Ushauri wangu kwa Ndanda FC

Ushauri wangu kwa Ndanda FC

burungutu

Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
66
Reaction score
10
Ndugu wanajamvi,
Sisi watu wa mikoa ya kusini na majirani zetu tulifurahi sana baada ya kuona timu yetu ya mpira ndanda FC ikitutoa kimasomaso kwenye ligi za soka hapa nchini, matatizo madogo tu yaliyojitokeza wamemfukuza kocha, sasa tunatoa ushauri kuwa kumfukuza kocha alieitoa timu kimasomaso kwa michezo ya awali siyo sahihi, wangevuta subira kwa michezo mingine ijayo na kwa sasa wakae nae chini wayamalize matatizo yao ili timu iendelee kutoa burudani kwa watanzania , pia timu wasiihusishe na sherehe za kisiasa kwani hilo hawalioni wanaona kocha tu ndie anamatatizo.
 
Dah kweli kiongozi mwanzo huwa mgumu na ss tupo nyuma kuwapa support
 
haya bana sie watu wa kanda ya ziwa hususan mkoa wa mwanza tuaisubiria kuipokea timu yetu ya TOTO AFRIKA ligi kuu ya msimu ujao
 
Nakuambia wamakonde,wamakua,wamwera etc hawana uvumilivu kabisa.mashabiki walikuwa na mategemeo makuuuubwaa juu ya timu yao,hivi sasa kila mtu huku kusini wanaiongelea vibaya hii timu.Juzi si umesikia wamepigwa mawe hao wachezaji wa Ndanda?kiufupi timu itarudi itakapotoka na hawa wakusini ndio wataendelea kuikosa burudani ya soka hapa Tanzania
 
Wabunge wawili wenye nguvu ya kipesa na kisiasa ndio chanzo cha timu ya Ndanda kufanya vibaya, sitaki uniulize kwann nasema hivo....
 
Back
Top Bottom