Kuna uwezekana wa mambo mawili hapo; la kwanza huyo Dada ana busara na tayari ana mtu wake hivyo hataki kuwachanganya au kukupotezea muda, kama ni hivyo, ana busara na ni mke mzuri mtarajiwa, maana mwingine angekukubalia ili afaidi Boom lako. Jambo la pili, anaweza kuwa anataka kukusoma kama kweli una nia ya dhati. Kwa hili la pili utahitajika kuwa mvumilivu na kuendelea kubisha hodi kwa muda mrefu ili kujiridhisha bila mashaka kwamba ni kweli hutakiwi. Lakini angalia usiwe kero kwake, huku kwa nchi za wenzetu kama mtu hakutaki akaendelea kumlazimisha ni kosa kisheria; na vile vile ukumbuke kilichokupeleka chuo....Elimu Kwanza.