Ushauri wa serikali kwa wanafunzi waliokosa mikopo

Ushauri wa serikali kwa wanafunzi waliokosa mikopo

Rosh Hashannah

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
3,415
Reaction score
2,044
Serikali kupitia Wizara ya elimu, imewataka wanafunzi wote wa elimu ya juu ambao hawajapata mikopo wachangamkie fursa ya kukata rufaa iliyotolewa na bodi ya mikopo kuanzaia jana, Jumatatu, Novemba 13, mpaka jumapili, Novemba 19, mwaka huu.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako aliyasema hayo bungeni jana (Novemba 13) ambapo aliiagiza Bodi ya Mikopo kupitia majina yote ya wanafunzi waliopata na ambao hawajapata mikopo ili kuhakikisha kama mikopo imewafikia walengwa.

“Tayari nimeiagiza Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya mikopo kupitia jina moja baada ya jingine ili kujiridhisha kwamba je, wale waliopangiwa mikopo ndio wenye uhitaji kuliko wale ambao hawjapangiwa lakini pia kupitia majina yote ya wanafunzi ambao hawajapata mikopo ili kujiridhisha kama kweli hawana vigezo kwa mujibu wa vigezo ambavyo vimewekwa,” alisema Waziri Ndalichako.

Aliongeza kuwa sera ya Serikali ni kutoa mikopo kwa wanafunzi wenye uhitaji na siyo kwa wanafunzi wote kama wengi wanavyodhani kwani bado haijafikia kiwango cha kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu.

“Serikali inatekeleza sera ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wenye uhitaji tu…. Sera yetu ya elimu ya juu ni sera ya uchangiaji, hatujafikia mahali ambapo serikali inatoa mikopo kwa wanafunzi wote na ndio maana hata sheria ya bodi ya mikopo imeaninisha wazi kuwa mikopo itatolewa kwa wanafunzi wenye uhitaji. Kwa hiyo kazi ya Wizara yangu ni kusimamia na kuhakikisha kwamba wale wanaopangiwa mikopo ni wenye uhitaji tu na si vinginevyo,” alisema Prof. Ndalichako.

Aidha siku ya Jumatatu, Novemba 13, mwaka huu, bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ilitoa taarifa kuhusu mambo wanayotakiwa kuyafanya wanafunzi wote wanaotaka kukata rufaa kama inavyosomeka hapa chini.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) inapenda kuwataarifu waombaji wote wa mikopo kuwa dirisha la rufaa litafunguliwa kwa siku 7 kuanzia Jumatatu, Novemba 13 hadi Jumapili, Novemba 19, 2017. Waombaji wote wa rufaa wanapaswa kufuata hatua zifuatazo: –

(i) Mwombaji anapaswa kukamilisha taarfa zote katika fomu ya maombi mtandaoni, na kuichapisha, kisha kuambatanisha vielelzo vyote vinavyohitajika au barua inayoeleza sababu za yeye kukata rufaa. Fomu za rufaa mtandaoni zinapatikana kupitia http://olas.heslb.go.tz

(ii) Baada ya kukamilisha kujaza fomu ya maombi ya rufaa, mwombaji anapaswa kuipakua kisha kuambatanisha na nakala ya vyeti vilivyothibitishwa (certified documents) na mamlaka husika kisha kuzifikisha kwa Afisa wa Taasisi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.

(iii) Malalamiko yote yanapaswa kupitishwa na Maafisa wa Bodi ya Mikopo ambao watakusanya fomu zote za kukata rufaa kutoka katika Taasisi zao na kuzifikisha Bodi ya Mikopo Novemba 21, 2017. Bodi haitopokea malalamiko yoyote ambayo yatakusanywa moja kwa moja na mwanafuzi.

(iv) Bodi itapokea na kuchunguza malalamiko yote na pale itakapojiridhisha itarekebisha mkopo au kutoa mkopo mpya kwa waombaji ambao maombi yao ya mikopo yalipigwa awali na Bodi.

Ni nani anayeweza kukata rufaa dhidi ya ugawaji wa Mikopo?

Mbali na vigezo vya jumla vya ustahiki vilivyotolewa katika Miongozo na Vigezo vya utoaji wa Mikopo na Misaada kwa mwaka wa kitaaluma 2017/2018, mwombaji anahitaji kutekeleza yafuatayo:

 Lazima awe mwanafunzi aliyekubaliwa kuanza au kendelea na diploma/shahada katika Taasisi ya Elimu ya Juu ya Tanzania inayokubaliwa.

 Anapaswa kuwa mwanafunzi wa mwaka wa kwanza aliyekuwa ameomba mkopo au mwanafunzi anayeendelea na masomo aliyeomba mkopo kwa mara ya kwanza kwa mwaka 2017/2018 au mwanafuzi anayenufaika na mkopo.

 Wanafunzi ambao hawakuomba mkopo kwa mwaka 2017/2018 hawatakiwi kukata rufaa.

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Novemba 12, 2017
 
si sahihi serikali kusema inatoa mikopo kwa wenye uhitaji tu, si sahihi hata kidg kwan wengi wenye uhitaji hawajapata hio mikopo.........serikali iwe wazi tu iseme kwamba mikopo inatolewa kulingana na uwezo wa kifedha ilionao hapa wangeeleweka,,sasa watu wanakazana kusema kuwa walio na uhitaji ndio wamepata wakati watoto kibao wenye uhitaji wamekosa.........
 
tunakazana kujisifia kutoa elimu bure watoto wa maskini wote wanasoma hawalipi 20,000 ya ada lakin wakifika elimu ya juu ambao ada ni zaidi ya millioni tunawambia hawana uhitaji wa mikopo, kweli?basi angalau tuseme tu kwamba tunatoa mikopo kulingana na ukomo wa bajeti lakin kusema kuwa waliokosa wote hawana uhitaji dah sio vizuri aisee maana si kweli
 
Aliongeza kuwa sera ya Serikali ni kutoa mikopo kwa wanafunzi wenye uhitaji na siyo kwa wanafunzi wote kama wengi wanavyodhani kwani bado haijafikia kiwango cha kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa elimu ya juu.

hatudhani, ndo malengo ya kuundwa kwa HESLB.
nakumbuka tulivyopigwa mabomu na virungu pale mlimani city 2004 tulipoandamana kupinga mswada wa sheria ya kuunda HESLB. tuliona harufu ya rushwa na upendeleo lkn tulipewa majina yote mabaya kuuaminisha umma kuwa tulikuwa wabinafsi, hatukutaka wenzetu nao wapate elimu, n.k. naona yanatimia tuliyokuwa tunasema.
it's so painful. poleni wadogo zangu
 
tungekuwa na bunge makini huyu mama alipaswa kufukuzwa kazi mara moja. kitu chenyewe kinaitwa mkopo bado serikali inawayumbisha wanachuo na mpaka wanshairisha masomo. bunge lilipaswa kuilazimisha serikali iongeze pesa za bodi ya mikopo ili wanafunzi waliokosa wapewe. kwangu mimi wote walioomba mkopo na kupata chuo ni wahitaji wa mkopo.ndalichako kachoka...
 
Back
Top Bottom