Ushauri wangu kwa maendeleo ya taifa langu

Obrigador

New Member
Sep 13, 2021
2
2
Amani iwe nanyi wakuu!

Bila kupoteza muda, ningependa kuipongeza na kuishauri serikali yangu ya jumuhuri ya muungano wa Tanzania katika swala la kupigania na kuwarudisha shule wanafunzi wa jinsia (ke) walio shidwa kuendelea na mfumo wa elimu rasmi kutokana na changamoto mbali mbali walizo kutananazo.

Ushauri wangu
1. Hawa mabinti wafundishwe au kupewa elimu ya ufundi na stadi za maisha, na sio warudishwe tena kwenye masomo ya kawaida kama physics na history kutaja kwa uchache, kwani mwisho wa siku watarudi mitaani na kutafuta ajira kama ilivyo kwa wanafunzi wa mifumo rasmi. Na kwa sasa kama inchi tunachangamoto katika mfumo wa elimu na soko la ajira.

2. Eneo sahihi, hawa mabinti wanatakiwa wakaandikishe katika vituo mbali mbali vya veta nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kutenda na kufanya kwa mifano na sio kusoma kwa nadharia tena, kwa sababu wengi wao muda umeshawatupa mkono na lengo liwe kuwajengea uwezo wa kuyakabili maisha practical nasio kuwakaririsha tena, what is Geography.

3. Serikali iandae na kutoa mafunzo maalumu kwa wakufunzi au waalimu watakao toa au kuwezesha mpango wa kutoa elimu kwa hawa mabinti na sio kama inavyofanyika sasa. Mafunzo yajumuishe stadi za kufundisha na namna ya kufundisha wanafunzi hawa ikiwemo kujua na kutambua saikologia vizuri kwani wengi wa hawa wanafunzi walishakata tamaa ya maisha na wengine bado wanatoka mazingira magumu mno.

4. Kushirikisha wanafunzi hawa na kufahamu wanataka kujifunza nini, sio kila mwanafunzi anapenda kufundishwa types of Geography, au branches of science, wengine wanapendelea kujifunza physical activities kama shughuli za ujasiriamali n.k. hvyo mjadala wa pamoja utawezesha kufundisha kile anachokipenda mwanafunzi na atakisoma kwa moyo mmoja kwa kuwa ameshiriki katika kufanya maamuzi ya atakachofundishwa.

5. Tusiwakatishe tamaa hawa mabinti tuwaache watimize ndoto zao, haijalishi changamoto wanazopitia, tuwape moyo, tujenge saikolojia zao na kuwapa uhuru wa kutenda kadiri inavyofaa kwa lengo la kutimiza ndoto zao na za serikali kwa pamoja. Pia nipongeze jitiada za serikali katika hili.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom