Ushauri wa Shemeji Yangu-Reloaded

Ushauri wa Shemeji Yangu-Reloaded

Carnivora

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2018
Posts
3,650
Reaction score
6,028
Naam habari za usiku wakuu

Leo nataka nihitimishe kisanga kilichotokea kule Kibada. Si mbali sana na pale anapoishi Masanja Mkandamizaji, kwa wanaofaham maeneo ya Kibada.

Mwanzo wa mwezi huu nilileta uzi hapa

Nikaahidi Jumanne yake kumalizia. Kutokana na pilika pilika nikawa sijamalizia. Nilisafiri kidogo nilikwenda county 001 ya Hassan Joho, Mombasa. Ila mpango kazi ulishakamilika siku ile ile.

Haya basi twende kwa usalama.

Jumanne majira ya saa 8 unusu dalali akanipigia to know the plan. Nikamwambia nakuja bila wasi wasi....so niwaambie nao watoke? Jibu ndio. Nilikua na bukta tu ndani baada ya mamsapu kunishibisha pilau naye akianza kusinzia beneath yangu. Nikamwamsha mama twenzetu.

Basi mamsapu akaniweka kushoto mtu mzima nikasinzia kabisa. Tulipofika tulimkuta dalali eneo la tukio akiwa na viongozi wa mtaa na majirani (wanaoshare mpaka). Wauzaji walikua hawajafika. Punde tu boda boda 2 zikaja zikawashusha mama na bintiye. Nilikua nimegeuka upande wa pili nikiongea na mzee 1 ambaye alikua anazungumza habari za siasa zetu nikijifanya sijui kitu. Akinipa story namna anko Magu alivyokuwa anafanya kazi NCU enzi hizo. Namna mzee alivyokuwa mtata na mwenye nyumba wake maeneo ya Nyamanoro jijini Mwanza.

Tukaitwa, tukatoka kuelekea walipo. Mama aliponiona akanichangamkia. Bint naye hakuwa nyuma, alionesha kunifahamu haswaa. Akaniambia nimekuwa bonge...mara akahoji nimefikaje kule? Mara hatujaonana kitambo, naendeleaje. Nilikua serious kidogo nikimjibu kila alichouliza. Vipi nawe kwa upande wako? Jibu lake lilikua "Dah changamoto sana, ila tutaongea usijali." Dalali akatambulisha tuliokuwa pale. Baada ya kusikia mimi ndio mnunuzi akashtuka. "Ina maana H*** (jina langu) ndio nikuuzie wewe?" Akauliza kwa hamaki. Kabla sijajibu, dalali akahoji kwani nyie mnafamiana kivipi? Mama naye ikabidi aingilie kati, "huyu (mimi) siku ile alisema anakujua. Kwani kuna nini?
Mama huyu ndo H*** nlokuwa nakwambiaga kipindi kile. Alijibu.
Akawa mnyonge, na machozi yakimlenga lenga. Alishindwa kujizuia....akalia kwa uchungu. Na sauti yake ikasikika.

Sasa watu wote wakawa wananiangalia mimi. Sikuwa mwenye kusema chochote. Mama akawa anambembeleza bintiye, yule mzee wa story za uncle Magu akasema muache kwanza duku duku ya uchungu imtoke. Ghafla akapata strenght akasema mi siuzi tena nimeghairi, mama tuondoke. Kwanini? Watu wakawa wanahoji. Ikabidi nami niulizwe, kwani we umemfanya nini huyu? Nikawaambia labda aseme yeye mwenyewe, mimi siwezi kusema. Kama ye anafanya siri basi acha ibaki hivyo hivyo siri. Dalali akauliza sasa kuna biashara hapa? Mama akadakia, ipo baba, tutafanya.

Mda wote alikua amejiinamia, alipoinuka akapenga vijikamasi na kufuta machozi akasema anzeni kupima. Mamsapu akawa ameamka na kutoka kwenye gari akaja moja kwa moja kunipa nusu chupa ya maji ambayo alikua anakunywa. Wakasalimiana na yule mama, akampa hi na "mke" mwenzie. Tukapima na baada ya taratibu zote, tukaanza kuelekea ofisi ya serikali ya mtaa akiwa mnyonge kabisa.

Kama kawaida I offered them a ride. Wakakaa back seat. Mke akiwa anaendesha yeye akafunguka ikabidi ajifanye kuchombeza mbona sijamtambulisha wifi? Mara ooh una mke mzuri....na mimi sikuvunga nikamwambia sema tu ukweli kuwa nafasi hii ilikua yako. Mke akanikata jicho. Sijawahi kumwambia habari ya huyu mwanamke na kile kisanga hakukiona. Akampongeza mamsapu kuwa amepata jembe....wakati anashuka akaomba namba. Mamsapu akavuta card moja akampa.

Alivyopandisha tu kioo, swali lililofata kwani yule nani? Nikamueleza. Baadae ikaingia message ya majuto yake kwangu na kunitakia heri mimi na mke wangu. Nikamsomea wifey ndo akazidi kuniamini.

Mtoto mwerevu faida kwa baba yake. Mtoto mpumbavu hasara kwa mama yake.

Shati lile lile la jana ila nimebadilisha gari.

Meraki
 
yule mzee wa story za uncle Magu akasema muache kwanza duku duku ya uchungu imtoke...ah ah ah..
Ungwplay na wimbo za huzuni za kina celine dion type ingependeza..
All in all safi sana mkuu..
Wapenzi wa chess,tunasema CHECKMATE!!!
 
Iiommokjiiiik
Ila na wewe hukufanya vizuri. Kulikuwa hakuna haja ya kumuongezea machungu, ungempa taarifa mapema tu.
To tOlli I kioug, Tokyok the I i lot r not llthe , tuog the first tg I iii to gol,, bet Pou u of my friends list price is a very nice of a sudden and st k
 
Naam. Shati lile lile la jana ila gari nimebadili. MWANA FA hatari sana

Back
Top Bottom