Ushauri wakuu najihisi upweke

Kapepo

JF-Expert Member
Aug 14, 2015
1,063
1,188
Mimi ni muhitimu wa chuo kikuu age 26 kwa kifupi nina maisha mabaya mno especially kwenye saikolojia kwan nimekuwa nikisumbuliwa sana na msongo wa mawazo, napiga sana punyeto ntajitahid kuacha , nimekuwa muoga sana kwan hali yangu ya kiafya imekufa sio nzuri sana nimekuwa nikisumbuliwa sana na uchovu uliokithiri, maumivu kwa mbali kwenye joints Kuna muda hunitoka vijipele vidogo vyekundu mwilini nakuwa naogopa mno nimeenda hospital mara nyingi sana kuangalia kama nina presha lakin sikuwah kuwa nayo,

Kuna kipindi mwili uankosa nguvu kabisa nimekuwa muoga kwa kufikiria Magonjwa makubwa mno nimejawa na hofu kubwa mwilini kwan kila kinachotokea mwilini kwangu kimenifanya nitengeze hofu hii haya yote yalitokea baada ya kuwa na mahusiano na Dada mmoja ambaye anadai ni muathirika lkn kwa sasa tumeachana nimejaribu kucheki afya maranyingi mno lakin sina mambukizi .

Je ndugu zangu nini tatizo naombeni USHAURI kuondokana na hii hari. Kwa sasa baadhi ya vidole vyang vya mkono vimekuwa kama vinavibrate kwa muda pamoja na macho.
 
Hobi yako ni ipi/zipi? Kama unaamini uwepo wa MUNGU, hudhuria ibada. Kuna amani ya pekee kule, amani ipitayo ile ya ulimwengu
 
Pole sana ndugu!! Naona hal inayokusumbua hapo n msongo wa mawazo unaosababishwa na upweke pia woga kuhusu ugonjwa alokua nao mpenz wako!

Usijali! Cha msingi hapo jitahid kujichanganya na watu wa rika tofauti tofauti na ujarib kuwaeleza tatizo lako

Sometimes kueleza tatzo kwa watu n kama unaondoa mzigo fulan kichwani!

Ukiona bado hali inaendelea jarib kwwnda kwa wanasaikologia watakusaidia mkuu


NB; Hlo tatzo la kutetemeka lnaonekana kama limetokana na ADDICTION ya kitu fulan! (Pombe,madawa, Punyeto) Jaribu kukiacha
 
Pole mkuu, usiwe mtu wa kukaa pekeako, jichanganye na watu ili upate ideas mpya,hudhuria ibada kama unaswali au unasali neno La Mungu/Allah ni dawa, utakua okey
 
Mkuu, pole sana.

Punyeto haikufanyi wewe kuwa hivyo, kitu pekee kinachokusmbua ni hali ya kuachana na huyo mpenzi wako sababu ulimpenda sana na ulikuwa karibu nae kila wakati ila sasa upo peke yako na kibaya zaidi ni hizo ugonjwa ambao unamsumbua huyo dada.
Mkuu, unahitaji kuwa na amani, hata mimi nikigubikwa na stress nyingi huwa napata homa, yaani kikitokea kitu kinakaniumiza moyoni hata dakika 10 hazifiki tayari nasikia kuumwa ndani mwangu.

USHAURI
1. Jichanganye na watu, mfano katika mazoezi, vijiwe vya chipsi, dukani n.k
2. Kaa karibu na watu wa imani yako.
3. Kuanzia sasa ishi na watu ambao watakupa majibu ambayo unafahamu hayatakuumiza moyo wako bali watakutia moyo, kukutia kwako moyo ndipo kutasaidia kurejea kwa kwa furaha mapema ndani mwako.
4. Jitahidi saaaana kula vizuri, yaani kula ushibe haswa.

Pole sana na nakutakia kila la heri.
 
Back
Top Bottom