotumia mafisadi kumng'oa Sita kwenye uspika ndio hizo hizo zitakazotumika kumng'oa Lowasa, sita na Membe. Watasema ni zamu ya mwanamke sasa. Hili likishindikana watasema ni zamu ya Zanzibar sasa. Wazanzibar watasema tumewaachia Bara miaka 20 ya kuongoza nchi sasa ni zamu yetu. Hili halipo katika katiba ya CCM LAKINI lina mantiki. Wazanzibar wakikomaa na hili fujo za Lowasa, membe na sita zitaishia hapo.Nani atalalamika hapo? Sita hatalalamika kwani yeye urais haumnyimi usingizi anachojaribu kufanya ni kupambana kuhakikisha fisadi haingii ikulu. Lakini pia wote wanaweza kuridhika japo kwa viwango tofauti kwa wao wote kukosa nafasi hiyo. Hili linaweza kusaidia kuwa na kamshikamano kadogo na kuifanya CCM isogeze kidogo siku zake za kuishi
 
Ushausi wako huo wa kipumbavu mpe membe,salma,sita na nape,..membe walai watanzania atakuwa dhaifu kuliko hata huyu mbayuwayu,me i thnk mjadala wa urais uwe kati ya dr.slaa au lowasa,.
 
Back
Top Bottom