Nyalotsi
JF-Expert Member
- Jul 20, 2011
- 6,989
- 5,069
Nilikuwa na mchumba ambaye nilimtambulisha hata kwa ndugu zangu(dada). Lakini baadaye alikuja kunigeuka bila kunieleza sababu ya kufanya hivyo. Alinitumia tu msg kunitaarifu kwamba anaolewa na mtu mwingine baada ya muda mrefu wa kukaa kimya bila mawasiliano kwani alikuwa mbali nami. Iliniumiza sana kwani nilimpenda na sikutegemea kufanyiwa hivyo na yeye. Huyo ni wa pili baada ya wa kwanza kuniambia nina muda mrefu na shule hivyo hawezi kunisubiri. Imepita kama miaka saba kati ya hivi visa viwili na kati niliwahi kuwa na mtu mwingine ila niliachana naye baada ya kutofautiana msimamo. Toka huyo dada wa tukio la karibuni kunifanyia hivyo nimejikuta nakuwa tofauti na nilivyokuwa mwanzo kwani nimepoteza kabisa interest na wanawake na hata kufikia kuwatukana ovyo. Hata wale niliozoeana nao kabla siku hizi wananiogopa hata kunitania. Yaani nimekuwa mtu ambaye kila mtu ananishangaa. Hali imekuwa mbaya zaidi kwani hata dada zangu natofautiana nao kauli bila sababu na kuanza kuwafokea. Wengine wameanza kukesha kwenye maombi kuniombea. Nimejitahidi kupambana na hii hali lakini dah, hali ngumu na siipendi kwa kweli. Naombeni ushauri nifanyaje ili nirudi kawaida?