Hii hali ya wabunge wa CHADEMA kutumia muda wao mwingi kwenye majukwaa badala ya kuwawakilisha wananchi bungeni ina sikitisha mno.
Ifike wakati sasa wabunge wa CHADEMA wachague moja, kama ni bunge au majukwaa, kwani huwezi kutumikia vyote hivi kwa wakati mmoja.
Hivi sasa bunge la bajeti linaendelea, bunge hili linahitaji umakini na ufanisi wa wabunge ili michango ya wabunge iwe yenye tija na kujenga wanapo ishauri serikali.
Lakini cha kusikitisha wabunge wa CHADEMA wamekuwa 'bize' kwenye majukwaa, hii ina pelekea wabunge wa CHADEMA kukurupuka kuandaa hotuba mbovu na kusababisha gumzo mara kwa mara pindi wanapo ziwasilisha bungeni hotuba zao.
Hivi sasa wabunge wengi wa CHADEMA wamejikita kutetea wagombea udiwani walio wasimamisha kwenye kata zenye uchaguzi mdogo wa udiwani. Mfano Tundu Lissu yuko Morogoro, Godbless Lema yuko Arusha n.k
Nitoe rai kwa CHADEMA, ni wakati sasa chama chenu kikomae, inapaswa chama kiwaache wabunge watekeleze majukumu yao ya msingi pindi bunge linapo kuwa hai, na chama kiunde kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kampeni, hasa za chaguzi ndogo.
Mbunge wa iramba magharibi mwigulu Nchemba kupitia ccm yuko Arusha akikinadi chama chake kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mdogo, pia yupo na mbunge wa viti maalumu wa ccm mh. DEVOTHA LIKOKOLA.
Lema yupo Arusha,kwani ni mbunge wa jimbo gani?
Kwa uelewa wako mbunge anawatetea wananchi wake akiwa bungeni tu? Wewe nadhani ukanywe uji ukalale. Mwigulu anapozunguka mikoa kadhaa anawateteaje wana Iramba Magharibi?
Hii hali ya wabunge wa CHADEMA kutumia muda wao mwingi kwenye majukwaa badala ya kuwawakilisha wananchi bungeni ina sikitisha mno.
Ifike wakati sasa wabunge wa CHADEMA wachague moja, kama ni bunge au majukwaa, kwani huwezi kutumikia vyote hivi kwa wakati mmoja.
Hivi sasa bunge la bajeti linaendelea, bunge hili linahitaji umakini na ufanisi wa wabunge ili michango ya wabunge iwe yenye tija na kujenga wanapo ishauri serikali.
Lakini cha kusikitisha wabunge wa CHADEMA wamekuwa 'bize' kwenye majukwaa, hii ina pelekea wabunge wa CHADEMA kukurupuka kuandaa hotuba mbovu na kusababisha gumzo mara kwa mara pindi wanapo ziwasilisha bungeni hotuba zao.
Hivi sasa wabunge wengi wa CHADEMA wamejikita kutetea wagombea udiwani walio wasimamisha kwenye kata zenye uchaguzi mdogo wa udiwani. Mfano Tundu Lissu yuko Morogoro, Godbless Lema yuko Arusha n.k
Nitoe rai kwa CHADEMA, ni wakati sasa chama chenu kikomae, inapaswa chama kiwaache wabunge watekeleze majukumu yao ya msingi pindi bunge linapo kuwa hai, na chama kiunde kikosi kazi maalumu kwa ajili ya kampeni, hasa za chaguzi ndogo.
Pale kwenye red sijakuelewa kabisa! Michango yenye ufanisi ya wabunge wetu ni kama yale ya akina Serukamba, Nkamia, Nchemba au Livingstone? Bungeni wabunge hawajadili bajeti kwa manufaa ya wananchi bali wanaenda kupitisha bajeti kwa niaba ya serikali ndiyo maana majibu yao ni kama ifuatavyo; kifungu hiki kinaafikiwa? Ndiyoooooooooooooooooo, nadhani waliosema ndiyo wameshinda kwa hiyo bajeti ya wizara ya .......imepita, naomba mtoa hoja (waziri husika) aje kutoa hoja.
Kwa hiyo ndg, wabunge wetu hasa wa CCM hawapo kwa ajili ya kuwakilisha wananchi bungeni bali ni wawakilishi wa chama chao na walinzi wa serikali yao bungeni. Ni heri wabunge wa CDM wameamua kurudi majimboni wakifanya kazi ya kuelimisha wanachi juu ya haki yao kuliko hao wanaobaki bungeni wakipitisha bajeti isiyo na tija kwa wananchi. Ni miaka 50 tupate uhuru, bunge lilikuwepo na wabunge wamekuwa wakihudhuria vikao na vikao vya bajeti lakini mbona maisha wa wananchi wanaowawakilisha habadiliki? Uchumi wa Tanzania mbona hauleti unafuu? Serikali mbona imeendelea kufanya kazi kwa mtindo uleule, staili ileile kila mwaka il-hali kuna wabunge wa kuishauri? Kwa kadri ulivyotoa rai kwa CDM na mm natoa rai kwako kwamba kwa sasa Tanzania halina bunge la wananchi bali kuna bunge la vyama vya siasa likisimamiwa na chama tawala (CCM). Bunge hili ni muhuri wa serikali. Ni lazima wananchi tuamue kuunda bunge letu litakalokuwa linajadili maslahi yetu kama walipa kodi na kuachana na hili bunge la vyama vya siasa.